Jubilei ya Wanawasiliano:Mbegu za Matumaini za kufanya Ukweli uchanue
Vatican News
Maadhimisho hayo kwa heshima ya Mtakatifu Francis wa Sales Msimamizi wa wanahabari, yalianza na Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano, ikiwa ni tukio la kwanza kati ya matukio makuu yaliyoandaliwa kwa Mwaka Mtakatifu 2025. Kwa njia hiyo tarehe 24 Asubuhi katika Ofisi ya Habari ya Vatican, mbele ya Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya kimsingi ya Uinjilishaji katika ulimwengu cha Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, na katibu wake Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, shughuli mbalimbali zitakazohuisha siku hizi ziliwasilishwa. Pia walikuwepo katika Chumba cha Waandishi wa Habari mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, mwanahabari Maria Ressa, na mwandishi Colum McCann, ambao ni wageni vile vile katika mkutano wa kiutamaduni katika Ukumbi wa Paul VI.
Fischella: Changamoto ya matumaini
"Jubilei hii ya Mawasiliano ni uzoefu wa wanadamu wote: ikiwa unaishi uzoefu wa kibinafsi unaweza pia kuwaambia wengine kwa njia bora zaidi. Hili ndilo kusudi: wawasilianaji ndio wa kwanza wanaohusika na kushiriki chanya, uzuri na kiroho na wengine. Kwa hivyo wataweza kutoa maelezo madhubuti yake mwaka mzima." Hayo yalizungumzwa na Monsinyo Fisichella, ambaye kulingana naye matumaini ya kuwasiliana yanawakilisha changamoto kubwa: “Hata wasanii hawajaweza kutoa uso wa matumaini. Uwakilishi pekee tulio nao ni ishara ya Kikristo ambayo ni nanga. Nanga hiyo inatoka katika kifungu katika Agano Jipya, lakini inapata uthibitisho katika maficho ya wakristo wa kwanza: hiyo ndiyo ishara ya tumaini katika uso wa kifo. Kuwasiliana kwamba licha ya vurugu na kifo, licha ya uovu unaotuzunguka kila siku, tuna uhakika wa tumaini ambalo halikatishi tamaa, na inamaanisha kuwa mema yatashinda daima."
Simulizi ya historia
Na kwa maoni Dk. Ruffini alibainisha kuwa: "Labda tunahitaji kurejea kwenye mizizi ya wito wetu, dhamira yetu, ya mapenzi yetu kwa taaluma hii ya waandishi wa habari na wanahabari. Hatujaishia katika hali mbaya, lakini labda tumejipoteza kidogo. Njia isiyo na mapito ambayo sisi sote tunawasiliana, lakini hatuelewani kila mmoja. Tukio hili linaweza kuwa wakati wa kuzaliwa upya, kwa waandishi wa habari lakini sio hilo tu. Hasa katika enzi ambayo tunaishi katika ulimwengu ambapo kila mtu ni mwasiliani, ambapo mawasiliano yamo ndani ya dhana ya kiteknolojia na ambayo labda yanahitaji kufikiria upya ili kurejesha uzuri wa kushiriki. Ni wakati wa kufikiria upya baadhi ya mambo, tuna wakati wa kutafuta njia ya mawasiliano tena.” Kwa Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, anabainisha: “tumefumwa na historia ambazo wazazi wetu walitusimulia tulipokuwa watoto; historia ya nchi yetu; historia za familia zetu; na historia tulizopitia.” Kadhalia alisema kuwa “ Kusimulia historia zinazohamasisha mienendo mizuri husaidia kubadilisha mambo. Hii ndiyo sababu pia tulianzisha lebo ya #hopetelling: hebu tuunganishe mtandao unaosimulia historia ya matumaini na tuone kitakachotokea.”
Ulimwengu wa ukweli
Kwa njia hiyo, Jubilei, kama muda wa kuwasilisha tumaini, kwamba haiwi “kitu kilichowekwa kwa ajili ya kila mmoja wetu; Badala yake, ni kitu tunachopokea ili kuwapa wengine. Ili ulimwengu wote, kama Papa asemavyo, uweze kuelewa tumaini hili litokalo kwa Mungu Nenda kwa wengine na ukweli unaoweza kuwasilishwa na kupanda tumaini. Hayo yalisisitizwa na Monsinyo Ruiz jinsi ilivyo muhimu “kuchukua chembe hizi za matumaini ambazo zipo katika uhalisia ili ziwe mishono inayosuka historia. Ikiwa kila mtu, angeweza kufanya hivyo kutoka katika ukweli mdogo wa kila siku hadi ukweli mkuu wa ulimwengu, angeweza kutazama ukweli na matumaini, mahusiano yangekuwa tofauti kabisa. Hiki ni kidogo cha wito wa Papa Francisko na maana ya Jubilei ya Mawasiliano ya kuweza kupanda matumaini ya kuunda ulimwengu unaotuongoza mbele katika ukweli."