ĞÓMAPµ¼º½

2021.12.23 Heri za Noeli kwa Curia Romana 2021.12.23 Heri za Noeli kwa Curia Romana  Tahariri

Uongofu wa Sinodi kwa Curia Romana kwenye njia ya unyenyekevu

"Sinodi ni mtindo ambao sisi tulio hapa lazima tuongoke kwanza,kwa sababu Sekretarieti kuu,sio tu chombo cha urasimu na ukiritimba kwa jili ya mahitaji ya Kanisa la ulimwengu wote,lakini awali ya yote ni kiungo kinachoitwa kushuhudia".Amesema hayo Papa Francisko,katika hotuba yake wakati wa kutoa matashi mema ya Siku kuu ya Noeli alipokutana na Makardinali na Sekretarieti kuu ya Vatican.

ANDREA TORNIELLI

Kwa mtazamo wa kwanza inaweza kuonekana kama kitendawili: hata Curia Romana, ambayo kwa asili yake ni au inapaswa kuwa ya ushirika na sio kama mamlaka yenyewe bali kama ni ya huduma kwa  ajili ya utume wa ulimwengu wa Askofu wa Roma, inahitaji kuwa na uongofu wa kisinodi. Njia hii imeoneshwa na Papa Francisko, katika hotuba yake wakati wa kutoa Heri na matashi mema ya  Siku kuu ya Noeli alipokutana na Makardinali pamoja na Jumuiya nzima ya Sekretarieti kuu ya Vatican au Curia Romana. “Sinodi ni mtindo ambao sisi tulio hapa lazima tuongoke kwanza, kwa sababu Sekretarieti kuu, sio tu chombo cha urasimu na ukiritimba kwa jili ya mahitaji ya Kanisa la ulimwengu wote, lakini awali ya yote ni kiungo kinachoitwa kushuhudiaâ€, alisema Papa.

Papa Francisko karibu kwa kurefusha Katekesi yake ya Jumatano tarehe 22 Desemba, alikumbusha kwamba Fumbo lote la Noeli ambayo iko karibu mlangoni, linajikusanya katika neno moja la unyenyekevu. Inawezekana kulitambua tu ikiwa tuko tayari kujifuvua haki, vyeo, na nafasi, yaani ikiwa tunaachana kujiaminisha jinsi tulivyo, daima kuwa bora zaidi ya waliotuangulia. Inawezekana kutambua ikiwa tunaachana na ndoto za mipango ya mitume kwa kutaka kupanua na kuelekeza kile ambacho kinapaswa kifanyike kwa kupoteza mawasiliano na hali halisi iliyoteseka ya watu wetu waaaminifuâ€.

Kwa mkristo wa kweli, Askofu wa Roma anatukumbusha kuwa, kuondolewa, majukumu, vyeo na mavazi, sisi sote ni waombaji wanaohitaji kuponeshwa. Wote kuanzia na wa kwanza hadi wa mwisho. Licha ya kuwa vyeo vinavyofunikaâ€. Ni kuanzia na utambuzi huu tu ya kwamba hata hilo ni zawadi msingi wa neema, ambayo inaweza kutazamwa kwa macho mapya kile ambacho anashauri Papa. Uongofu wa Kisinodi hautakuwa na matokeo ya kazi nyingine kama ya urasimu ikiwa itatekelezwa kama wajibu, lakini kwa namna mpya ya kushirikiana, kwa kujiuliza na kwa kusikiliza mwingine. Kwa kuruhhusu namna hiyo Roho avuvie na kutupeleka hata mahali ambapo hatukuwahi kufikiria ili kuongeza nguvu ya umoja na kujenga uhusiano ambao unakwenda mbali na urahisi tu wa kazi. Na zaidi ya hayo kwa kutembea katika njia ya unyenyekevu na mtindo wa kisinodi, Sekretarieti kuu itageuka kuwa jumuiya. Jumuiya moja ambayo imeunda na wadhambi, wanaume na wanawake wadhaifu, ambao hawajifichi nyuma ya vyeo na nafasi walizo nazo, lakini ambao wanadhamiri kwamba wote kuanzia  na wa kwanza hadi wa mwisho ni mwenye kuhitaji msamaha, wa wokovu na wa uponywaji.

23 Desemba 2021, 15:38