WYD Lisbon 2023:Papa Francisko amefika Ureno
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Takriban dakika kumi na tano mapema kuliko muda uliopangwa, Baba Mtakatifu Francisko aliwasili saa 3.43 kwa saa za huko na saa (4.43 nchini Italia), ambapo alitua katika uwanja wa ndege wa Figo Maduro huko Lisbon, katika ziara yake ya kimataifa ya 42 na ikiwa ni kwa mara ya pili nchini Ureno Mara ya kwanza ilikuwa ni mnamo Mei 2017 wakati wa maadhimisho ya miaka 100 tangu kutokea kwa Mama Yetu wa Fatima 1917 na hivyo sasa Baba Mtakatifu atashiriki Siku ya 37 ya Vijana Duniani na vijana milioni wanaotarajiwa humo.
Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni ametoa taarifa kuhusu Mkutano wa Papa Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta kabla ya kuondoka kwenda Lisbon, tarehe 2 Agosti 2023. Katika taarifa hiyo Dk. Bruni mesema kuwa: “leo asubuhi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, kabla ya kuondoka kwenda Lisbon, Papa Francisko amewasalimia watu kama 15 na miongoni mwake, kulikuwa na baadhi ya vijana, wasichana na wavulana ambao wako wanaishi kipindi maalum katika Jumuiya ya kujijua na hivyo hawana uwezo wa kushiriki Siku ya vijana. Hawa waliambatana na babu na bibi watatu na wajuu wao. Mkutano huo ni sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Bibi na Babu na wazee iliyoadhimishwa hivi karibuni kwa kutaka kusisitiza uhusiano kati ya vizazi, ambapo wanaweza kusaidiana pamoja na kujifunza kutoka mmoja na mwingine”.
Telegram za Papa
Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ndege, kuelekea Ureno kama kawaida yake, ametuma telegram kwa viongozi wakuu wa nchi ambazo ndege inapitia. Kwanza kabisa kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Segio Mattarella kwamba:“ katika wakati ambapo ninajiandaa kuondoka kwenda Ureno katika fursa ya Siku ya vijana duniani; kwa kuhuishwa na furaha ya kukutana na vijana kutoka kila upande wa dunia kwa kuongozwa na imani na shuku ili kuinuka na kujiweka katika mwendo kuwa na nguvu za kukutana na Kristo na ili waweza kutiwa moyo katika kutafuta ukweli na maana ya maisha". Kwa hakika katka kushirikishana tumaini hili na wewe Bwana Rais, nimependelea kukutumia salamu zangu za dhati ambazo zisambazwe kwa waitalia wote kwa kukusindizwa kwa sala na matashi mema na matarajio!
Na telegram kwa Rais wa Ufaransa, Baba Mtakatifu Francisko ameandika kuwa: “ Nimepitia juu ya Ufaransa kwa ndege nikiwa njiani kueleka Ureno, ninakutumia salamu za matashi mema mhesh. na wazalendo wote kwa pamoja nikiwahakikisha sala zangu na kwa amani na ustawi wa taifa.” Kwa upande wa Rais wa Hispania, Baba Mtakatifu Francisko ameandikia Mfalme Pilipe VI kuwa: “Ninakutumia salamu zangu na wajumbe wote wa familia ya kifalme na watu wa Hispania, nikiwa juu ya nchi yako kuelekea Ureno. Ninakuhakikishia wewe uhakika wa sala zangu na juu ya yako ninakupa baraka kutoka kwa Mungu kwa ajili ya utulivu na furaha.
Ujumbe wa Rais Mattarella wa Italia
Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella,naye amemtumia Baba Mtakatifu Francisko kama jibu la ujumbe wake: “Ninataka zikufikie kwa dhati shukrani kwa ajili ya ujumbe ulionitumia katika wakati huu ambao unajiandaa kwenda Ureno”. Ziara ya kitume katika fursa ya Siku ya XXXVII ya Vijana duniani, inawakilisha fursa maalum ya kukutana na vijana wengi kutoka kila pande ya ulimwengu ambayo itashuhudia urafiki na katika imani ya kuamini wakati ujao na utashi wa vijana katika ulimwengu jumuishi zaidi na mshikamano. Ninakuelekeza Baba Mtakatifu wazo langu la kina kwa kuungana na mwelekeo wa kina kwako”.
Ziara ya 42 ya kitume
Kwa hiyo imeanza ziara ya 42 ya kitume ya Papa Francisko. Nchi ya Ureno iliyokuwa ikimsubiri Mfuasi wa Petro imekuwa na furaha kubwa kukaribisha Siku ya vijana duniani ambayo ilifunguliwa kwa ibada ya misa takatifu tarehe Mosi Agosti 2023 jioni jijini Lisbon. Misa ihiyo iliongozwa na Patriaki wa mji wa Lisbon, Kardinali Manuel Clementj. Kwa mujibu wa takwimu za ndani kuhusiana na washiriki itakuwa ni milioni moja ya vijana, ambapo pamoja na siku hiyo Baba Mtakatifu anatarajiwa kwenda huko Fatima katika madhabahu ya Mama Yetu wa Fatima ili kusali kwa ajili ya Amani akiwa na mahujaji wagonjwa mnamo Jumamosi tarehe 5 Agosti 2023.
Salamu wakati akiwa kwenye ndege
Baba Mtakatifu akiwa katika ndege kama kawaida yake amewasalimu na kuzungumza na waandishi wa habari wanaombatana naye katika hija hii. Aidha kulikuwa na barua moja ambayo Eva Fernández wa Radio Cope amemkabidhi Papa iliyoandikwa na kijana Pablo, wa Hispania mwenye wa miaka 21 aliyetamani sana kushiriki Siku ya vijana duniani lakini kwa bahati mbaya tarehe 15 Julai 2023 aliaga dunia kutokana na saratani, baada ya kuwa amejiunga na shirika la wakarmeli. Katika maneno yake ni yana matumaini kwa ajili ya vijana wote wanaoshiriki tukio hilo Lisbon na shauku ya kijana aliyempenda Yesu kwa dhati.
Kwa hiyo Papa Francisko amewasalimia karibu waandishi 80 wanaomsindikiza katika ziara hii ambapo Dk Bruni wakati anatoa utangulizi alisema kuwa karibu ndege imejaa na kwamba kwa uhakika kuna umati mkubwa Ureno ambao unasubiri kwa upande wa waandishi, kwa ishara na maneno yake kwa siku hizi. Na kwa upande wa Papa Francisko amesema: “Habari za asubuhi na asante kwa sindikizo hili na kwa ajili ya kazi zenu na sasa ninasalimia mmoja baada ya mwingine, asante,” alihitimisha.