MAP

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu jioni, tarehe 4 Agosti 2025 amekwenda kumtembelea na kumjulia hali kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania. Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu jioni, tarehe 4 Agosti 2025 amekwenda kumtembelea na kumjulia hali kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania.   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV Amtembelea Kijana Ignacio Gonzàlvez Hospitalini

Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania, alipata changamoto ya afya na kulazimika kulazwa kwenye Hospitali ya Bambin Gesù iliyoko mjini Roma. Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu jioni, tarehe 4 Agosti 2025 amekwenda kumtembelea na kumjulia hali kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuzungumza na kuwafariji wazazi wa kijana huyu na wamemshukuru.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Dominika tarehe 3 Agosti 2025 ameongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo kwa vijana na kuhudhuriwa na: Vijana zaidi ya milioni moja kutoka katika nchi 146; Mapadre 7,000 na Maaskofu ni 450, na wadau wa tasnia ya mawasiliano walikuwa ni 850, matendo makuu ya Mungu. Baada ya maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo kwa vijana iliyonogeshwa na kauli mbiu: “Vijana mahujaji wa matumaini” Baba Mtakatifu Leo XIV ametangaza kwamba, Maadhimisho ya Siku ya Vijana Ulimwenguni kwa Mwaka 2027 Jimbo kuu la Seoul, Corea ya Kusini, yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 3 hadi 8 Agosti 2027 na kwamba, maadhimisho haya yatanogeshwa na kauli mbiu; “Jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” Yn 16:33.

Bikira Maria ni faraja na matumaini ya Kanisa linalosafiri hapa duniani
Bikira Maria ni faraja na matumaini ya Kanisa linalosafiri hapa duniani   (@Vatican Media)

Matumaini yaliyomo ndani ya nyoyo za waamini ndiyo yanayowapatia nguvu na jeuri ya kutangaza na kushuhudia ushindi wa Kristo Mfufuka dhidi ya dhambi na mauti. Kwa hakika anasema, Baba Mtakatifu Leo XIV vijana wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa matumaini hadi miisho ya dunia. Amewakaribisha vijana wengi zaidi huko Seoul, Corea ya Kusini, ili kwa pamoja waweze kuendeleza ndoto na matumaini. Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania, alipata changamoto ya afya na kulazimika kulazwa kwenye Hospitali ya Bambin Gesù iliyoko mjini Roma.

Ignacio Gonzalves alipata changamoto ya afya wakati wa mkesha wa Jubilei
Ignacio Gonzalves alipata changamoto ya afya wakati wa mkesha wa Jubilei   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu jioni, tarehe 4 Agosti 2025 amekwenda kumtembelea na kumjulia hali kijana Ignacio Gonzálvez, kutokana Hispania. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuzungumza na kuwafariji wazazi wa kijana huyu. Mwishoni, Baba Mtakatifu amewasalimia pia wagonjwa waliolazwa kwenye Wodi ya Saratani, baadaye amekutana na kusalimiana pia baadhi ya vijana wagonjwa wakiwa na wazazi wao, baadhi ya wafanyakazi wa hospitalini na baadaye, amesali pamoja nao na hatimaye kuwapatia baraka zake za kitume! Wazazi wa kijana Ignacio Gonzálvez, aliyepata changamoto ya ugonjwa wakati wa mkesha wa Jubileo ya Vijana, Jumamosi tarehe 2 Agosti 2025 wamemshukuru Baba Mtakatifu Leo XIV kwa: Neno la Mungu, uwepo wake na faraja na kwamba, amewataka kusimika imani na matumaini yao katika mapenzi ya Mungu.

Wapapa Wagonjwa

 

05 Agosti 2025, 15:34