ÐÓMAPµ¼º½

Kashfa ya mgogoro kati ya watu ambao wanashirikisha ubatizo sawa yaani Urussi na Ukraine. Kashfa ya mgogoro kati ya watu ambao wanashirikisha ubatizo sawa yaani Urussi na Ukraine.  Tahariri

Miezi tisa ya vita:jeraha ambalo linatutazama kama wakristo

Kashfa za mgogoro kati ya watu ambao wanashirikisha ubatizo sawa:imani na tamaduni za kidini haziwezi kamwe kuchukuliwa za kawaida na kudharauliwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tunakaribia mwezi wa tisa tangu kuanza kwa vita vya kutisha vya Urussi kuvamia Ukraine. Miezi tisa ni wakati ambapo maisha ya binadamu huchukua sura ndani ya umbu la mama na kisha kujifungua katika mwanga, lakini katika muktadha huu, Ukraine haijawa ujauzito wa maisha, bali ni wa kifo, chuki na uharibifu. Kuna kipengele kimoja cha vita hivi ambacho hatukumbuki kila mara kwamba ni mzozo unaohusisha watu wawili walio na imani moja katika Kristo na ubatizo uleule. Ukristo katika eneo hilo la kijiografia unahusishwa na ubatizo wa Rus ', uliokamilishwa mnamo mwaka wa 988, wakati Vladimir Mkuu alitaka familia yake na wakazi wa Kiev kupokea sakramenti katika maji ya Dnieper. Wakristo wa Urussi na Ukraine wanashiriki liturujia ya kimungu iliyo sawa na hali ya kiroho sawa na Makanisa ya Mashariki.

Leo hii kuna tabia ya kuficha ushirikishwaji huu wa pamoja wa imani na tamaduni  ya kiliturujia kwa sababu zinazohusiana na propaganda za vita: unapopigana, unapoua, lazima usahau uso na ubinadamu wa mwingine, kama nabii wa amani Don Tonino Bello alivyokumbusha. Na lazima hata usahau kwamba mwingine ana ubatizo sawa na wewe. Ukweli wa kile kilichozuka katika moyo wa Ulaya ambavyo ni vita kati ya Wakristo vinafanya kidonda kuwa kichungu zaidi cha wafuasi wa Yesu. Hatukabiliwi na mzozo wa kuainishwa katika mpango unaofaa wa "mgongano wa ustaarabu", nadharia ambayo ilipata umaarufu baada ya mashambulizi ya Kiislamu ya mnamo tarehe 11 Septemba 2001 ili kuashiria tofauti kati ya "sisi" na "wao". Hapana, hapa washambuliaji wanasoma Injili sawa na walioshambuliwa.

Kufadhaika kunakochochewa na uchunguzi huo, kunaweza kutuongoza kutafakari jinsi ambavyo ujumbe wa Injili bado unapaswa kuingia katika mioyo ya Wakristo na kueneza utamaduni wao, ili kuiga mfano wa Yesu ambaye akiwa kule Gethsemane alimwamuru Petro arudishe upanga katika ala yake. Inaweza hata kutushawishi kupanda juu ili kuhukumu na kuwatuliza wale wanaotaka kuweka alama ya tofauti kati ya Ukristo "wetu" na ule wa watu wanaochochea vita wakichanganya sanamu takatifu na mabango ya askari, wakihalalisha uchokozi na jeuri kwa mazungumzo ya kidini, kama tulivyokuwa tukifanya kufikia siku iliyotangulia na kama labda mtu angependa kufanya leo hii pia.

Lakini mtazamo huo ungekuwa kwetu njia rahisi tu ya kutoroka, aina ya kujiondoa ili kutoweka jeraha linalotokana na vita hivi vilivyo wazi. Kinyume chake mgogoro unaoendelea nchini Ukraine unatufundisha kwamba kuwa wa tamaduni moja, ikimaanisha utambulisho na utamaduni unaotokana na tangazo lile lile la kiinjili na kwamba  haitoshi kutuzuia kutumbukia katika ukatili wa ghasia, chuki na mauaji ya vita. Kubaki na jeraha lililo wazi kwa maana hiyo kunamaanisha kukumbuka kila siku kwamba imani yetu na tamaduni zetu za kidini haziwezi kamwe kuchukuliwa kuwa za kawaida au kuchukuliwa kuwa za kudharauliwa. Inamaanisha kukumbuka kwamba tunaweza kutenda kama Wakristo kwa neema tu, na si kwa mapokeo au utamaduni. Inamaanisha kukumbuka maneno ya Yesu: "Bila mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote", ili kurudi kuwa  wanyenyekevu wanaoomba kwake, walio hai na waliopo leo na wa amani yake.

 

14 Novemba 2022, 15:34