MAP

Kumbukizi ya miaka 96 ya kusainiwa Mikataba ya Lateran Makumbaliana na Mkataba wa Mapitio ya Makubaliano kati ya Vatican na Italia (1929-2025). Kumbukizi ya miaka 96 ya kusainiwa Mikataba ya Lateran Makumbaliana na Mkataba wa Mapitio ya Makubaliano kati ya Vatican na Italia (1929-2025).  (ANSA)

Kard.Parolin,Mikataba ya Lateran:Tunatumaini amani na hakuna kufukuzwa Wapalestina

Katibu wa Vatican akiwa pembezoni mwa hafla ya kumbukizi ya Mikataba ya Lateran katika Jumba la Borromeo,jiji Roma alisema:wale waliozaliwa na kukulia Gaza lazima wabaki katika ardhi yao wenyewe.Kuhusu Ukraine,alionesha matumaini kwamba kuna mwanga wa matumaini ya kujaribu kumaliza vita,lakini amani lazima iwe ya haki na kudumu.Suala la wahamiaji lilishughulikiwa:Itifaki za ushirikiano zinahitajika.Mwisho wa maisha ni mada ya kujadiliwa mahali pengine.

Na Alessandro Guarasci – Roma.


Ulinzi wa familia, migogoro ya kimataifa, kuanzia Mashariki ya Kati hadi Ukraine, wahamiaji. Haya ni baadhi ya masuala yaliyoshughulikiwa jioni ya tarehe 13 Februari 2025, katika mkutano wa kilele kati ya Italia na Vatican katika Jumba la Borromeo mjini Roma wakati wa Hafla ya maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 96 tangu kutiwa saini ya Mikataba ya Lateran kunako 1929 – 2025. Viongozi wakuu wa taasisi walikuwepo, akiwemo Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella na Waziri Mkuu, Bi Giorgia Meloni.

Suluhisho la Mashariki ya Kati linabaki kuwa la mataifa mawili

Vatican daima iko makini na kile kinachotokea Gaza. Idadi ya Wapalestina lazima iweze kubaki katika ardhi yake: "Hakuna kufukuzwa na hii ni moja ya mambo msingi," alisema hayo Kardinali Parolin akiwa kando ya hafla hiyo akihojiwa na waandishi wa habari. "Kuna mtu wa upande wa Italia alisisitiza jinsi ambavyo jambo hili lingeweza kuleta mvutano katika eneo hilo. Nchi jirani hazipatikani, kwa mfano tulimsikia Mfalme wa Jordan hivi karibuni akisema 'hakuna kabisa, tunahitaji kutafuta suluhisho na kwa maoni yetu, ni ya Mataifa hayo mawili kwa sababu hii ina maana pia kutoa matumaini kwa wakazi,” alisema Katibu wa Vatican kuhusiana na suala lililoibuliwa na Rais mpya wa Marekani hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Bwana Antonio Tajani, pia aliweka wazi kwamba hali hiyo inaweza kubadilika, akisisitiza kwamba kuna baadhi ya mwanga chanya wa matumaini ya kusonga mbele: "Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa mapatano hayo yanaimarishwa, kwa hivyo ninataka kutumaini kwamba mateka wataachiliwa. Na kwa upande wa Ukraine Waziri Tajani, aliongeza kusema kuwa “EU na Kyiv lazima zihusishwe katika mazungumzo hayo.”

Kwa Ukraine Amani ya Haki

Diplomasia inachukua hatua kwa Ukraine, pia kwa kuzingatia simu ya hivi karibuni kati ya Rais Trump, wa Marekani na Rais Putin, wa Urusi. Kardinali Parolin alisema kwamba "tunahitaji amani ya haki na na kuna harakati nyingi na fursa nyingi. Tunatumaini ni kwamba yatatokea na tunatumaini kuwa tunaweza kufikia amani ambayo, ili kuwa thabiti, ya kudumu, lazima iwe na amani ya haki, inayohusisha wahusika wote ambao wako hatarini na kwa kuzingatia kanuni za sheria za kimataifa na matamko ya UN. Kila kitu kinachopendekezwa ni muhimu kwa sababu lazima tukomeshe mauaji haya."”

Sheria ya Kusaidiwa ya kujiua ya huko Toscana nchini Italia

Mada ya kujiua kwa kusaidiwa, ambayo mara baada ya sheria ya hivi karibuni ya Mkoa wa Toscana nchini Italia haikuguswa, lakini hata hivyo inaweza kushughulikiwa katika matukio mengine. Kwa upande wa Waziri Tajani aliingilia kati suala hilo na alipoulizwa iwapo sheria hiyo itapingwa alijibu: “Ni suala la umahiri wa taifa, tutalizungumzia, lakini cha ajabu wale ambao wanapinga uhuru wa kujitawala basi wanataka kutunga sheria ya Toscana ya kusaidiwa kujiua, na si katika mkoa mwingine. Ikiwa ni juu yangu, ndiyo, lakini tutazungumza juu yake. Sio suala la umahiri wa kikanda, tunahitaji umahiri wa kitaifa juu ya mada hii." Kwa kutaja pia kwa mada ya wahamiaji. Kardinali Parolin aliripoti kwamba mkutano wa pande mbili ulijadili mapokezi na ushirikiano kwa ajili ya kupokea na kuunganisha wahamiaji nchini Italia. Kanisa linafanya mengi, itifaki za ushirikiano zinahitajika katika ngazi ya kikanda."

Mahojiano na Kard. Parolin
14 Februari 2025, 16:35