Kard.Parolin: Kutangazwa kuachiliwa kwa wafungwa wa Cuba ni ishara ya matumaini makubwa
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akihojiwa na vyombo vya habari vya Vatican alipokuwa nchini Ufaransa kuhusiana na taarifa ya Havana alisema kuwa: "Habari za kuachiliwa polepole kwa wafungwa 553 wa Cuba ni ishara ya matumaini makubwa mwanzoni mwa Jubilei hii. Ni muhimu kwamba mamlaka ya Havana wameunganisha uamuzi huu moja kwa moja na wito wa Papa ambazo zimetokea mara kadhaa wakati wa Mwaka Mtakatifu."
Katibu wa Vatican aidha aliongeza kusema: "Mwaka 2024 ulimalizika kwa Rais wa Marekani kubadilisha makumi ya hukumu za kifo hadi kifungo cha maisha, na kwa habari kwamba Zimbabwe ilikuwa imefuta hukumu ya kifo. Tunatumaini kuwa 2025 itaendelea katika mwelekeo huu na kwamba habari njema itaongezeka, hasa kwa kusitishwa kwa migogoro mingi ambayo bado inaendelea."