Tutakapokuwa wadogo
Andrea Tornielli
Katika Siku ya Wagonjwa Ulimwenguni,(11 Februari) wakati ambapo maswali mengi huzungukia juu ya hatua za mwisho wa maisha, mamilioni ya Waitaliani wanasikiliza, wakiwa na hisia kali, kwa wimbo unaozungumzia utunzaji wa upendo wa mtoto kwa ajili ya mama yake ambaye akili yake imerudi kuwa ya mtoto: "Ni siku nyingine tena na wewe, ili kukurudishia maisha haya yote uliyonipatia na kutabasamu kuhusu wakati na jinsi gani umenibadilisha. Ukiwa mdogo nitakushika sana, hata kutokuweza kuogopa kifo. Wewe utanipa mkono na mimi nitakubusu katika paji la uso."
Kila neno lililoimbwa na Simone Cristicchi kwenye jukwaa la Sanremo linatoa mwonekano wa shukrani na upendo. Linazungumza nasi juu ya maisha, juu ya hadhi ya maisha. Linatuambia juu ya kile ambacho kila mmoja wetu anatamani: kupendwa, kusindikizwa, kuishi vifungo vya mshikamano vikali hasa wakati wa mateso na ugonjwa.
"Wakati utakapokuwa mdogo", anatupendekeza swali hili: tunawezaje kuhakikisha kwamba kila mtu, kiukweli kila mtu, katika kila awamu ya maisha, anasindikizwa na kamwe haachwi peke yake?
Je, hatuhitaji mtu wa kututazama jinsi ambavyo Simone anavyomtazama mama yake, akimpenda licha ya kupungua kutokana na ugonjwa?
Kutunza haimaanishi kuponya kila ugonjwa au kushinda kila udhaifu, lakini ni kujua jinsi ya kumtazama mwingine, kumkaribisha na kumpenda, na hivyo kufanya kila awamu ya maisha kuwa na thamani ya kuishi.