Papa Leo XIV:Haitoshi kukiri kwa maneno Yesu,bali kuvuka mlango mwembamba wa Msalaba
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 24 Agosti 2025 , kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Kwa kudadavua Injili ya siku, Papa Leo alianza kusema: “Katikati kitovu cha Injili ya leo(Lk 13,22-30) tunapata sura ya “mlango mwembamba” ulitumiwa na Yesu ili kujibu maswali kadhaa ikiwa niwachache ambao wanaokoka; Yesu alisema: “jitahidi kuingia mlango mwembamba kwa sababu na wambia wengi, watatafuta kuingia, lakini hawataweza.”(Lk 13,24). Kwa mtazamo wa kwanza, sura hii inafanya kuibuka maswali kadhaa: ikiwa Mungu ni Baba wa upendp na wa huruma, ambaye daima anabaki mikono iliyofunguliwa wazi kwa ajili ya kutukaribisha, kwa nini Yesu anasema kwamba mlango wa wokovu ni mwembamba?
Kwa hakika Papa aliongeza kusema “Bwana hataki kutukatisha tamaa. Maneno yake kinyume chake utafikiri, yanasadia hasa kukung’uta majivuno ya wale wanaofikiri kuwa wameokolewa tayari, ya wale ambao wanafanya mazoea ya kidini, na kwa hiyo wanahisi wako tayari sawa. Kiukweli, wao hawakutambua kuwa haitoshi kutumiza matendo ya kidini ikiwa hayo hayabadilishi moyo: Bwana hataki ibada inayotengenisha maisha, na hapendezwi na dhabihu na sala, ikiwa hazipelekei kuishi kwa upendo kuelekeza ndugu na kutenda haki.” Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu alithibitisha kuwa “watakapojiwakilisha mbele ya Bwana kwa kudai kwamba walikula na kunywa na Yeye na kuwa walimsikiliza mafundisho yake, watasikia akiwajibu: “Sijuhi ninyi ni wa wapi? Nendeni mbali nami, nyinyi wahudumu wasio na haki!
Papa Leo aliongeza kusema: “uchochezi huo ni mzuri ambao unatufikia kutoka katika Injili ya leo: wakati mwingine inaweza kutokea kuhukumu aliye mbali na Imani, Yesu anatuweka kwenye mgogoro, “uhakika /usalama wa waamini.” Yeye kwa dhati, anatuambia kuwa haitoshi kukiri kwa maneno, kula na kunywa Naye kwa kuadhimisha Misa ya Ekaristi na kujua vizuri mafundisho ya kikristo. Imani yetu ni ya dhati ikiwa inakumbatia maisha yetu yote, ikiwa inageuka kigezo cha chaguzi zetu, ikiwa inatufanya kuwa wanaume na wanawake ambao wanajibidisha katika wema na kujihatarisha katika upendo binafsi kama alivyofanya Yesu; Yeye hakuchagua njia rahisi ya mafanikio au ya nguvu, lakini pamoja na kutuokoa, alitupenda hadi kuvuka katika“mlango mwembamba”wa Msalaba.
Yeye ni kipimo cha Imani yetu, Yeye ni mlango ambao tunapaswa kuuptia ili kuweza kuokolewa (Yh 10,9), kwa kuishi upendo huo huo na kugeuka kwa maisha yetu, wahudumu wa haki na wa amani. Wakati mwingine, hii ina maana ya kutimiza chaguzi ngumu, na isiyo ya kawaida, kupambana binafsi dhidi ya ubinafsi na kutenda kwa ajili ya wengine, kutunza wema mahali ambamo utafikiri matinki za ubaya zinaoneshwa wazi na mengine. Lakini kwa kuvuka kizingiti hiki, tunagundua kuwa maisha yanafunguliwa mbele yetu kwa namna mpya, na tangu wakati huo tutaingia katika moyo mpana wa Mungu na katika furaha ya milele ambaye Yeye alituandalia.
Baba Mtakatifu kwa kuhitimisha tafakari yake aliomba tumgeukie Bikira Maria ili atusaidie kuvuka kwa ujasiri Mlango mwembamba, wa Injili na kwa namna hiyo tunaweza kujifungulia kwa furaha katika upendo mpana zaidi wa Mungu Baba!