ÐÓMAPµ¼º½

2023.10.20 Sinodo  ya Maaskofu Inaendelea mjini Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. 2023.10.20 Sinodo ya Maaskofu Inaendelea mjini Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.  (Vatican Media)

Sinodi,kuna mabadiliko ya ratiba&kazini kuhusu Barua kwa Watu wa Mungu

Katika Mkutano Mkuu Oktoba 23 O hati itakayoelekezwa kwa Waamini wote itawasilishwa na kujadiliwa na Vikundi vidogo na kwa pamoja.Katika uwasilishaji wa muhtasari wa ripoti tarehe 25 Oktoba utatolewa na Msemajai mkuu na Wajumbe wa Sinodi watasali Oktoba 27 katika Kanisa la Mtakatifu Petro kuombea Aman kwa ombi la Papa.

Vatican News.

Tarehe 19 Oktoba 2023 alasiri  wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kumi na tatu wa Baraza Kuu la XVI la kawaida la Sinodi ya Maaskofu, Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi hiyo, alitoa maelezo kuhusiana na ratiba ya siku chache zijazo. Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Sekretarieti Kuu ya Sinodi inabainisha kuwa  “Tume ya Ripoti ya Sinodi  imeonesha vigezo vipya vya uandishi wa maandishi. Kwanza kabisa, mpango hautawasilishwa katika sehemu mbili (A na B), kama inavyokuwa imeoneeshwa kwenye ratiba ya awali; zaidi ya hayo, Sekretarieti Kuu na Ofisi ya Rais inakusudia kutoa muda wa Mkutano Mkuu  wa kuamua kuhusu mbinu na hatua za awamu itakayofuata ya mchakato wa sinodi kwa kuzingatia kikao cha pili. Na hatimaye, Mkutano Mkuu wa Sinodi  tayari umepitisha pendekezo la kuchapishwa kwa Barua  ya Watu wa Mungu mwishoni mwa kikao hicho cha kwanza.

Mabadiliko ya ratiba

Kwa  sababu hizo tatu   imehitajika kufanya mabadiliko fulani kwenye Ratiba nzima. Kwa hiyo siku ya Jumatatu tarehe 23 Oktoba 2023, kama ilivyopangwa, washiriki watakutana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Adhimisho la Ekaristi Takatifu kwenye Altare ya Kuu. Baadaye, kuelekea katika Mkutano Mkuu  na  Waraka wa Watu wa Mungu utawasilishwa na kujadiliwa ambapo kwanza katika katika Makundi Madogo na kisha katika wakati wa pamoja. Baadaye Kura husika itafuata. Kazi ya Sinodi itakatizwa  kwa hiyo Jumatatu alasiri na siku nzima tarehe 24 Oktoba. Washiriki watakutana Jumatano tarehe 25 Oktoba 2023 kwa  ajili ya uwasilishaji wa muhtasari wa ripoti na msemaji mkuu wa Sinodi. Nakala itakuwa ya kwanza kusomwa kibinafsi na kujadiliwa baadaye katika Mkusanyiko la Jumla na katika Vikundi vidogo vya mduara kwenye Ukumbi wa Paulo VI, katika mwendelezo wa mchakato wa safari na hivyo alasiri  Jumatano  25 Oktoba na asubuhi ya Alhamisi  26 Oktoba 2023.

Sala katika Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro

Pia siku ya Alhamisi alasiri, kuna mabadiliko  tofauti na  ilivyokuwa imeelezwa hapo awali, washiriki watakutana katika Mkutano Mkuu kwa mapendekezo ya mbinu na hatua za miezi kati ya kikao cha kwanza na cha pili cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu. Siku ya Ijumaa tarehe 27 Oktoba 2023, ikiwa ni sikukuu, washiriki wote wanaalikwa kushiriki katika maombi  kwa ajili ya Amani  duniani saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Mabadiliko ya ratiba ya Sinodi inayoendelea
20 Oktoba 2023, 10:05