Papa Francisko ameunda Jimbo jipya la Alto Molócuè,Msumbiji na kumteua Askofu wake wa kwanza
Na Angela Rwezaula
Alhamisi tarehe 23 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko ameunda Jimbo jipya la Alto Molócuè nchini Msumbiji kwa kulimega Jimbo Katoliki la Gurúè na Quelimane na kulifanya kuwa mshiriki wa Jimbo Kuu la Nampula na wakati huo huo kumteua Askofu wake wa Kwanza, Mheshimiwa Padre Estêvão Ângelo Fernando, wa huko Quelimane.
Wadhifa
Monsinyo Estêvão Ângelo Fernando alizaliwa mnamo Juni 17, 1974, huko Inhassunge,Jimbo la Quelimane. Baada ya Mafunzo ya Seminari ya Maandalizi ya Mtakatifu Agostino huko Quelimane, aliendelea na Seminari ya Falsafa ya Mtakatifu Agostinho huko Matola na, baadaye, Seminari ya Kitaalimungu ya Mtakatifu Pio X huko Maputo, na kupata digrii ya Shahada.
Alipewa daraja la Upadre tarehe 24 Juni 2001.
Alishika nyadhifa zifuatazo na kukamilisha masomo zaidi
Padre wa Parokia na kisha Paroko wa Mocuba (2001-2006); Mjumbe wa Tume ya Wakimbizi Kusini mwa Afrika (2002-2006); Mkurugenzi wa Kiroho wa Harakati ya Kitume ya Xaveri (2003-2010); Mkuu wa Seminari ya Maandalizi ya Mtakatifu Agostino ya Quelimane (2007-2010); Rais wa Tume ya Mawasiliano ya Quelimane (2010-2011); Mshiriki katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mkuu huko Cordenons, Jimbo la Concordia-Pordenone nchini (Italia) (2011-2014); Leseni katika Taalimungu ya Kichungaji katika Kitivo cha Taalimungu cha Triveneto huko Padova (2014); Mshiriki katika Parokia ya Mtakatifu Francis wa Assisi huko Pordenone, Jimbo la Concordia-Pordenone (Italia) (2015-2019); Mkufunzi katika Seminari ya Falsafa ya Mtakatifu o Agostino huko Matola (2020-2021); Shahada ya Uzamivu katika Talimungu ya Kichungaji, katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma. Tangu 2022 amekuwa Mkufunzi na katika Seminari Falsaf ya Mtakatifu Carlos Lwanga huko Nampula.
Takwimu za Majimbo
Wilaya zifuatazo za kiraia zinaunda eneo la Jimbo jipya la Alto Molócuè (Molócuè Superioris): Mocubela, Pebane, Gilé, Mulevala na Alto Molócuè.
Jimbo jipya la kikanisa ni mshiriki wa Jimbo kuu la Nampula. Kiti cha Makao ya Jimbo ni mji wa Alto Molócuè. Kanisa la parokia lililowekwa wakfu kwa Nossa Senhora Rainha do Mundo linakuwa Kanisa kuu la Jimbo Jipya.
Ifuatayo ni takwimu inayohusiana na dMajimbo yota mawili mama (Gurúè na Quelimane), baada ya kugawanywa, na Jimbo jipya la Alto Molócuè:
|
Gurúè |
Quelimane |
Alto Molócuè |
Ukubwa |
18. 578 km2 |
57.798 km2 |
28.632 km2 |
Watu |
1.255.736 |
3.440.268 |
1.199.649 |
Wakatoliki |
559.783 |
1.366.593 |
487.465 |
Parokia |
12 |
29 |
14 |
Padre Kijimbo |
24 |
52 |
21 |
Mapadre watawa |
9 |
21 |
11 |
Waseminari |
18 |
45 |
16 |
Watawa/sio mapadre |
0 |
7 |
2 |
Watawa/kike |
37 |
98 |
26 |