杏MAP导航

Tafuta

2025.01.24 Bi Myriam Spiteri Debono, Rais wa Jamhuri ya Malata amekutana na Papa. 2025.01.24 Bi Myriam Spiteri Debono, Rais wa Jamhuri ya Malata amekutana na Papa.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Malta

Papa alikutana na Myriam Spiteri Debono katika Jumba la Kitume mjini Vatican pamoja na wasaidizi wake.Mazungumzo ya faragha na Papa yalidumu kwa dakika 20,mwisho ilikuwa ni kubadilishana zawadi.Katika mazungumzo na Sekretarieti ya Vatican,yamezingatia hali ya Bahari ya Mediterania,migogoro ya Mashariki ya Kati na Ukraine na changamoto za uhamiaji.

Vatican News

Tarehe 24 Januari 2025 Baba Mtakatifu Francisko alikuta na Rais wa Jamhuri ya Malta, Bi Myriam Spiteri Debono, katika mkutano wao wa Mazungumzo ya faragha yalifanyika katika Ukumbi wa Jumba la kitume, akisindikizwa na mume wake na wasaidizi wake. Mkutano huo ulidumu kwa dakika 20 katika Maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican.

Papa na rais wa Malta na wasindikizaji wake
Papa na rais wa Malta na wasindikizaji wake   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mwishoni, baada ya uwasilishaji wa wajumbe wa Malta, kulikuwa na kubadilishana zawadi. Papa alitoa mchongo mmoja wa udogo unaoitwa Upole na Upendo, vile vile wingi wa nyaraka za Papa, Ujumbe wa Siku ya Amani ya Dunia mwaka huu 2025, uliotiwa saini naye, na Kitabu cha picha ya Jumba Kitume.

Kubadilishana zawadi
Kubadilishana zawadi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Bi Spiteri Debono alijibu zawadi kwa Papa chombo cha Tecartherapy ambacho kitaruhusu matibabu ya (physiotherapy) mazoezi ya viungo na ukarabati wa kimwili kwa watu wasio na makazi, kwa lengo la kupunguza kuvimba na maumivu katika aina za magonjwa makuu kama yale ya mishipa ambayo ni za kawaida sana kwa watu hawa kutokana na maisha yao magumu. Kifaa kitatumwa kwa Idara ya Huduma ya Kliniki ya Wagonjwa ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo. Pia alitoa kikapu cha bidhaa za kawaida za utamaduni wa Malta.

Zawadi
Zawadi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican

Baada ya mkutano na Papa, Rais wa Malta na wasaidizi wake walikwenda kwenye Sekretarieti ya Vatican ambako walikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican  inabainisha kuwa“Wakati wa mazungumzo yao walionesha kupongezana na kushukuru kwa pande zote kwa uhusiano thabiti wa nchi mbili kati ya  Vatican na Malta, ikithibitisha tena dhamira ya kuimarisha zaidi ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya kawaida."

Mkutano wa Rais wa Malta na Sekretarieti ya Vatican
Mkutano wa Rais wa Malta na Sekretarieti ya Vatican   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Katika muendelezo wa mazungumzo masuala kadhaa ya umuhimu wa kimataifa yalishughulikiwa, kwa kuzingatia hasa hali ya eneo la Mediterania, migogoro ya Israeli na Palestina, mgogoro wa Ukraine, pamoja na changamoto zinazohusiana na uhamiaji".

24 Januari 2025, 17:04