“Fratelli tutti”,kwa ajili ya kufanya iwe Injili hai ya maisha
ANDREA TORNIELLI
Baaada ya mwaka mmoja tangu kuchapishwa kwake, bado ni haraka kuweza kutoa tathimini ikiwa Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu, utakuwa kama ule wa Laudato si’, ambao ni Hati nyingine muhimu sana ya Kipapa iliyotangazwa mnamo 2015, ambayo kama hapo awali haikuwahi kugunduliwa mahitaji ya watu wa mbali na Kanisa kwa kuanzisha mipango na juhudi za kweli kuanzia chini.
Fratelli tutti, kama ilivyo Laudato si’, zinatokana na mafundisho Jamii ya Kanisa na lazima kuepuka hatari ya kuzipunguza kama hati zinazoangalia dharura na matatizo ya sasa katika kupendekeza njia za kupitia kutokana na hayo tu. Badala yake ulinzi wa maisha, utunzaji wa kazi ya Uumbaji ambao umekabidhiwa, ikolojia ya binadamu na fungamani si mapendekezo ya kufanya chaguzi na ya bahati mbaya kwa ajili ya wakati uliopo, zinapata asili na msingi wa Neno la Mungu.
Na kwa namna hiyo ni mwaliko pia wa udugu, kwa kumfikiria mwingine, kwa namna yoyote aliyo nayo na mahali popote atokako na sio kama mwingine, lakini ni kama ndugu kutokana na kwamba ni mwana wa Mungu, sio bahati mbaya tu au kwa namna ya upendeleo maalum wa kipindi cha Maisha ya Kanisa, lakini kwa kuwa na mtazamo wa kina wa kiinjili. Miaka sita iliyopita, Papa Francisko katika Waraka wake wa Laudato si’ aliweza kuweka pamoja katika mkusanyiko wa mambo yaliyopo kati ya mgogoro wa mazingira, mgogoro wa kiuchumi na kijamii ambao ni wa haki na kuheshimu kazi ya Muumba ili iweze kuwa kitovu cha mwandamu na sio muungu pesa.
Mwaka mmoja uliopita kwa njia ya Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu, Papa alielekeza njia ya kupitia ili kufikia malengo ambayo ni kujitambua kuwa sisi ni kaka na dada, walinzi wa mmoja na mwingine na anafufuka kila ndugu ambaye anasimama tena. Lakini pia hata kwa yule ambaye hakupata zawadi ya kuwa na imani ya kikristo, anatambua pia ujumbe wa udugu ambao ni kama dawa pekee ya kuzuia kujiharibu kuelekea chuki na ubinafsi wa ushabiki. Hakuna jingine zaidi ya Injili kama inavyofundisha mfano wa Msamaria Mwema, ambao ni ya wa aina yake wa nje ya mazoea.
Hata ikiwa bado ni mapema kutathimini, matunda ya Waraka wa kipapa uliochapishwa mwaka mmoja uliopita, lakini zawadi na mbegu za matumaini hazikosekani. Inatosha kwa mwenye mazoea ya kusoma habari amepata fursa katika siku ziliopita kusoma juu ya habari za Dale Recinella mwakiri wa zamani wa Marekani ambaye alikuwa na bahati ya kutumia masaa yake machache mwanasheria wa zamani wa kifedha wa Wall Street ya Amerika ambaye kwa miaka mingi, pamoja na mkewe Susan, wameweza kujitolea maisha yao kuwasindikizwa wafungwa ambao wamekuwa wakisubiri kunyongwa katika Jeshi la Kifo huko Florida.
Wengi wao shukrani kwa urafiki wake, walikabiliana na suala la upatanisho na Mungu. Dale alitambua Yesu katika ndugu hao na kwa maana hiyo licha ya ugumu na kutokuelewana alisema jinis ambavyo anahitaji sio chini ya vile wanavyomuhitaji. Macho yake yakiwa yamejaa machozi, alieleza kuwa ujumbe wa Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu, kila neno na kila ishara ya Papa Francisko, kwake yeye ilikuwa ni kama tendo la kuweka damu, ambayo inasaidia kuishi na kwenda mbele. Kuna watu wengi ulimweguni, ambao wako mbali ya Matangazo ya vyombo vya habari na mikutano mikuu,na ambao kwa kutazama namna hiyo ushuhuda wa mfuasi wa Petro wanauishi ujumbe huo wa Maisha yao kupitia Injili iliyo hai.