Maaskofu 192 wapya walioteuliwa wanashiriki kozi za mafunzo jijini Vatican
Vatican News
Asubuhi ya Alhamisi, tarehe 11 Septemba, katika Ukumbi wa Sinodi, Baba Mtakatifu Leo XIV atawapokea na kukutana mjini Vatican maaskofu mia moja tisini na wawili kutoka mabara matano ambao tangu tarehe 3 Septemba 2025 wamekuwa wakishiriki katika mafunzo yanayoendelezwa na Baraza la Kipapa Uinjilishaji (Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa mapya malalia) na Baraza la Kipapa la Maaskofu.
Mafunzo kwa Shughuli za Kichungaji
Kozi hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu kwa mada ya "Shahidi na Watangazaji wa Matumaini Walioanzishwa Katika Kristo," kuanzia tarehe 3 Septemba itahitimishwa Alhamisi tarehe 11 Septemba 2025. Fursa hii ya mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Sinodi mjini Vatican, yanawalenga Maaskofu walioteuliwa katika mwaka uliopita(2024). Imeundwa kama mfululizo wa mikutano juu ya mada ambazo zinaweza kusaidia kwa shughuli za kichungaji na za kiutawala, na pia kwa tafakari ya kibinafsi na ya kijamii katika majimbo yao. Kozi hizo hufundishwa na wakuu wa Curia Romana na watu wa kikanisa na wasio wa kikanisa ambao ni wataalam katika maeneo yao ya utaalamu.
Kuzingatia Utamadunisho
Kozi ya mafunzo kwa Maaskofu wapya, iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji (Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Malia), ilianza asubuhi ya Alhamisi, tarehe 4 Septemba 2025. Siku ya Ijumaa, tarehe 5 Septemba, mkazo ulikuwa juu ya mahitaji ya dharura ya utamaduni, wakati Jumamosi, Septemba 6, maaskofu walipitia Mlango Mtakatifu, na walishiriki Misa ya Jubile, na kuheshimu masalio ya Mtume katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Siku ya Dominika tarehe 7 Septemba, Maaskofu wote walishiriki katika Misa Takatifu ya Kutangazwa Watakatifu kwa Wenyeheri Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis.
Siku zilizoshirikishwa
Washiriki wa kozi zote mbili walishiriki siku kadhaa pamoja, ikiwa ni pamoja na ile ya Septemba 6, na kifungu kupitia Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro. Na zile za Septemba 8 na 9, zilizoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kwa kuhitimishwa na tafakari ya Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican kuhusu "Kazi ya Kiti Kitakatifu, Vatican katika ulimwengu wa utandawazi kwa ajili ya matumaini na amani." Muundo huu unakusudiwa kama wakati wa ushirikiano, kuelewana, na uwezekano wa kujenga uhusiano kati ya Makanisa tofauti mahalia.
Fursa ya kukutana na kujifunza
Maaskofu 78 walijiandikisha kwa ajili ya kozi ya Uinjilishaji, huku maaskofu 114 wakishiriki katika kozi iliyoandaliwa na Baraza la kipapa la Maaskofu. Miongoni mwa hao wa mwisho, ni maaskofu watano kutoka Makanisa Katoliki ya Mashariki na Maaskofu watano waliowekwa wakfu hivi karibuni ambao wananyadhifa katika Curia Romana. Kozi za malezi kwa maaskofu walioteuliwa hivi karibuni zimekuwa kipengele cha kawaida cha programu ya mwezi Septemba ya Curia Romana.