杏MAP导航

Tafuta

Wanahija wanaombwa kuungana katika sala ya kuombea  siku ya vijana duninai 1-6 Agosti 2023. Wanahija wanaombwa kuungana katika sala ya kuombea siku ya vijana duninai 1-6 Agosti 2023. 

WYD,Vatican :kuanzia 1-6 Agosti wanahija wanaombwa kusali kwa ajili ya siku ya vijana

Huu ni mwaliko kwa kila mjujaji anayeingia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwenye Kikanisa cha Kuabudu kilichopo kulia mwa Basilika hiyo,ili kuwasindikiza vijana hawa.

Vatican News

Katika kipindi chote cha  maadhimisho ya  Siku ya Vijana Duniani(WYD), iliyopangwa kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti  ijayo, mahujaji watakaofika mjini Vatican kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro vile vile  wataalikwa kujumuika katika sala kwa ajili ya vijana waliokusanyika Lisbon na Baba Mtakatifu Francisko.

Kuabudu kauaniza saa  asubuhi baada ya misa  hadi saa 10.30 jioni

Mwaliko wa kuwasindikiza vijana kwa  sala ya mahujaji kwenye Kaburi la Mtakatifu Petro utawahusu kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha, Misa inayoadhimishwa kwenye Kanisa kuu la Vatican na Ibada ya kila siku ya Ekaristi Takatifu katika Kikanisa cha Sakramenti Takatifu, ukiingia ni   katika upande wa  kulia wa Basilika. Nyakati za Kuabudu huanzia mwisho wa Misa ya asubuhi, inayoadhimishwa saa 2:30 asubuhi katika Kikanisa hicho na kuhitimishwa hadi saa 10:30 jioni.

Unaweza kupakua sala kupitia tovuti ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Kwa hiyo maelezo ya maandishi ya kukumbusha yatawekwa katika lango la kuingilia kwenye Kikanisa  ili kuwakumbusha mahujaji wanaoingia kwa ajili ya Kuabudu juu ya mipango  maalum ya Siku ya (WYD), ikiwa pia  na maagizo ya kufikia ukurasa wa tovuti ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ambalo linalotolewa kwa ajili ya Siku ya Vijana ( WYD) na kupakua maandishi rasmi ya maombi ya sala ya  Siku ya vijana (WYD) katika lugha kadhaa.

Sala kwa ajili ya kuombea WYD
31 Julai 2023, 18:05