ÐÓMAPµ¼º½

Papa amemteua Askofu Mpya wa Jimbo Jipya la Alto Molócuè nchini Msumbiji, Padre Estêvão Ângelo Fernando. Papa amemteua Askofu Mpya wa Jimbo Jipya la Alto Molócuè nchini Msumbiji, Padre Estêvão Ângelo Fernando. 

Papa Francisko ameunda Jimbo jipya la Alto Molócuè,Msumbiji na kumteua Askofu wake wa kwanza

Papa ameunda Jimbo jipya Alto Molócuè nchini Msumbiji kwa kulimega Jimbo Katoliki la Gurúè na Quelimane na kulifanya kuwa mshiriki wa Jimbo Kuu la Nampula na wakati huo huo kumteua Askofu wake wa kwanza,Mheshimiwa Padre Estêvão Ângelo Fernando,wa Quelimane.Alizaliwa tarehe 17 Juni 1974,huko Quelimane.

Na Angela Rwezaula

Alhamisi tarehe 23 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko   ameunda Jimbo jipya la Alto Molócuè nchini Msumbiji kwa kulimega Jimbo Katoliki la Gurúè na Quelimane na kulifanya kuwa mshiriki wa Jimbo Kuu la Nampula na wakati huo huo kumteua Askofu wake wa Kwanza, Mheshimiwa  Padre Estêvão Ângelo Fernando, wa huko  Quelimane.

Wadhifa

Monsinyo  Estêvão Ângelo Fernando alizaliwa mnamo Juni 17, 1974, huko Inhassunge,Jimbo la  Quelimane. Baada ya Mafunzo ya  Seminari ya Maandalizi ya Mtakatifu Agostino huko Quelimane, aliendelea na Seminari ya Falsafa ya Mtakatifu  Agostinho huko Matola na, baadaye, Seminari ya Kitaalimungu ya Mtakatifu Pio X huko Maputo, na kupata digrii ya Shahada.

Alipewa daraja la Upadre tarehe 24 Juni 2001.

Alishika nyadhifa zifuatazo na kukamilisha masomo zaidi

Padre wa  Parokia na kisha Paroko wa Mocuba (2001-2006); Mjumbe wa Tume ya Wakimbizi Kusini mwa Afrika (2002-2006); Mkurugenzi wa Kiroho wa Harakati ya Kitume ya Xaveri (2003-2010); Mkuu wa Seminari ya Maandalizi ya Mtakatifu  Agostino ya Quelimane (2007-2010); Rais wa Tume ya Mawasiliano ya Quelimane (2010-2011); Mshiriki katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mkuu  huko Cordenons, Jimbo la  Concordia-Pordenone nchini  (Italia) (2011-2014); Leseni katika Taalimungu ya Kichungaji katika Kitivo cha Taalimungu cha Triveneto huko Padova (2014); Mshiriki katika Parokia ya Mtakatifu Francis wa Assisi huko Pordenone, Jimbo la  Concordia-Pordenone (Italia) (2015-2019); Mkufunzi katika Seminari ya Falsafa ya Mtakatifu o Agostino huko Matola (2020-2021); Shahada ya Uzamivu katika Talimungu  ya Kichungaji, katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma. Tangu 2022 amekuwa Mkufunzi na katika Seminari  Falsaf ya Mtakatifu Carlos Lwanga huko Nampula.

Takwimu za  Majimbo

Wilaya zifuatazo za kiraia zinaunda eneo la Jimbo jipya la Alto Molócuè (Molócuè Superioris): Mocubela, Pebane, Gilé, Mulevala na Alto Molócuè.

Jimbo jipya la kikanisa ni mshiriki wa Jimbo kuu la Nampula. Kiti cha Makao ya Jimbo  ni mji wa Alto Molócuè. Kanisa la parokia lililowekwa wakfu kwa Nossa Senhora Rainha do Mundo linakuwa Kanisa kuu la Jimbo Jipya.

Ifuatayo ni  takwimu inayohusiana na dMajimbo yota mawili  mama (Gurúè na Quelimane), baada ya kugawanywa, na Jimbo  jipya la Alto Molócuè:

 

  Gurúè

  Quelimane

  Alto Molócuè

Ukubwa

   18. 578 km2

  57.798 km2

  28.632 km2

Watu

  1.255.736

  3.440.268

  1.199.649

Wakatoliki

  559.783

  1.366.593

487.465

Parokia

  12

  29

  14

Padre Kijimbo

  24

  52

  21

Mapadre watawa

  9

  21

  11

Waseminari

  18

  45

  16

Watawa/sio mapadre

  0

  7

  2

Watawa/kike

  37

  98

  26

 

23 Januari 2025, 12:57