Hivi ndivyo Tumaini la Jubilei likuwa thabiti!
Andrea Tornielli
Ufunguzi wa Mlango Mtakatifu wa Jubilei uliofunguliwa mnamo tarehe 24 Desemba, ambao ulikuwa umetanguliwa na masaa machache kabla, kwa maamuzi ya Rais wa Marekani Joe Biden, kuwaachilia, wafungwa 37 waliohukumiwa kifo katika magereza ya Shirikisho. Mwanzoni mwa Januari, zaidi ya habari mbili ni nzuri: huko Carolina Kaskazini, mkuu wa mkoa alitoa agizo lake la kubadilisha hukumu ya kifo kwa kifungo cha maisha kwa wafungwa 15 waliokuwa chini ya serikali yake na wakati huo huo huko Afrika, Rais wa Zimbabwe, aliondoa hukumu ya kifo kutoka katika kifungu cha sheria ya Nchi. Na sasa katika mwanzo wa Mwaka Mtakatifu, tangazo limefika la kuwaachia huru wafungwa 553 nchini Cuba.
Tunahitaji sana ishara za matumaini ambazo zinatusaidia kuinua mtazamo kutoka katika huzuni wa mandhari ya vita na vurugu: hapangekuwa na mwanzo mzuri zaidi wa mwaka huu wa neema kwa sababu ni habari inayounganisha Jubilei ya Kikristo na asili yake ya kibiblia, kama vile Papa Francisko alivyokumbusha katika Waraka wake wa kutangaza Jubilei hii iutwao: "Spes non confundit," maana yake “Matumaini hayakatishi tamaa” kwamba: “Ninapendekeza kwa serikali kwamba katika Mwaka wa Jubilei wachukue hatua zinazorudisha matumaini; aina za msamaha au ondoleo la hukumu zinazolenga kuwasaidia watu kurejesha imani ndani yao na katika jamii; njia za ujumuishaji upya wa jumuiya zinazolingana na dhamira thabiti ya kufuata sheria.”
Huu ni wito wa kizamani, alieleza Askofu wa Roma huku akinukuu maneno katika Kitabu cha Walawi kwamba: “linatokana na Neno la Mungu na kubaki na thamani yake yote ya hekima katika kuomba matendo ya huruma na ukombozi ambayo huturuhusu kuanza tena: “Mtautangaza mwaka wa hamsini kuwa mtakatifu, nanyi mtatangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote.” Msamaha, ondoleo la adhabu, huruma huambatana na maneno mawili muhimu ya kila Jubilei ambayo ni huruma na msamaha. Ulimwengu wetu unauhitaji zaidi kuliko hapo awali.