ĞÓMAPµ¼º½

2025.01.24 Kardinali Reina aliongoza misa ya ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano. 2025.01.24 Kardinali Reina aliongoza misa ya ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Jubilei ya Mawasiliano:kushiriki matumaini kwa upole na fadhila kuu ya utume

Maadhimisho ya Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano yalifunguliwa kwa adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Francis wa sales,Msimamizi wa wahandishi,katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane,Laterano.Kardinali Reina:Kristo aliondoa silaha ya kiburi na ili kuondoa silaha za mawasiliano ni lazima tuondoe kwanza kiburi chetu.Padre Albanese,Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kijamii ya Vikarieti ya Roma aliongoza liturujia ya Toba.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ufunguzi wa Jubilei uliakisi zana mbili muhimu kwa kila mwanahabari: moyo na matumaini. Maadili haya yalijidhihirisha katika nyakati mbili za uzinduzi wa maadhimisho haya,ambapo kulikuwa na Liturujia ya toba, iliyoongozwa na Padre Giulio Albanese, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kijamii ya Vikarieti ya Roma na Misa ya kimataifa iliyoongozwa na Kardinali Reina, Makamu wa Papa wa kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane  Laterano. Kiini cha sherehe hiyo kiliashiriwa pia na masalia ya Mtakatifu Francis wa Sales, ambayo yaliletwa jijini Roma kutoka mji wa Treviso, Kaskazini mwa Italia, ambako yamehifadhiwa tangu mwaka 1913. Hata hivyo Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 59 ya Hupashanaji habari Ulimwenguni kwa mwaka 2025 uliochapishwa katika siku hii ya tarehe 24 Januari, ulinukuliwa sana wakati wa hafla zote na kusisitiza wito wa kushiriki matumaini kwa upole na fadhila kuu katika utume wa Jubilei kwa ujumla.

Kardinali Reina wakati wa ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano
Kardinali Reina wakati wa ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano

Kristo aliondoa silaha za kiburi

Katika mahubiri yake, Kardinali Reina alisema kuwa Jubilei ni wakati wa rehema, ambapo mwelekeo hubadilika kutoka katika dhambi zilizotendwa hadi kufikia nguvu ya mabadiliko ya msamaha wa Mungu. Alielekeza fikira kwenye mwaliko wa Papa Francisko wa kuwa “wawasilianishaji wa matumaini na kuondoa silaha za mawasiliano na kufuata kielelezo cha Kristo. Kardinali Reina aliendelea na tafakari ya masimulizi ya Injili ya mwanamke aliyenaswa katika uzinzi kuwa kielelezo cha njia hiyo. Yesu, alikabiliana na hali ya kashfa, na alichagua njia ya mawasiliano ya upole, huku akiepuka uchokozi na kushirikiana na ukweli. Kwa kuuliza, “Ni nani miongoni mwenu asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupa jiwe,†Kardinali Reina alieleza kwamba Kristo aliondoa silaha ya kiburi na kukaribisha kutafakari. Kwa njia hiyo ili kuondoa silaha za mawasiliano, ni lazima kwanza tuondoe kiburi chetu. Maandiko yanatukumbusha kwamba Mungu pekee ndiye mwamuzi. Kardinali Reina alisisitiza kuwa “Alisema kwamba Yesu hakumfafanua mwanamke huyo kwa kosa lake bali alitambua hadhi yake ya asili, na hivyo kutoa tumaini la kufanywa upya.

Baadhi ya washiriki wa misa ya ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa mawasiliano
Baadhi ya washiriki wa misa ya ufunguzi wa Jubilei ya Ulimwengu wa mawasiliano

Kardinali katika mahubiri yake kwa kutafakari maneno ya Yesu kwa mwanamke huyo alisema: “Nenda zako na usitende dhambi tena.†Maneno haya, yanajumuisha matumaini na yanaelekeza kwenye mustakabali wa mabadiliko. Tendo hili la huruma, lilikuwa Jubilei ya kibinafsi ya mwanamke huyo. Ikiwa tunataka kusherehekea Jubilei yetu kama ulimwengu wa mawasiliano, lazima tufuate dhana hii, tukikumbatia mtindo wa mawasiliano unaotambua utu wa kila mwanadamu na kukuza utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja,†Kardinali alihitimisha kwa ushauri huo kwetu kama wanahabari.

Washiriki wa Jubilei ya Ulimwengu wa mawasiliano
Washiriki wa Jubilei ya Ulimwengu wa mawasiliano   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Liturujia ya toba iliyotanguliwa na Misa ilianza kwa usomaji kutoka kwa Tamko la Papa la Maelekezo ya Jubilei ya 2025 “Spes nonconfundit.†Katika liturujia hiyo ilitolewa mwaliko kwa washiriki wote kutafakari juu ya matumaini yaliyo katika kila moyo na kukumbatia njia ya uwongofu unaoashiriwa kupitia Mlango Mtakatifu unaomwakilisha Kristo mwenyewe.

Tafakari  ya Padre Albanesi

Katika kuwaandaa washiriki wa ibada hiyo, Padre Albanese alianza na tafakari. Tumekusanyika hapa pamoja kwa ajili ya liturujia hii ya toba na hamu yetu ni kupata wongofu wa kweli. Kupitia nabii Ezekieli Bwana anamwambia kila mmoja wetu: “Nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyoni mwako wa jiwe, nami nitakupa moyo wa nyama.†Kwa hiyo, sote tunaalikwa katika Jubilei hii ya Matumaini kupita katika Mlango Mtakatifu, tukiwa na uhakika kwamba mlango huo ni Yesu Kristo. Kifungu kinachoashiria mabadiliko, uongofu kwa kweli, na kuacha nyuma mtu wa kale kuwa viumbe vipya. Tunajua vyema kwamba ulimwengu wa mawasiliano kwa ujumla ni uwanja wa kimisionari na kwa hivyo uongofu tunaozungumzia hauwezi kupuuza muktadha wa kitaalamu ambamo tumeitwa kuishi maisha yetu ya kusisimua kama waamini.

Padre Albanese akitoa tafakari katika liturujia ya Toba
Padre Albanese akitoa tafakari katika liturujia ya Toba

Hatari, inayonyemelea kila wakati, ni ile ya kusaliti maagizo ya Injili kwa kuwa, kwa maana - inafaa kusema, kuna  wa mwengine", yule aliye na herufi ndogo "p", lakini sio ya Mungu. Yesu, katika kujibu swali la mwandishi katika kifungu cha Injili ambacho kilisikia punde (ambacho ndiyo amri ya kwanza kati ya amri zote?), alipaswa kujibu, kulingana na taalimungu ya Kiyahudi, kwamba amri ya kwanza kati ya zote ni amri ambayo Mungu pia hushika. Na ni amri gani ambayo Mungu hushika? Pumziko la Sabato. Hii ndiyo sababu kushika pumziko la Sabato ni sawa na kushika Sheria nzima. Na hapa jibu la Yesu linashangaza, kwani hataji amri yoyote. Yesu anarejea imani ya Israeli, Shema Israeli, Sikiliza Israeli, sala ambayo Mwisraeli mcha Mungu huisoma mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, na inayopatikana katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati katika sura ya sita, lakini bila kutaja Dekalojia. “Ya kwanza ndiyo,†asema Yesu: “Sikiliza, Israeli! “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote."

Kwaya iliyoongoza ibada ya Misa
Kwaya iliyoongoza ibada ya Misa

 

Yesu anaongeza umiliki wa maandishi ya Kiebrania ili kuonyesha upesi, nguvu ya amri hii, "kwa roho yako yote". Ni maisha, akili katika Kigiriki, "kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote." Lakini ili kuwa wa kweli, upendo kwa Mungu lazima utafsiriwe katika upendo kwa jirani yako na hivyo Yesu anaongeza kwenye sala hii agizo lililotolewa katika kitabu cha Mambo ya Walawi, sura ya 19, na kusema “Ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Bwana anamalizia kwa kusema: “Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.†Na ‘Dekalojia’ yaani amri 10 za Mungu? Kwa Yesu, kila kitu kinapata muhtasari wake katika amri kwa Mungu ambayo haiwezi kupuuza upendo kwa jirani. Pande mbili za sarafu moja.

Wakati wa maungamo
Wakati wa maungamo   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Muhtasari unaopata maelezo yake katika Injili ya Yohane wakati, akihutubia mitume, alisema: "Mpendane kama nilivyowapenda ninyi. Kwa hiyo, tujiulize kama wakati fulani njia yetu ya kuwasiliana-haijalishi kama kwa wasomaji, kwa umma, kwa jumuiya ya kiraia kwa ujumla - inaonesha Upendo wa Mungu, yale ambayo Mwalimu anazungumzia, au kama badala yake inajibu mantiki maalum, ya kidunia, ya kukera, hasa dhidi ya Mungu na dhidi ya mwanadamu. Tunaombwa na Baba Mtakatifu katika Jubilei hii kuwa wabeba Matumaini, naam, Tumaini hilo ambalo mara nyingi hatujui jinsi ya kuwasiliana! Mtakatifu Augustino anasema kuwa Tumaini lina watoto wawili. Wa kwanza anaitwa "hasira", wa pili anaitwa "ujasiri." Kukasirika kwa mambo ambayo sio sawa na ujasiri, yaani ujasiri wa kuthubutu kuyabadilisha. Kwa hiyo, tumaini ni fadhila ambayo lazima itekelezwe kama ishara ya wazi ya uongofu wetu. Kwa maneno ya Papa Francisko: “kupata cheche za wema zinazotuwezesha kutumaini.â€

24 Januari 2025, 22:30