Uteuzi wa Maaskofu wapya wa Bubanza na Rutana nchini Burundi
Vatican News
Jumamosi tarehe 15 Februari 2025, Baba Mtakatifu amemteua kuwa Askofu wa Jimbo la Bubanza nchini Burundi, Mhes.Padre Emmanuel Ntakarutimana, O.P.,hadi uteuzi alikuwa ni Mratibu wa Baraza la uundwaji wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Burundi.
Wasifu wake
Mheshimiwa Padre Emmanuel Ntakarutimana, wa Shirika la Wahubiri, alizaliwa tarehe 30 Desemba 1956 katika Jimbo kuu la Gitega. Baada ya masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Bujumbura na Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Kinshasa, Congo, alipata Shahada ya Uzamivu ya Taalimu Msingi katika Chuo Kikuu cha Friborg nchini Uswiss. Alifunga nadhiri zake za kwanza huko Ibadan, Nigeria tarehe 28 Septemba 1981, nadhiri zake za Milele mwaka 1984 huko Rweza (Burundi) na akapewa daraja la Upadre huko Gitega tarehe 23 Agosti 1987.
Alishika nyadhifa zifuatazo: Profesa wa Taalimungua Msingi katika Seminari Kuu ya Gitega (1986-1989); Katibu wa Tume ya Maaskofu ya Haki na Amani (1988-1990); Mwalimu wa Wanafunzi katika NyumMapadre wadominikani (1993-1999); Mratibu wa Kituo cha Ubuntu cha Kukuza Amani na Maridhiano mjini Bujumbura (2001-2015); Mkurugenzi wa Ofisi ya Baraza la Maaskofu la Uinjilishaji (2015-2021); tangu 2021, amekuwa Mratibu wa Baraza la kuundwa kwa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Burundi.
Uteuzi wa Askofu wa Rutana
Baba Mtakatifu amemteua pia Mhesh. Padre Léonidas Nitereka, ambaye hadi uteuzi alikuwa Makamu jimbo la Bururi, kuwa Askofu wa Jimbo la Rutana nchini Burundi.
Wasifu wake
Mhes. Padre Léonidas Nitereka alizaliwa tarehe 1 Septemba 1960 huko Martyazo, katika Jimbo katoliki la Bururi. Mafunzo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu wa Yohane Vianney huko Bujumbura na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane Paulo II huko Gitega.
Alipewa daraja takatifu la Upadre tarehe 17 Agosti 1986 huko Bururi.
Alishika nyadhifa zifuatazo na kumaliza masomo zaidi: Padre msimamizi wa shule za sekondari katika Jimbo (1986-1987); Paroko wa Murago, Jimbo la Bururi (1987-1990); Mchumi wa Jimbo (1990-1997); Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, Roma na Huduma ya Kichungaji katika Jimbo la Firenze, Italia (1997-2006); Mkuu wa Seminari Ndogo ya Buta na Rais wa Baraza la Mapadre wa Bururi(2007-2012); tangu 2010, Makamu Mkuu wa jimbo la Bururi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kichungaji.