Papa ameridhia kuwatangaza watakatifu watawa 6,mashahidi wa Amerika Kaskazini na Hispania
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati wa Mkutano uliofanyika Jumatatu tarehe 27 Januari 2025 kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Papa aliidhinisha Baraza hilohilo kutangaza Amri kuhusu: muujiza wa Mwenyeheri Vincenza Maria Poloni, Mwanzilishi wa Taasisi ya Masista wa Huruma, aliyezaliwa Verona tarehe 26 Januari 1802 na kufariki tarehe 11 Novemba 1855.
Kuuawa kwa imani kwa Watumishi wa Mungu Petro wa Corpa na wenzake wanne, wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafranciskani (OFM)waliouawa kwa chuki mnamo Septemba 1597 huko Florida, sasa Georgia (Marekani);
Kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Licarione May (kwa jina ni Francesco Beniamino), Ndugu wa Taasisi ya Mabruda wa Shule wa Marist, aliyezaliwa Bagnes (Switzerland) tarehe 21 Julai 1870 na kuuawa kwa chuki ya imani mnamo tarehe 27 Julai 1909 huko Barcelona( Hispania;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Riccarda wa Damu ya Thamani Zaidi Beauchamp Hambrough (kwa jina Caterina), Abasia kuu ya Shirika la Mwokozi Mtakatifu zaidi wa Mtakatifu Bridget, aliyezaliwa mnamo tarehe 10 Septemba 1887 huko London na akafa mnamo 26 Juni 1966, Roma;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Quintino Sicuro, Padre wa jimbo. Alizaliwa tarehe 29 Mei 1920 huko Melissano (Italia) na kufariki tarehe 26 Desemba 1968 kwenye njia ya kuelekea Mlima Fumaiolo ya Verghereto (Italia);
Hatimaye fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Luigia Sinapi, mwamini mlei, aliyezaliwa tarehe 8 Septemba 1916 huko Itri (Italia) na kufariki tarehe 17 Aprili 1978,jijini Roma.