Papa Francisko anatarajia kwenda Luxembourg na Ubelgiji Septemba 26-29
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Ziara yake ya 45 ya Kitume , iliyomuona akitembelea Nchi za Asia na Osceania, sasa kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kwenda Ziara yake ya Kitume ya 46 akitembelea Nchi ya Ubelgiji na Luxembourg. Kwa mujibu wa taarifa kuhusu ziara hiyo iliyokuwa imechapishwa mnamo tarehe 19 Julai 2024, ilibainishwa kuwa katika zafari hiyo: “Kuondoka kwa ndege ya Papa kunatarajiwa kuanzia Alhamisi 26 Septemba 2024 saa 2.05 asubuhi majira ya Ulaya kutoka Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fiumicino, Roma kuelekea Luxembourg, ambapo kuwasili kulipangwa saa 4.00 asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Findel- Luxembourg.
Hapo baada ya sherehe ya kukaribisha, atafanya ziara ya heshima kwa Mfalme wa Luxembourg kumeratibiwa saa 4.45 asubuhi katika Jumba la Kifalme. Hii itafuatiwa na mkutano na waziri mkuu na ule wa mamlaka, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia katika Ukumbi wa 'Mzunguko wa Miji' katika hali zote mbili, Papa Francisko atatoa hotuba. Mchana, majira ya saa 10.30 Jioni, atakutana na Jumuiya ya Kikatoliki katika Kanisa Kuu la Mama wa Luxembourg.
Bruxelles
Saa 11.45 jioni sherehe ya kuaga itafanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Findel - Luxembourg- kutoka hapo ambapo ndege itampeleka Papa hadi Bruxelles ikpaa saa 12.15 jioni na kuwasili kumepangwa saa 1:10 usiku, katika Uwanja wa Ndege wa Melsbroek, ambapo sherehe itafanyika ya kuwakaribisha. Ijumaa tarehe 27 Septemba 2024, itafunguliwa saa 3.15 asubuhu kwa ziara ya heshima kwa Mfalme wa Wabelgiji katika Ngome ya Laeken; ikifuatiwa na mkutano na waziri mkuu na ule wa mamlaka na mashirika ya kiraia, ambapo Papa Francisko atatoa hotuba. Mchana, saa 10.30 jioni, katika Chuo Kikuu Katoliki cha Leuven, Papa anatarajiwa kufanya mkutano na maprofesa wa vyuo vikuu ambapo Baba Mtakatifu atahutubia hotuba.
Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024, saa 4.00 asubuhi, Papa anatarajiwa kukutana na maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na wahudumu wa kichungaji katika Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu huko Koekelberg; Papa Francisko atawahutubia pia mchana wanafunzi wa chuo kikuu atakaokutana nao saa 10.30 katika ukumbi mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Louvain. Saa 12.15 jioni atafanya mkutano wa faragha na washiriki wa Jumuiya ya Yesu (Jesuit) kama desturi yake katika Chuo cha Mtakatifu Mikaeli.
Dominika tarehe 29 Septemba 2024, itakuwa siku ya mwisho ya Ziara yake ya kitume, ambapo Papa Francisko ataongoza Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa ‘King Baudouin’ saa 4:00 Sala ya Malaika wa Bwana. Sherehe ya kuaga imepangwa kufanyika saa 6.15 jioni katika kituo cha anga cha Melsbroek kutoka ambapo ndege ya Papa itapaa kuelekea Roma saa 6.45 jioni. Kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Rome-Fiumicino kumepangwa saa 8.55 mchana.
Tutazamame na kujua kwa undani nchi hizi mbili atakazotembelea
Jedwali la 1 ni Idadi ya watu na muundo wa kikanisa nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 ambapo: |
|
||||||
|
Ubelgiji |
|
Luxembourg |
|
|
||
|
|
|
|
||||
Ukubwa kwa (km²) |
30.528 |
|
2.586 |
|
|
||
Idadi ya watu (kwa maelfu)
|
11.618 |
|
654 |
|
|
||
Msongamano (Wakazi/Km2) |
381 |
|
253 |
|
|
||
Wakatiliki (kwa maelfu) |
8.361 |
|
271 |
|
|
||
Wakatoliki kwa kila wakaaji 100 |
719 |
|
41,43 |
|
|
||
Majimbo ya Kikanisa |
9 |
|
1 |
|
|
||
Maparokia |
3.656 |
|
275 |
|
|
||
Vutuo vingine vya kichungaji |
434 |
|
- |
|
|
||
Vituo vya Kichungaji katoliki |
2.044 |
|
985 |
|
|
|
||||
Jedwali la 2 - Watu wanaohusika katika shughuli za utume nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa: |
||||
|
Ubelgiji |
Luxemburg |
|
|
|
||||
Maaskofu |
22 |
3 |
|
|
Mapadre wa Majimbo |
2.066 |
121 |
|
|
Mapadre Watawa |
1.677 |
49 |
|
|
Mapadre kwa ujumla wake
|
3.743 |
170 |
|
|
Mashemasi wa kudumu |
577 |
20 |
|
|
Watawa wa kiume wasio Mapadre |
355 |
1.3 |
|
|
Watawa wa Nadhiri |
5.045 |
225 |
|
|
Wajumbe wa Taasisi za Kisekulari |
91 |
6 |
|
|
Wamisionari Walei |
34 |
- |
|
|
Makatekista |
4.803 |
- |
|
|
|
||||
Jedwali la 3 - Viashirio vya Jukumu la kichungaji nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa: |
||||
|
Ubelgiji |
Luxembourg |
|
|
|
||||
Wakatoliki kwa Mapadre |
2.234 |
1,594 |
|
|
Wakatoliki kwa wahudumu wa kichungaji |
570 |
620 |
|
|
Mapadre kwa kituo cha uchungaji |
0,92 |
0,62 |
|
|
Mapadre kwa watu 100 wanaojishughulisha na shughuli za kitume
|
25,7 |
39,6 |
|
|
Jedwali la 4 - Miito ya kikuhani nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa: |
||||
|
Ubelgiji |
Luxembourg |
|
|
|
||||
Waseminari ndogo |
1 |
- |
|
|
Waseminari Kuu |
197 |
12 |
|
|
Waseminari wakuu kwa kila wakaaji 100,000 |
1,70 |
1,83 |
|
|
Waseminari wakuu kwa kila Wakatoliki 100,000 |
2,36 |
4,43 |
|
|
Waseminari wakuu kwa kila mapadre 100 |
5,26 |
7,06 |
|
|
Jedwali la 5 - Vituo vya elimu vinavyomilikiwa na/au vinavyoelekezwa na mapadre au Watawa nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa: |
||||
|
||||
|
Ubelgiji |
Luxembourg |
|
|
|
||||
Shule |
|
|
|
|
- Awali na Msingi |
3.368 |
2 |
|
|
- Sekondari ya Kati na Sekondari |
1.076 |
5 |
|
|
- Masomo ya juu na Chuo Kikuu |
30 |
- |
|
|
Wanafunzi wa: |
|
|
|
|
- Shule za awali na Msingi |
608.989 |
1.980 |
|
|
- Wa Shule za Kati na Sekondari |
572.292 |
2.500 |
|
|
- Taasisi za Juu na Chuo Kikuu |
172.563 |
- |
|