Papa amemteua Mons.Maurizio Bravi kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na visiwa vya Solomon
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatano tarehe 15 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na katika visiwa vya Solomon, Monsinyo Maurizio Bravi, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirika la Utalii Duniani (O.M.T.), Roma kwa kumpatia moja kwa moja ya kiti cha Kanisa la Tolentino, kwa hadhi ya Uaskofu Mkuu.
Wadhifa
Monsinyo Maurizio Bravi alizaliwa huko Capriate Mtakatifu Gervasio (Bergamo),Italia tarehe 20 Julai 1962. Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 21 Juni 1986, kwa ajili ya Jombo la Bergamo. Katika mafunzo yake analipata shahada ya Sheria ya Kanoni. Alijiunga katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican kunako tarehe 1 Julai 1995 na kujikita katika shughuli za uwakilishi wa Kipapa katika Jamhuri ya Dominika na Argentina, katika kitengo cha Vatican cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa na baadaye katika Ubalozi wa Kitume huko Ufaransa na Canada. Aliteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Kimataifa ya Utalii(O.M.T.), kunako tarehe 27 Februari 2016. Anajua Kiingereza, kifaransa na kispanyola.