ĐÓMAPµĽş˝

Papa Leo XIV:Hatupaswi kujiuzulu kwa kuenea kwa mantiki ya migogoro na silaha!

Katika kutangaza dogma ya Kupalizwa mbinguni,wakati tukio la kutisha la Vita vya Pili vya Kidunia ambavyo bado vilikuwa bado vinaunguza Papa,Pio XII aliandika:“Tunapasa kutumainia kwamba wote wanaotafakari juu ya mfano mtukufu wa Maria wataendelea kusadikishwa zaidi kuhusu thamani ya maisha ya mwanadamu,” alitumaini kwamba“maisha ya mwanadamu hayapotezwe tena kwa kuchochea vita.”Ni kwa jinsi gani maneno haya yanafaa sana!Ni maneno ya Papa bara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Agosti 15.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika lango la Jumba la Kipapa huko Castel Gandolfo,  siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, tarehe 15 Agosti 2025, alisema: “Leo tunataka kukabidhi ombi letu la amani kwa maombezi ya Bikira Maria aliyepalizwa  mbinguni. Yeye kama Mama anateseka kwa maovu yanayowatesa watoto wake, hasa watoto wadogo na wanyonge. Amethibitisha hili mara nyingi kwa karne nyingi kwa ujumbe na maonesho.”

Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, huko Castel Gandolfo
Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, huko Castel Gandolfo   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kusema kuwa: “Katika kutangaza dogma ya Kupalizwa mbinguni, wakati tukio la kutisha la Vita vya Pili vya  Kidunia ambavyo vilikuwa bado moto vinaunguza,  Papa, Pio XII aliandika: “Tunapaswa kutumainia kwamba wote wanaotafakari juu ya mfano mtukufu wa Maria wataendelea kusadikishwa zaidi kuhusu thamani ya maisha ya mwanadamu,” na alikuwa na matumaini kwamba  â€śmaisha ya mwanadamu hayapotezwi tena kwa kuchochea vita” (Katiba ya Kitume Munificentissimus Deus ).

Waamini katika uwanja wa Castel Gandolfo
Waamini katika uwanja wa Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Ni kwa jinsi gani maneno haya yanafaa sana! Kwa bahati mbaya, hata leo tunahisi kutokuwa na msaada katika kukabiliana na kuenea kwa jeuri duniani kote, inazidi kuwa kiziwi na kutokuwa na hisia kwa kila msukumo wa binadamu. Licha ya hayo hatupaswi kupoteza tumaini: Mungu ni mkuu kuliko dhambi ya wanadamu. Hatupaswi kujiuzulu kwa kuenea kwa mantiki ya migogoro na silaha.

Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@VATICAN MEDIA)

Pamoja na Maria, tunaamini kwamba Bwana anaendelea kuwasaidia watoto wake, akikumbuka huruma yake. Ni ndani yake tu ndipo inawezekana kugundua tena njia ya amani.

Papa Leo XIV aliendelea kutoa salamu zake kwa wote, mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali. Aliwasalimia jumuiya ya uinjilishaji ya Chuo kikuu kutoka Honduras; familia za Harakati ya Upendo wa Familia, ambao wamehitimisha Mafungo  yao ya Kiroho; na kikundi cha "Mtakatifu Rita" cha wanandoa na wachumba. Heri na  siku kuu njema kwa wote!

Papa huko Castel Gandolfo
Papa huko Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)
Papa Baada ya Malaika wa Bwana,Agosti 15
15 Agosti 2025, 14:13