ÐÓMAPµ¼º½

Papa alikutana na kiongozi wa Panama Papa alikutana na kiongozi wa Panama 

Papa akutana na marais wa Panama na Haiti

Jumamosi tarehe 25 Januari 2025,Papa amekutana katika Jumba la Kitume na José Raul Mulino Quintero,Kiongozi wa Panama na Leslie Voltaire,mkuu wa Baraza la Urais wa Mpito la Haiti.Baadaye walifanya mazungumzo katika Sekretarieti ya Vaticanambapo pamoja na kiongozi wa Panama walizingatia masuala ya ulinzi wa mazingira,uhamiaji,kijamii na kisiasa na kwa upande wa Haiti walirejea hali ya nchi,masuala ya usalama katika uwanja wa kibinadamu na wahamiaji.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko alikuwa na mikutano miwili  ya viongozi wa Nchi, Jumamosi  tarehe 25 Januari 2025, kwanza kabisa na Rais wa Jamhuri ya Panama, Bwana José Raul Mulino Quintero, kisha na Rais wa Baraza la Mpito la Haiti, Leslie Voltaire, wote walipokelewa katika Jumba la Kitume mjini Vatican.

José Raul Mulino Quintero

Quintero alikuwa na mazungumzo ya faragha na Papa kuanzia sa 2:05 hadi 2:35, asubuhi na kufuatiwa na kubadilishana zawadi. Kutoka kwa Papa, Zawadi ya Mfinyanzi   yenye jina la "Upole na Upendo Kitabu cha  hati za upapa, Ujumbe wa Amani wa mwaka 2025, kitabu cha Njia ya Msalaba Statio Orbischa tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV, Kitabu cha Picha za  Nyumba ya kipapa kilichohaririwa na Msimamizi wa Nyumba ya Kipapa. Mkuu wa nchi alijibu zawadi hizo kwa kiasi fulani cha picha kwenye Mfereji wa Panama na medali ya ukumbusho ya Urais.

Kiongozi wa Panama
Kiongozi wa Panama   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Katika Sekretarieti ya Vatican,  Mulino Quintero alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akifuatana na Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. "Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti, taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican  inabainisha kuridhika kwa uhusiano mzuri kati ya Panama na  Vatican.

Kiongozi wa Panama na Katibu wa Vatican
Kiongozi wa Panama na Katibu wa Vatican   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kwa upande wa  Leslie Voltaire

Saa 3.30, asubuhi  alikuwa na kikao na Voltaire, mkuu wa Baraza la uongozi la mpito  la Haiti (yenye majukumu ya Urais wa Jamhuri), iliyoundwa baada ya uasi wa magenge mnamo 2024. Awali walianza na mazungumzo ya faragha  kati ya Papa Kiongozi wa Haiti. Na baadaye walibadilishana zawadi : Jani la shaba lenye kichwa "Mazungumzo kati ya vizazi", kitabu cha  hati za papa, Ujumbe wa Amani wa mwaka 2025 , kitabu cha Statio Orbis Njia ya Msalaba cha 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV, Kitabu cha Picha zinazoonesha Ghorofa za Kipapa, kimehaririwa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa na wakati huo Rais alimpa Papa baadhi ya vitabu vya picha kuhusu Haiti.

Papa alikutana na kiongozi wa Haiti
Papa alikutana na kiongozi wa Haiti   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Voltaire pia alihamia Sekretarieti ya Vatican  katika mkutano na Kardinali Parolin na Askofu Mkuu Gallagher. "Wakati wa majadiliano ya dhati kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican inaarifu  kuridhika kwa uhusiano mzuri kati ya Haiti na Vatican.

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kisha waliakisi mchango wa thamani ambao Kanisa hutoa kwa nchi, licha ya matatizo yaliyosababishwa na mgogoro wa sasa. Katika muendelezo wa mazungumzo hayo - taarifa kwa vyombo vya habari - baadhi ya masuala ya sasa nchini Haiti yaliguswa, kama vile hali ya kijamii na kisiasa ya nchi hiyo, usalama, matatizo ya kibinadamu na wahamiaji, na hatua zinazochukuliwa kutafuta suluhisho kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa."

25 Januari 2025, 15:45