ĐÓMAPµĽş˝

2025.08.02 Wawakilishi wa kuongoza Mkesha wa Jubilei ya vijana huko Tor Vergata. 2025.08.02 Wawakilishi wa kuongoza Mkesha wa Jubilei ya vijana huko Tor Vergata.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akutana na wasanii wauhishaji wa mkesha wa vijana huko Torvergata

Papa Leo XIV alikutana katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican,Agosti 2 asubuli na wanamuziki,waigizaji na watangazaji ambao watachangamsha hafla ya Jubilei ya Vijana huko Tor Vergata:“Muziki,ngoma na aina nyingine nyingi za kisanii ni zawadi ambazo Bwana ametupatia,na kujitolea kwenu mchana huu ni zawadi kwa ajili yetu sote na kwa Kanisa zima."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wakati mamia elfu ya vijana tayari wamekwishafika kwenye uwanja wa Tor Vergata ili kujionea siku mbili za mwisho za Jubilei yao, ikiwa ni pamoja na mkesha na Baba Mtakatifu usiku huu na Misa ya kufunga Dominika tarehe 3 Agosti 2025, Papa Leo XIV alikutana katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican na wasanii, wanamuziki, waigizaji, na  watangazaji ambao watahuisha tukio la kabla ya Mkesha kuanzia saa 9:00 kamili alisiri  hadi saa 8.00 usiku. Kundi hili lilisindikizwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji na ambaye katika salamu zake za mwanzo kwa ufupi alimshukuru Baba Mtakatifu kwa moyo. “Ninakushuku kwa mkutano huu uliopenda usio rasmi."

Papa akutana na wasanii watakaongoza mkesha wa vijana
Papa akutana na wasanii watakaongoza mkesha wa vijana   (@Vatican Media)

Askofu Mkuu Fisichella alisema kuwa: "Tutaanza mkutano wetu hadi wewe utakapowasili Baba Mtakatifu kuanza mkesha. Hawa watawahuisha vijana wetu, ambao tayari wako njiani, wengine tayari wamefika. Asante kwa moyo wote kwa wakati huu ambao tumetamani sana. Asante!”

Kwa upande wa Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kwa salamu ya asubuhi na kuwashukuru kwa mambo mengi. Nilitaka kuwa na mkutano huu mdogo, tuseme kama familia, kukutana nanyi asubuhi ya leo, kujua uzuri, sanaa, muziki, vipaji vyote mnavyotoa kwa hadhira hii kubwa tuliyo nayo jijini Roma siku hizi. Zaidi ya nusu milioni, wanasema, au labda vijana milioni moja ambao wametoka katika nchi nyingi ulimwenguni pote.

Papa akutana na wasanii
Papa akutana na wasanii   (@Vatican Media)

Kwangu mimi, ni fursa, baraka kuweza kushiriki katika utume huu, katika huduma hii, kama Askofu wa Roma, kama Baba Mtakatifu, nikijua juu ya imani, shauku, na furaha tunayoshiriki na ambayo inatoa sauti kwa kile tulicho nacho mioyoni mwetu, ambayo ni juu ya hamu yote ya kupata furaha na upendo; kupata uzoefu wa imani pia kupitia karama ambazo Bwana ametupatia kama vile: muziki, ngoma, na aina nyingi za kisanii ambazo mtashiriki mchana wa leo na vijana.”

Baba Mtakatifu Leo XIV  alisisitiza kuwa: “Hakika ni zawadi kwa ajili yetu sote na kwa Kanisa zima, na ninakushukuru kwa dhati. Asante kwa wakati huu, na ninamwomba Mungu awabariki na kuwasaidia kuwasindikiza vijana hawa ambao wanahitaji sana kupata furaha ya kweli, furaha ya kweli ambayo sisi sote tunaipata katika Yesu Kristo. Ninawatakia heri njema na asante nyingi!” Baba Mtakatifu alihitimisha.

Papa na wasanii wa kuburudisha vijana Torv Vergata
02 Agosti 2025, 13:00