ÐÓMAPµ¼º½

Maaskofu wa Kanisa katoliki. Maaskofu wa Kanisa katoliki.  (Vatican Media)

Maaskofu 192 wapya walioteuliwa wanashiriki kozi za mafunzo jijini Vatican

Papa Leo XIV atakutana na kundi la maaskofu 192 Alhamisi tarehe 11 Septemba katika Ukumbi wa Sinodi.Kozi ya mafunzo ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ilianza tarehe 4 Septemba na kuhudhuriwa na maaskofu wapya 78 walioteuliwa.Kozi hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Maaskofu,ilianza tarehe 3 Septemba na kuhudhuriwa na watu 114. Washiriki hawa walipitia Mlango Mtakatifu pamoja tarehe 6 Septemba na kushiriki Misa Takatifu ya kutangazwa Watakatifu wapya Acutis na Frassati,Septemba 7.

Vatican News

Asubuhi ya Alhamisi, tarehe 11 Septemba, katika Ukumbi wa Sinodi, Baba Mtakatifu Leo XIV atawapokea na kukutana mjini Vatican maaskofu mia moja tisini na wawili kutoka mabara matano ambao tangu tarehe 3 Septemba 2025 wamekuwa wakishiriki katika mafunzo yanayoendelezwa na Baraza la Kipapa Uinjilishaji (Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa mapya malalia) na Baraza la Kipapa la  Maaskofu.

Mafunzo kwa Shughuli za Kichungaji

Kozi hiyo iliyoandaliwa na Baraza la  Kipapa la Maaskofu kwa mada ya "Shahidi na Watangazaji wa Matumaini Walioanzishwa Katika Kristo," kuanzia tarehe 3 Septemba  itahitimishwa Alhamisi tarehe 11 Septemba 2025. Fursa hii ya mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Sinodi mjini Vatican, yanawalenga Maaskofu walioteuliwa katika mwaka uliopita(2024). Imeundwa kama mfululizo wa mikutano juu ya mada ambazo zinaweza kusaidia kwa shughuli za kichungaji na za kiutawala, na pia kwa tafakari ya kibinafsi na ya kijamii katika majimbo yao. Kozi hizo hufundishwa na wakuu wa Curia Romana na watu wa kikanisa na wasio wa kikanisa ambao ni wataalam katika maeneo yao ya utaalamu.

Kuzingatia  Utamadunisho

Kozi ya mafunzo kwa Maaskofu wapya, iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji (Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Malia), ilianza asubuhi ya Alhamisi, tarehe 4 Septemba 2025. Siku ya Ijumaa, tarehe 5 Septemba, mkazo ulikuwa juu ya mahitaji ya dharura ya utamaduni, wakati Jumamosi, Septemba 6, maaskofu walipitia Mlango Mtakatifu, na walishiriki Misa ya Jubile, na kuheshimu masalio ya Mtume katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Siku ya Dominika tarehe 7 Septemba, Maaskofu wote walishiriki katika Misa Takatifu ya Kutangazwa Watakatifu kwa Wenyeheri Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis.

Siku zilizoshirikishwa

Washiriki wa kozi zote mbili walishiriki siku kadhaa pamoja, ikiwa ni pamoja na ile ya Septemba 6, na kifungu kupitia Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro. Na zile za Septemba 8 na 9, zilizoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kwa kuhitimishwa na tafakari ya Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican  kuhusu "Kazi ya Kiti Kitakatifu, Vatican  katika ulimwengu wa utandawazi kwa ajili ya matumaini na amani." Muundo huu unakusudiwa kama wakati wa ushirikiano, kuelewana, na uwezekano wa kujenga uhusiano kati ya Makanisa tofauti mahalia.

Fursa ya kukutana na kujifunza

Maaskofu 78 walijiandikisha kwa ajili ya kozi ya Uinjilishaji, huku maaskofu  114 wakishiriki katika kozi iliyoandaliwa na Baraza la kipapa la  Maaskofu. Miongoni mwa hao wa mwisho, ni maaskofu watano kutoka Makanisa Katoliki ya Mashariki na Maaskofu watano waliowekwa wakfu hivi karibuni ambao wananyadhifa katika Curia Romana. Kozi za malezi kwa maaskofu walioteuliwa hivi karibuni zimekuwa kipengele cha kawaida cha programu ya mwezi Septemba ya Curia Romana.

Maaskofu 192 watakutana na Papa Septemba 11
09 Septemba 2025, 17:36