WYD,Vatican :kuanzia 1-6 Agosti wanahija wanaombwa kusali kwa ajili ya siku ya vijana
Vatican News
Katika kipindi chote cha maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani(WYD), iliyopangwa kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti ijayo, mahujaji watakaofika mjini Vatican kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro vile vile wataalikwa kujumuika katika sala kwa ajili ya vijana waliokusanyika Lisbon na Baba Mtakatifu Francisko.
Kuabudu kauaniza saa asubuhi baada ya misa hadi saa 10.30 jioni
Mwaliko wa kuwasindikiza vijana kwa sala ya mahujaji kwenye Kaburi la Mtakatifu Petro utawahusu kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Misa inayoadhimishwa kwenye Kanisa kuu la Vatican na Ibada ya kila siku ya Ekaristi Takatifu katika Kikanisa cha Sakramenti Takatifu, ukiingia ni katika upande wa kulia wa Basilika. Nyakati za Kuabudu huanzia mwisho wa Misa ya asubuhi, inayoadhimishwa saa 2:30 asubuhi katika Kikanisa hicho na kuhitimishwa hadi saa 10:30 jioni.
Unaweza kupakua sala kupitia tovuti ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Kwa hiyo maelezo ya maandishi ya kukumbusha yatawekwa katika lango la kuingilia kwenye Kikanisa ili kuwakumbusha mahujaji wanaoingia kwa ajili ya Kuabudu juu ya mipango maalum ya Siku ya (WYD), ikiwa pia na maagizo ya kufikia ukurasa wa tovuti ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ambalo linalotolewa kwa ajili ya Siku ya Vijana ( WYD) na kupakua maandishi rasmi ya maombi ya sala ya Siku ya vijana (WYD) katika lugha kadhaa.