MAP

Kituo cha Televisheni Vatican(CTV) kimetimiza miaka 40 tangu kuzaliwa kwake  tarehe 22 Oktoba 1983. Kituo cha Televisheni Vatican(CTV) kimetimiza miaka 40 tangu kuzaliwa kwake tarehe 22 Oktoba 1983. 

Miaka 40 ya CTV: kumtumikia Papa, kwa mtazamo wa siku zijazo

Maadhimisho ya Kituo cha Televisheni cha Vatican,kilianzishwa mnamo tarehe 22 Oktoba 1983 kwa utashi wa Mtakatifu Yohane Paulo II."Hatua inayofuata ni Jubilei ya 2025,kwa kuzingatia teknolojia mpya za uzalishaji na majukwaa mapya ya usambazaji,"anaelezea Stefano D'Agostini,mkurugenzi wa kitu hicho.

Vatican News

"Ili kujibu maswali mengi kuhusu hatua bora zaidi ya Kanisa kuhusu mawasiliano ya kijamii, hasa mawasiliano ya sauti na kuona, ili kutoa zana mpya za kutekeleza utume wa Kanisa ulimwenguni". Ndiyo madhumuni, kutoka katika maandiko yaliyoidhinishwa mnamo tarehe 22 Novemba 1983 na Mtakatifu Yohane Paulo II yalianzisha Kituo cha Televisheni cha Vatican, ambacho ni  huduma rasmi ya radio na televisheni ya Vatican. Katika miaka 40 ya kituo hiki (CTV), ambacho tangu 2017 katika mageuzi ya vyombo vya habari vya Vatican ilichukua jina la Vatican Media -kimetangaza moja kwa moja shughuli zote za Kipapa, ikiwa ni pamoja na ziara za kichungaji, nchini Italia na nje ya nchi, na kwa ujumla zaidi matukio na maonesho ambayo yana nafasi kuu katika  mji wa Vatican.

Mtazamo na umakini kwa vyombo vya habari

"Mtazamo wa mbele na umakini mkubwa kwa vyombo vya habari" ni sifa mbili za Mtakatifu Yohane Paulo II zilizosisitizwa na mkurugenzi wa sasa wa  Kituo hicho CTV -  cha Vyombo vya Habari vya Vatican Stefano D'Agostini. Kwa mujibu wake amesema:  "Kupitia waraka wa kipapa aliotia sahihi na sheria ya msingi iliyofuata ambayo asili, malengo na kazi zimebainishwa vyema zaidi, huanza shughuli ya televisheni ya Vatican".  Aidha Mkurugenzi D’Agostini alisema kuwa:“Hatua nyingine muhimu ni hati ya pili ya papa ya mnamo tarehe 25 Novemba 1996 ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II alitambua CTV kama moja ya taasisi zilizounganishwa kikamilifu na Vatican  ambayo ilihamisha  Kituo kutoka hatua ya majaribio hadi kufikia ukamilifu zaidi wa  maendeleo, na tarehe 1 Juni 1998, ilikuwa  tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria mpya ambapo majukumu yamebainishwa vyema zaidi, yakibainisha vitendo na ushirika kuendana na muktadha wa vyombo vya habari vya kimataifa."

Sehemu ya kumbukumbu

"Marehemu Emilio Rossi, rais wa zamani wa bodi ya wakurugenzi wa CTV, alisema kuwa katika Katekesi yake iliyotolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II "aliwasilisha Kituo kama mtoto akielekea kwenye ujana na ukomavu uliofuata. Ulikuwa ni ulinganisho wa kweli, kwani katika miaka iliyofuata, hasa wakati wa Jubilei kuu ya 2000, ukuaji wa CTV katika kiwango cha kimataifa na kutoka kwa mtazamo wa utayarishaji ulipata kasi kuelekea kutambuliwa kamili kama chombo cha marejeo cha utayarishaji wa televisheni cha Vatican na shughuli za Papa". Stefano D'Agostini alipenda kutoa shukrani za pekee kwa "watu wote ambao, kwa kuamini kwa dhati umuhimu wa taasisi yenye tija ya Vatican, wameongoza uthibitisho na maendeleo ya CTV kwa muda. Na akiwataja alisema: Kardinali John Patrick Foley, Fiorenzo Tagliabue, Sandro Baldoni, Emilio Rossi, Padre Antonio Stefanizzi, Ugo Moretto, Padre Federico Lombardi na Monsinyo Dario Edoardo Viganò ambao walielekeza Kituo kwenye maadhimisho yake ya miaka 30 ya shughuli, kuelekea malengo ya kisasa ya kiteknolojia (utayarishaji wa 3D na 4K) na televisheni ya hali ya juu na uzalishaji wa filamu, hebu fikiria filamu "A Man of His Word" iliyoongozwa na Wim Wenders.

Kuelekea Jubilei 2025

"Roho ya maendeleo ya miaka ya kwanza haijawahi kushindwa, hata leo hii  ndani ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano baada ya mageuzi yaliyotakiwa na Papa Francisko, pamoja na faida zote za mwelekeo wa pamoja wa vyombo vya habari vya Vatican na harambee zilizofuata. Kwa hiyo  CTV - Vyombo vya Habari vya Vatican vinaendelea kukua na kutafiti, pia kupitia lugha mpya za televisheni, ili kutekeleza dhamira yake ya kimataifa ya kusambaza picha za Papa na mamlaka yake kwenye kila chombo cha sauti na kuona na kuhakikisha chanzo cha kipekee cha kumbukumbu na muhimu kwa wanahistoria wa siku zijazo. Hatua inayofuata ni Jubilee ya 2025 kwa kuzingatia teknolojia mpya za uzalishaji na majukwaa mapya ya uenezaji," alihitimisha maelezo D'Agostini -

Viganò: nguvu ya kusisimua ya picha

Hata kulingana na Monsinyo Dario Edoardo Viganò, ambaye leo hii ni  rais wa msingi wa Kumbukumbu za Sauti na Vielelezo za Ukatoliki na makamu mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi Jamii, kuwa msingi wa kuzaliwa kwa CTV, miaka arobaini iliyopita, lazima itambuliwe kama "kipindi kisicho cha kawaida katika maono ya  Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alikuwa amefahamu jinsi historia na masimulizi yalivyohitaji taswira.” Kwa hiyo, alihisi mabadiliko katika mikakati ya mawasiliano, mienendo yake, lugha na muundo. CTV haisemi tu historia za Papa, lakini kwa miaka mingi imekuwa muundo ambao umewezesha kuunda vyanzo vya sauti na taswira muhimu katika historia." Mosninyo  Viganò alitoa mfano wa nguvu ya kuamsha picha: "Ikiwa tunazungumza juu ya Papa na Uviko - anaonesha - mara moja tunamfikiria Papa akiwa peke yake wakati anasali katika uwanja wa  Mtakatifu Petro kwenye Statio Orbis, Njia ya msalaba katika sala  kwa ajili ya janga  hilo usiki wa tarehe 27 Machi 2020".

Kwa upande wa Padre Federico Lombardi

Kwa upande wa Padre Federico Lomabardi Mjesuiti ambaye kwa miaka alikuwa Mkurugeniz na Mhariri Mkuu wa Radio Vatican, pamoja na Msemaji Mkuu wa Vyombo vya habali alisema kuwa kumbukumbu yenye nguvu zaidi ilikuwa ikisindikizwa na Kituo cha Televisheni cha Vatican, awamu nzima ya mwisho ya ugonjwa wa Mtakatifu Yohane Paulo II, baada ya kifo chake, mkutano wa baraza la Makardinali na kisha mwanzo wa Upapa wa Benedikto XVI. Kwa njia hiyo kituo cha  CTV kilitambuliwa kama huduma ya televisheni inayoweza kutekeleza kazi yake katika mwoekano mpya ya televisheni ya dunia." Kufuatia na picha  Mtakatifu Yohane Paulo  II, ambaye ulimwengu wote ulimpenda sana, na ishara dhahiri za ukuaji wa ugonjwa huo, ilikuwa ngumu sana. Ilikuwa na uzoefu mkubwa na wafanyakazi wote wa Kituo cha Televisheni, ambao waliona wajibu wote wa kuwasiliana na ulimwengu mtu ambaye kila mtu alimpenda katika udhaifu wake wa kimwili, kwa ukweli na heshima, kwa sababu alitaka kuendelea kuwa Papa na kushiriki kikamilifu katika maisha ya Kanisa. Kwa kichukua na kusambaza picha ilikuwa kuitikia mapenzi yake na njia yake ya kuliongoza na kulitumikia Kanisa na ubinadamu katika miaka hiyo, hata kwa ugonjwa wake. Kufanya vizuri - anaongeza Padre Lombardi - kuheshimu nia yake na wakati huo huo kuheshimu utu wa mtu anayeonekana kuwa mgonjwa lilikuwa jambo la changamoto sana. Katika miaka hiyo nilikuwa na heshima kubwa kwa waendeshaji na mafundi wote wa CTV kwa jinsi walivyofanya kazi hii. Na pia ninamshukuru sana Monsinyo Stanislaw Dziwisz, ambaye alitusaidia sana kwa ushauri, akisindikizana  nasi na kuelewa vizuri dhamira ya kazi yetu".

Picha za kihistoria

Kulingana na Padre Lombardi, upigaji picha muhimu zaidi chini ya uongozi wake wa CTV ni ule wa "ushiriki wa Papa anayeteseka katika (Via Crucis), Njia ya Msalaba ya mwisho kwenye Ukumbi wa Colosseum, magovu ya Kale ya Mateso ya Wakristo jijini Roma. Na anaikumbuka pamoja na hamu  nyingine kubwa ya kihistoria", chini ya uongozi wa Monsinyo Dario Viganò, wa  Papa Benedikto XVI ambaye aliacha upapa  wake mnamo mwaka 2013 kwa safari ya helikopta kutoka Vatican hadi Castel Gandolfo. Matashi mema kutoka kwa Padre Lombardi kwa miaka 40 ya CTV - Vatican Media ni kwamba “iendelee kutekeleza wajibu wake kama ilivyofanya katika miaka yote hii, ikikua hatua kwa hatua na daima kujidhihirisha kuwa sawa na huduma yake”.

Utajiri wa kumbukumbu

Inastahili kuzingatiwa na muhimu sana leo ni kumbukumbu ya rekodi za sauti na kuona katika umiliki wa CTV: huhifadhi kila kitu ambacho kimetolewa kutoka 1984 hadi leo katika mazingira ya angahewa na kuorodheshwa na mifumo ya kisasa ya kompyuta.

Miaka 40 ya CTV
23 Oktoba 2023, 16:10