杏MAP导航

Tafuta

Nembo ya ziara ya 46 ya Kitume ya Papa nchini Ubelgiji na Luxembourg kuanzia 26-29 Septemba 2024. Nembo ya ziara ya 46 ya Kitume ya Papa nchini Ubelgiji na Luxembourg kuanzia 26-29 Septemba 2024.  

Papa Francisko anatarajia kwenda Luxembourg na Ubelgiji Septemba 26-29

Ni ziara ya kitume ya 46 katika nchi za Luxembourg na Ubelgiji kuanzia tarehe 26-29 Septemba 2024 ambapo safari hii inaongozwa na kauli mbiu:"Kwa kuhudumia" ya huko Luxembourg wakati "Njia ya kuwa na matumaini,"ndiyo ya nchini Ubalgiji katika mji wa Bruxelles.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Ziara yake ya 45 ya Kitume , iliyomuona akitembelea Nchi za Asia na Osceania, sasa kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024,  Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kwenda Ziara yake ya Kitume ya 46 akitembelea Nchi ya Ubelgiji na Luxembourg. Kwa mujibu wa taarifa kuhusu ziara hiyo iliyokuwa imechapishwa mnamo tarehe 19 Julai 2024, ilibainishwa kuwa  katika zafari hiyo: “Kuondoka kwa ndege ya Papa kunatarajiwa kuanzia Alhamisi 26 Septemba 2024 saa 2.05 asubuhi majira ya Ulaya kutoka Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fiumicino, Roma kuelekea Luxembourg, ambapo kuwasili kulipangwa saa 4.00 asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Findel- Luxembourg.

Kardinali Jean-Claude Hollerich,Askofu Mkuu wa Luxembourg
Kardinali Jean-Claude Hollerich,Askofu Mkuu wa Luxembourg   (Archeveche de Luxembourg / SCP)

Hapo baada ya sherehe ya kukaribisha, atafanya ziara ya heshima kwa Mfalme wa Luxembourg kumeratibiwa saa 4.45 asubuhi katika Jumba la Kifalme. Hii itafuatiwa na mkutano na waziri mkuu na ule wa mamlaka, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia katika Ukumbi wa 'Mzunguko wa Miji' katika hali zote mbili,  Papa Francisko atatoa hotuba. Mchana, majira ya saa 10.30 Jioni, atakutana na Jumuiya ya Kikatoliki katika Kanisa Kuu la Mama wa Luxembourg.

Luxembourg
Luxembourg   (pixabay)

Bruxelles

Saa 11.45 jioni sherehe ya kuaga itafanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Findel - Luxembourg- kutoka hapo ambapo ndege itampeleka Papa hadi Bruxelles ikpaa saa 12.15 jioni na kuwasili kumepangwa saa 1:10 usiku, katika Uwanja wa Ndege wa Melsbroek, ambapo sherehe itafanyika ya kuwakaribisha. Ijumaa tarehe 27 Septemba 2024,  itafunguliwa saa 3.15 asubuhu  kwa ziara ya heshima kwa Mfalme wa Wabelgiji katika Ngome ya Laeken; ikifuatiwa na mkutano na waziri mkuu na ule wa mamlaka na mashirika ya kiraia, ambapo Papa  Francisko atatoa hotuba. Mchana, saa 10.30 jioni, katika Chuo Kikuu Katoliki cha  Leuven, Papa anatarajiwa kufanya mkutano na maprofesa wa vyuo vikuu ambapo Baba Mtakatifu atahutubia hotuba.

Ziara ya Papa huko Luxembourgo na Ubelgiji
Ziara ya Papa huko Luxembourgo na Ubelgiji
Bruxelles
Bruxelles   (AFP or licensors)

Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024, saa 4.00 asubuhi, Papa anatarajiwa kukutana na maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na wahudumu wa kichungaji katika Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu huko  Koekelberg; Papa Francisko atawahutubia  pia mchana wanafunzi wa chuo kikuu atakaokutana nao saa 10.30 katika ukumbi mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki  cha  Louvain. Saa 12.15 jioni atafanya mkutano wa faragha na washiriki wa Jumuiya ya Yesu (Jesuit) kama desturi yake katika Chuo cha Mtakatifu Mikaeli.

Dominika tarehe 29 Septemba 2024, itakuwa siku ya mwisho ya Ziara yake ya  kitume, ambapo Papa Francisko ataongoza Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa ‘King Baudouin’ saa 4:00 Sala ya Malaika wa Bwana. Sherehe ya kuaga imepangwa kufanyika saa 6.15 jioni katika kituo cha anga cha Melsbroek kutoka ambapo ndege ya Papa itapaa kuelekea Roma saa 6.45 jioni. Kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Rome-Fiumicino kumepangwa saa 8.55 mchana.

Tutazamame na kujua kwa undani nchi hizi mbili atakazotembelea

Jedwali la 1 ni  Idadi ya watu na muundo wa kikanisa nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 ambapo:

 

 

   Ubelgiji

 

   Luxembourg

 

 

 

 

 

 

Ukubwa kwa (km²)

    30.528

 

    2.586

 

 

 

Idadi ya watu

(kwa maelfu)

 

    11.618

 

     654

 

 

Msongamano (Wakazi/Km2)

    381

 

     253

 

 

Wakatiliki (kwa maelfu)

   8.361

 

   271

 

 

Wakatoliki kwa kila wakaaji 100

    719

 

41,43

 

 

Majimbo ya Kikanisa

     9

 

    1

 

 

Maparokia

    3.656

 

    275

 

 

Vutuo vingine vya kichungaji

     434

 

     -

 

 

Vituo vya Kichungaji katoliki

    2.044

 

     985

 

 

 

Jedwali la 2 - Watu wanaohusika katika shughuli za utume nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa:

 

Ubelgiji

Luxemburg

 

 

 

Maaskofu

      22

    3

 

 

Mapadre wa Majimbo

      2.066

   121

 

 

Mapadre Watawa

     1.677

   49

 

 

Mapadre kwa ujumla wake

 

     3.743

    170

 

 

Mashemasi wa kudumu

    577

     20

 

 

Watawa wa kiume wasio Mapadre

    355

    1.3

 

 

Watawa wa Nadhiri

    5.045

    225

 

 

Wajumbe wa Taasisi za Kisekulari

    91

    6

 

 

Wamisionari Walei

    34

    -

 

 

Makatekista

    4.803

     -

 

 

 

 

Jedwali la 3 - Viashirio vya Jukumu la kichungaji nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa:

 

Ubelgiji

Luxembourg

 

 

 

Wakatoliki kwa Mapadre  

   2.234

   1,594

 

 

Wakatoliki kwa wahudumu wa kichungaji

   570

   620

 

 

Mapadre kwa kituo cha uchungaji

    0,92

     0,62

 

 

 

 

Mapadre kwa watu 100 wanaojishughulisha na shughuli za kitume

 

 

   25,7

   39,6

 

 

Jedwali la 4 - Miito ya kikuhani nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa:

 

   Ubelgiji

  Luxembourg

 

 

 

Waseminari ndogo

       1

      -

 

 

Waseminari Kuu

      197

     12

 

 

Waseminari wakuu kwa kila wakaaji 100,000

       1,70

     1,83

 

 

Waseminari wakuu kwa kila Wakatoliki 100,000

      2,36

     4,43

 

 

Waseminari wakuu kwa kila mapadre 100

     5,26

     7,06

 

 

 

Jedwali la 5 - Vituo vya elimu vinavyomilikiwa na/au vinavyoelekezwa na mapadre au Watawa nchini Ubelgiji na Luxembourg kufikia tarehe 31 Desemba 2022 inaonesha kuwa:

 

 

   Ubelgiji

  Luxembourg

 

 

 

Shule

 

 

 

 

-       Awali na Msingi

   3.368

   2

 

 

-       Sekondari ya Kati na Sekondari

    1.076

   5

 

 

-       Masomo ya juu na Chuo Kikuu

   30

    -

 

 

Wanafunzi wa:

 

 

 

 

-       Shule za awali na Msingi

    608.989

    1.980

 

 

-       Wa Shule za Kati na Sekondari

   572.292

     2.500

 

 

-       Taasisi za Juu na Chuo Kikuu

    172.563

       -

 

 
23 Septemba 2024, 14:17