AI:Chombo ambacho hakiwezi kuchukua nafasi ya utajiri wa ubinadamu!
Andrea Tornielli
Jambo la kwanza ambalo linapotosha ni jina. Kinachojulikana kama "Akili Mnemba" ni mojawapo ya matukio ambayo jina limehesabu na kuzingatiwa sana katika mtazamo wa kawaida wa jambo hilo. Hati ya "Antiqua et nova" ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na lile la Utamaduni na Elimu inatukumbusha kwanza kabisa kwamba AI ni chombo: kinafanya kazi, lakini hakifikirii. Haiwezi kufikiri. Kwa hiyo inapotosha kuhusisha sifa za kibinadamu, kwa sababu ni "mashine" ambayo inabakia kwenye eneo la mantiki ya kihisabati. Chombo hiki hakina ufahamu wa kisemantiki wa ukweli, wala uwezo wa angavu na ubunifu. Hakiwezi kuiga utambuzi wa kimaadili au uwazi usio na shauku kwa kile ambacho ni cha kweli na kizuri, zaidi ya matumizi yoyote mahususi. Kwa kifupi, Akili Mnamba haina kila kitu ambacho ni kweli na cha kina cha binadamu.
Akili ya mwanadamu kiukweli ni ya mtu binafsi na ya kijamii kwa wakati mmoja, ya busara na ya kuathiri kwa wakati mmoja. Inaishi kupitia mahusiano endelevu yanayopatanishwa na umbile lisiloweza kutengezwa tena la mtu. Kwa hivyo AI inapaswa kutumika tu kama zana inayosaidia akili ya mwanadamu, na sio kujifanya kuchukua nafasi ya utajiri wake wa kipekee. Licha ya maendeleo ya utafiti na matumizi yake iwezekanavyo, AI inaendelea kubaki "mashine" ambayo haina jukumu la maadili, jukumu hilo ambalo badala yake linabaki kwa wale wanaoiunda na kuitumia. Kwa sababu hiyo, hati mpya inasisitiza kuwa ni muhimu kwamba wale wanaofanya maamuzi kulingana na AI wawajibike kwa uchaguzi uliofanywa, na kwamba inawezekana kuwajibika kwa matumizi ya chombo hiki katika kila hatua ya mchakato wa kufanya maamuzi.
Ncha na njia zinazotumiwa katika masuala ya AI lazima zitathminiwe ili kuhakikisha kwamba zinaheshimu na kukuza utu wa binadamu na manufaa ya wote: tathmini hii inajumuisha kigezo cha kimsingi cha kimaadili cha kutambua uhalali au vinginevyo wa matumizi ya akili mnemba. Kigezo kingine cha tathmini ya maadili ya AI, Hati inapendekeza, kuhusu uwezo wake wa kutekeleza mahusiano chanya ambayo mwanadamu anayo na mazingira yake na ya asili, kukuza muunganisho mzuri wa watu binafsi na jamii na kuinua uwajibikaji wa pamoja, kuelekea manufaa ya wote. Ili kufikia malengo haya, ni muhimu kwenda zaidi ya mkusanyiko wa data na ujuzi tu, kufanya kazi ili kufikia "hekima ya kweli ya moyo," kama Papa Francisko anapendekeza, ili matumizi ya akili ya mnemba isaidie wanadamu kuwa bora zaidi.
Kwa maana hii, Hati inaonya dhidi ya utii wowote wa kiteknolojia, na kualika matumizi yake kutochukua nafasi ya kazi ya binadamu hatua kwa hatua - ukweli ambao unaweza kuunda aina mpya za kutengwa na usawa wa kijamii - lakini kama zana ya kuboresha usaidizi na kuboresha huduma ubora wa mahusiano ya kibinadamu. Na pia kama msaada katika kuelewa ukweli changamano na kama mwongozo katika kutafuta ukweli. Kwa sababu hiyo, kupambana na bidhaa bandia zinazoendeshwa na AI sio kazi tu kwa wataalam wa tasnia, lakini inahitaji juhudi za kila mtu. Ni lazima pia tuzuie akili mnemba kutumiwa kama aina ya unyonyaji au kuweka mipaka ya uhuru wa watu, kuwanufaisha waliowachache kwa gharama ya wengi, au kama aina ya udhibiti wa kijamii, kupunguza watu katika seti ya data. Na haikubaliki kwamba katika muktadha wa vita tunakabidhi uchaguzi wa kuchukua maisha ya wanadamu kwa mashine: kwa bahati mbaya tumeona ni kiasi gani na ni aina gani ya silaha za uharibifu zinazoongozwa na akili mnemba zinahusika, kama inavyooneshwa kwa huzuni katika migogoro mingi inayoendelea.