ĐÓMAPµĽş˝

2025.01.21 Dk.Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. 2025.01.21 Dk.Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. 

Dk.Ruffini:kuwasiliana si kwa njia moja bali thamani yake kubwa iko katika uhusiano!

Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Vatican azungumzia Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano,itakayofanyika kuanzia Januari 24-26:"Mwaka Mtakatifu ni fursa ya kujiuliza na kuanza kugundua tena maana ya wito wetu wa kina kama wana mawasiliano."

Vatican News.

Katika kuwasilisha Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano iliyopangwa kuanzia tarehe 24 hadi 26 Januari 2025, Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Mawasiliano, asubuhi ya tarehe 21 Januari,  wakati wa  Kipindi cha "matangazo ya Radio Vaticana  kiitwacho "con Voi,” alisema kuwa: “Hatutaki kufanya chochote zaidi ya kushiriki tafsiri ya ulimwengu. Ni ukweli ambao umefunuliwa kwetu na tunataka kuutafuta katika historia yetu kwa nguvu zetu zote.”

Tukio  hilo ni pamoja na mfululizo wa mipango  itakayofuata  ambayo ni ya kwanza kati ya mengi yaliyopangwa Mwaka huu  Mtakatifu. Jubilei ya ulimwengu wa vyombo vya habari inaenda sanjari na kumbukizi la Mtakatifu Mlinzi wa waandishi wa habari, Mtakatifu Francis de Sales, ambayo itaadhimishwa tarehe24 Januari.

Mahusiano ni ufunguo wa uandishi bora wa habari

Alipoulizwa kuhusu ukweli kwamba waandishi wa habari wanaitwa kuwa wabeba matumaini na ukweli, Dk. Ruffini alikumbusha kwamba "bila uhusiano hakuna tumaini, sisi wenyewe tumefungwa. Uhusiano ni kuaminiana na mwingine na katika kuamini tunaweza kuingia katika uhusiano na wengine hata kama wanaweza wasifikiri kama sisi. Uhusiano unaweza pia kuhusisha mambo magumu sana kama msamaha, yaani, kuanza upya. Kama Papa Francisko alivyosema, wakati mwingine,  alikumbusha Dk. Ruffini  kuwa uhusiano huvunjika, lakini basi tunaweza kuanza tena, hata kwa njia tofauti, lakini kila wakati.” Kwa njia hiyo “Uhusiano huo, baada ya yote, huzaliwa kutokana na kuaminiana na matumaini ni kuaminiana na kutegemeana na kisha kuujenga.” Na ndiyo maana, “hata ile dhana ya mawasiliano si ya njia moja, bali ni msingi wa upendo, kuhusu uaminifu na kuhusu mahusiano."

Mipango mingine

Tukio hilo la siku tatu lililotolewa kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano linajumuisha matukio mengi, ambayo Mkuu wa Mawasiliano ya Vatican alikumbuka wakati wa mahojiano

“Ndio, matukio yapo mengi na naweza kusema kwamba yalizaliwa yenyewe, kutokana na shauku  ya kufanya uchunguzi wa nafsi, tujiulize na labda tuanze kutafuta tena maana ya awali kabisa, ya chanzo cha wito wetu, hasa hiyo ya waandishi wa habari.  Kwa hivyo kuwasiliana, kuchagua mawasiliano kama taaluma ni kwa njia zote za wito. Miongoni mwa matukio mengi, la muhimu zaidi ni mkutano na  Papa Francisko na hija ya kuvuka Mlango Mtakatifu pamoja na kutafakari mahali tulipo na tunapotaka kwenda, kwa hiyo ni kutafuta mizizi ya matumaini yetu inapatikana wapi.”

Vyombo vya habari vya Vatican

Vyombo vya habari vya Vatican  vinaitwaje kuripoti juu ya Jubilei?

Kwa mujibu wa Dk. Ruffini  alibainisha kuwa: "ni kujaribu kwenda ndani ya kina cha Jubilei ambayo Papa alisema, ni ile ya kujiona kuwa si bora kuliko mimi, au  tukio, ambalo sio fataki,na wala sio kitu cha papo kwa hapo, lakini ni safari ambayo inaendelea na ambayo inahusu kila mtu, ambayo inatuhusu sisi  sote tunaoamini, lakini vile vile  kwa yeyote anayetaka kupata ishara ya mabadiliko ndani yake.” Miongoni mwa kile kinachohitajika kuwasiliana, hakika kuna ukweli kwamba Mwaka Mtakatifu sio wa ajabu, wa kile kitendo cha  kupitia Mlango Mtakatifu na kitu cha kiini macho la. Badala yake, ni kuamini kwamba ni ishara, kurejesha sababu kuu za imani yetu, zile zinazotufanya tuwe washiriki wa mtu mwingine. Kwa hivyo tunaweza kuchukua njia tofauti za kubadilika na kuanza tena. Kuchunguza dhamiri zetu na uelewe, kama Papa Francisko alivyosema katika kipindi kibaya cha janga la uviko.”.

Jukumu kuu la historia

Wakati wa simu ya moja kwa moja, wasikilizaji waliomba kuakisi umuhimu wa historia za maisha halisi. Dk. Ruffini alisisitiza kwa hiyo kuwa "historia ni sisi, yaani  sisi ni historia  tunazosimulia na historia tunazoishi. Akili ya mwanadamu ni mchanganyiko wa akili ya moyo na akili ya kifikra. Bila moyo hatuwezi kuelewa kila kitu kiukweli.”

Kisha mkuu wa  Mawasiliano Vatican alijikita  kuendelea  juu ya muda wa mawasiliano kwamba: “ Jambo muhimu ni kasi ya wakati wetu. Ili kuelewa mambo, pia tunahitaji kwenda polepole kidogo, pia tunahitaji kusimama ili kugundua upya roho zetu, kushika nafsi ya wengine ikiwa tunataka kuwa waandishi wazuri wa  habari. Papa anaposema kuchakaa kwa soli za viatu vyako, anazungumzia pia juu ya wakati wa kwenda polepole ambao wakati mwingine tunahitaji kuelewa na kusimulia historia , ili kuzielewa.

Kumbukumbu

Mkuu wa vyombo vya habari vya Vatican akiendelea alisema kuwa “kukuza kumbukumbu  ni kuwa na uwezo wa kuunganisha mambo ili kutoa mtazamo ambao ni mtazamo mzuri. Ni kazi ya waandishi wa habari, vinginevyo, tuseme, tungeishi mbali, kusahau na bila maana. Hii ni kidogo ni  kazi ya waandishi wa habari na pengine ni sisi tunaopoteza  katika kasi ya muda kwamba inaonekana zinazotumwa kwa papo hapo. Ulikuwa unasema ukweli kwanza, tafsiri ya ukweli kwa njia ya uwazi. Kwa kuhitimisha Dk. Ruffini alisema: “Sisi hatutaki kufanya chochote isipokuwa kushiriki tafsiri ya ulimwengu. Ni ukweli ambao umefunuliwa kwetu na tunatafuta katika historia yetu kwa nguvu zetu zote, katika uhusiano, na kupata kwa pamoja njia mpya na barabara mpya.”

Dk Ruffini na Jubilei ya Wanamawasiliano.
21 Januari 2025, 16:34