ĐÓMAPµĽş˝

2025.08.30 Papa akutana na Bwana Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe 2025.08.30 Papa akutana na Bwana Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV akutana na Rais wa Zimbabwe,Bw.Mnangagwa

Jummosi tarehe 30 Agosti,Papa Leo XIV alikutana na Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Bwana Mnangagwa,kisha rais huyo akakutana na Sekretarieti ya Vatican."Wakati wa mazungumzo ya dhati katika Sekretarieti ya Vatican ilibanishwa uhusiano mzuri kati ya Vatican na Zimbabwe."Kisha tahadhari ilitolewa kwa nyanja mbalimbali za hali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi ya nchi,hasa ushirikiano wake na Kanisa mahalia kuhusu mazingira, elimu na afya.”

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumamosi tarehe 30 Agosti alikutana na Bwana Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe. Kwa mjibu wa taarifa kutoka Vyombo vya habari, Vatican imebainisha kuwa: "Leo tarehe 30 Agosti 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV amempokea kwa mkutano, katika Jumba la Kitume la Vatican, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican  wa Uhusiano wa Kimataifa na Mashirika ya Kimataifa."

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi   (@VATICAN MEDIA)
Papa na ujumbe kutoka Zimbabwe
Papa na ujumbe kutoka Zimbabwe   (@VATICAN MEDIA)

Taarifa hiyo aidha inaongeza kusema: “Wakati wa mazungumzo ya dhati katika Sekretarieti ya Vatican  ilibanishwa uhusiano mzuri kati ya Vatican  na Zimbabwe. Kisha tahadhari ilitolewa kwa nyanja mbalimbali za hali ya kisiasa na kijamii na kiuchumi ya nchi, hasa ushirikiano wake na Kanisa mahalia kuhusu mazingira, elimu na afya.” Wakati wa mijadala hiyo, pia kulikuwa na “kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kikanda, yakisisitiza umuhimu wa kukuza ushirikiano wa pande nyingi, mazungumzo na ushirikiano kati ya mataifa.”

Rais alikutana na Sekretarieti ya Vatican
Rais alikutana na Sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)
Kardinali Parolini akisalimiana na Rais wa Zimbabwe
Kardinali Parolini akisalimiana na Rais wa Zimbabwe   (@Vatican Media)
Papa na rais wa Zimbabwe
30 Agosti 2025, 13:56