Mtaguso wa Nikea,chanzo na mwongozo wa umoja
Na Amedeo Lomonaco – Vatican.
Katika Mwaka huu wa Jubilei uliowekwa wakfu kwa ajili ya matumaini, ukumbusho muhimu sana unajitokeza wa Miaka 1700 iliyopita tangu maadhimisho ya Mtaguso wa kwanza la Kiekumene, ule wa Nikea nchini Uturuki. Hii ni hatua muhimu, kama Papa Francisko anavyosisitiza katikaHati ya kutangaza Jubilei kuu ya 2025. Kwa Wakristo wote inawakilisha tukio la kutambua na kutafuta umoja. Ni mojawapo ya sura kuu katika historia ya Kanisa. Mtaguso huo uliitishwa na Mtawala Konstantino mnamo mwaka 325 na kazi ya kuhifadhi umoja, iliyotishiwa sana kama alivyokumbusha Papa Francisko katika hati ya Spes non confundit yaani, Matumaini hayakatishi tamaa, kwa kutoka kukataa Umungu wa Yesu Kristo na usawa wake na Baba.
Mtaguso wa Nikea uliohudhuriwa na takriban maaskofu 300, wakiwemo wajumbe wa Papa na wawakilishi wa Kanisa la Mashariki, ulilaani uzushi wa Arius. Kutoka katika Mtaguso wa Nikea ndipo unafika mwaliko ambao bado ni muhimu hadi leo hii niule unaoelekezwa kwa Makanisa yote na jumuiya za kikanisa Ulimwenguni"kuendelea katika njia kuelekea umoja." Na Mababa wa Mtaguso kwa mara ya kwanza walitumia usemi wa Sisi tunasadiki.
Mkutano katika hatua mbili
Kumbu kumbu ya kufuatilia miaka 1700 iliyopita kwa hivyo inabaki kuwa chanzo cha kuchota mengi humo. kwa njia hiyo huko Nikea, sala ya Kanuni ya Imani ilianzishwa, ambayo ni msingi wa imani ya kawaida ya Kikristo, na ambayo tunasali kila Dominika ya kiliturujia. Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian kinaadhimisha kumbukumbu ya miaka hii, ambayo inaingiliana na Jubilei kuu ya 2025 na mkutano wenye kauli mbiu: Imani ya Nasadiki ya Mtaguso wa Nikea: Historia na Taalimungu, Mkutano ambao huko kwenye ratiba mjini Roma kuanzia tarehe 27 Februari 2025 hadi tarehe Mosi Machi 2025 katika Chuo Kikuu cha Münster, nchini Ujerumani na kuanzia tarehe 15 hadi 17 Oktoba 2025.
Lengo ni kuhamasisha mazungumzo kati ya utafiti wa kihistoria juu ya Mtaguso wa Nikea na masuala ya Kitaalimungu ya kiutaratibu kuhusu maana ya sasa ya Nasadiki ya Nikea. Tukio lingine limeongezwa kwa mipango ya Maonesho ya: “Of All Things Visible and Invisible”yaani,”Yote yanayoonekana na yasiyoonekana” ambayo unaweza kuyatembelea kuanzia tarehe 27 Februari hadi tarehe 13 Machi 2025. Maonesho haya, yameandaliwa katika maingilio ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Gregorian Roma, na ambayo yanalenga kufahamisha umuhimu wa kitaalimungu wa sanaa kuhusiana na Mtaguso wa Kwanza la kiekumene wa Kanisa. Picha hizo zinaelekea katika jiji la kale la Nikea, ambalo leo hii linaitwa Iznik na liko nchini Uturuki. Ni maeneo ya hija ambayo, katika Mwaka huu Mtakatifu, yanaunganishwa kwa namna ya pekee na Roma, ambapo mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanakutana kwa ajili ya Jubilei ya Matumaini.