Papa arudi Castel Gandolfo karibu siku moja!
Vatican News
Papa Leo XIV alirudi Castel Gandolfo kwa chini ya siku moja. Kwa mujibu wa taarifa fupi ya Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican iliyotolea inasomeka: "Jioni hii, (Septemba 8), Papa Leo XIV atasafiri hadi Jumba la Barberini huko Castel Gandolfo na ataendelea na shughuli zake kutokea hapo hadi kesho, wakati hakuna mkutano uliopangwa.” Taarifa hiyo iliendelea kwamba: "Papa atarejea Vatican kesho mchana" (yaani tarehe 9 Septeemba).
Na ikumbukwe kwamba, Papa alikuwa ametumia likizo ya majira yakiangaza katika kijiji cha Lazio kutoka Julai 6 hadi 22, kabla ya kurejea kwa siku chache katikati ya mwezi Agosti kwa Maadhimisho ya Kupalizwa kwa Bikira Maria mbinguni na tarehe 5 Septemba, vile vile Papa Leo XIV alitembelea Borgo Laudato si', na kuuzindua rasimi, mpango ulioanzishwa kwenye hekta 55 ambazo hapo awali zilikuwa za Majumba ya Kipapa, kukutana na wafanyakazi wanaotunza zaidi ya aina elfu tatu za mimea iliyopo.