ÐÓMAPµ¼º½

Kanisa Burkina Faso limempata Askofu Mpya Kanisa Burkina Faso limempata Askofu Mpya 

Papa amemteua Askofu Mpya wa Tenkodogo nchini Burkina Faso

Papa Francisko tarehe 6 Februari 2025 amemteua Askofu mpya wa Tenkodogo(Burkina Faso),Mhs Padre David Koudougou,Padre wa Tenkodogo,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Msimamizi wa Jimbo hilo.

Vatican News

Mhesh. Padre David Koudougou alizaliwa tarehe 1 Agosti 1972 huko Tenkodogo na kumaliza majiundo yake ya Falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji huko Wayalghin, Ouagadougou nchini Burkina Faso. Alipewa daraja la Upadre tarehe 14 Julai 2001. Alishika nyadhifa zifuatazo na kukamilisha masomo zaidi: Padre wa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Garango(2001-2002); Padre wa Parokia ya Boussouma (2002-2006); Profesa wa Sheria za Kanoni na katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Peter Claver huko Koumi (2009-2013).

Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma(2013-2016); Padre wa Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Moaga, Afisa wa Mahakama ya Koupèla; Mjumbe wa Baraza la Washauri wa Jimbo Kuu la Koupèla, Katibu Mkuu wa Tume ya Maaskofu wa Mabaraza ya Kikanisa na Masuala ya Kisheria ya Baraza la Maaskofu, Mjumbe wa Maaskofu katika Baraza la Jimbo la Elimu Katoliki Jimbo la Tenkodogo (2017-2023). Tangu 2023 amekuwa Mkuu wa Baraza la Kikanisa na mjumbe wa Baraza la Washauri wa Jimbo la Tenkodogo na Msimamizi wa Mjimbo la Tenkodogo.

Kuongezwa kwa idhini ya uchaguzi wa Mkuu na Makamu wa Baraza la Makardinali

Tarehe 7 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko alitoa kibali alichotoa kwa ajili ya kuchaguliwa kwa Kardinali Giovanni Battista Re kama Dekano wa Baraza la Makardinali. Zaidi ya hayo, tarehe 14 Januari 2025, Baba Mtakatifu aliongeza kibali alichotoa kwa ajili ya kuchaguliwa kwa Kardinali Leonardo Sandri kuwa Makamu Mkuu wa Baraza hilo hilo la Makardinali.

Katibu Msaidizi wa Baraza la kipapa la Uinjilishaji

Baba Mtakatifu amemteua kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji Monsinyo Samuele Sangalli, kuwa na Majikumu ya Utawala wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Maalum Mpya, akimkabidhi cheo binafsi cha kuwa Askofu Mkuu wa Zella.

Ujumuishaji wa Baraza la ushauri la Maaskofu

Baba Mtakatifu amemjumuishaji katika Baraza la ushauri la Maaskofu Kardinali Robert Francis Prevost, O.S.A., ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, huku akimkabidhi pia Kanisa la Albano.

06 Februari 2025, 17:11