Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Malta
Vatican News
Tarehe 24 Januari 2025 Baba Mtakatifu Francisko alikuta na Rais wa Jamhuri ya Malta, Bi Myriam Spiteri Debono, katika mkutano wao wa Mazungumzo ya faragha yalifanyika katika Ukumbi wa Jumba la kitume, akisindikizwa na mume wake na wasaidizi wake. Mkutano huo ulidumu kwa dakika 20 katika Maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican.
Mwishoni, baada ya uwasilishaji wa wajumbe wa Malta, kulikuwa na kubadilishana zawadi. Papa alitoa mchongo mmoja wa udogo unaoitwa Upole na Upendo, vile vile wingi wa nyaraka za Papa, Ujumbe wa Siku ya Amani ya Dunia mwaka huu 2025, uliotiwa saini naye, na Kitabu cha picha ya Jumba Kitume.
Bi Spiteri Debono alijibu zawadi kwa Papa chombo cha Tecartherapy ambacho kitaruhusu matibabu ya (physiotherapy) mazoezi ya viungo na ukarabati wa kimwili kwa watu wasio na makazi, kwa lengo la kupunguza kuvimba na maumivu katika aina za magonjwa makuu kama yale ya mishipa ambayo ni za kawaida sana kwa watu hawa kutokana na maisha yao magumu. Kifaa kitatumwa kwa Idara ya Huduma ya Kliniki ya Wagonjwa ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo. Pia alitoa kikapu cha bidhaa za kawaida za utamaduni wa Malta.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
Baada ya mkutano na Papa, Rais wa Malta na wasaidizi wake walikwenda kwenye Sekretarieti ya Vatican ambako walikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican inabainisha kuwa“Wakati wa mazungumzo yao walionesha kupongezana na kushukuru kwa pande zote kwa uhusiano thabiti wa nchi mbili kati ya Vatican na Malta, ikithibitisha tena dhamira ya kuimarisha zaidi ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya kawaida."
Katika muendelezo wa mazungumzo masuala kadhaa ya umuhimu wa kimataifa yalishughulikiwa, kwa kuzingatia hasa hali ya eneo la Mediterania, migogoro ya Israeli na Palestina, mgogoro wa Ukraine, pamoja na changamoto zinazohusiana na uhamiaji".