Papa Leo XIV;Septemba Mosi atafungua Mkutano Mkuu wa Shirika la Mt.Agostino
Vatican News.
Baba Mtakatifu Leo XIV atafungua Mkutano Mkuu wa 188 wa Shirika la Mtakatifu Agstino mnamo tarehe Mosi Septemba 2025. Siku ile ile itakuwa kumbukumbu ya kujiunga kwake unovisi mnamo mwaka 1977, ambapo Papa ataongoza Misa saa 12:00 jioni masaa ya Ulaya, Katika Basilika ya Mtakatifu Agostino huko Campo Marzio, jijini Roma. Misa hii itafungua kazi iliyopangwa hadi tarehe 18 Septemba katika Taasisi ya Kipapa ya Baba wa Kanisa (Augustinianum). Maadhimisho hayo yatarushwa mbashara na idhaa ya Italia ya Radio Vatican kuanzia saa 11:55 Jioni na itakuwa na maelezo katika lugha ya Kiitaliano, Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kijerumani, na Kipolandi. Itaweza pia kufuatwa kupitia utiririshaji wa sauti kwenye kurasa za lugha husika za Vatican News na kupitia video kwenye tovuti moja na kwenye kurasa husika za Facebook na YouTube.
Idadi ya washiriki katika Mkutano Mkuu wa Kiagostino
Jumla ya watu karibu mia moja Watawa wanahusika katika tukio hili muhimu, ambalo hufanyika kila baada ya miaka sita. Waagostinian 73 kutoka nchi 46 tofauti, wajumbe kutoka washirika wa Shirika hilo 41 watakuwa na haki ya kupiga kura. Hawa wanawakilisha Waagostinian 2,341 wakiwa na nyumba zao 395 zilizopo katika mabara matano, kama ilivyorekodiwa na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Kipapa hadi tarehe 31 Desemba 2024, na wameitwa kumchagua Mkuu mpya, wa 98, Ulimwenguni baada ya kuongoza kwa miaka 12 kwa Padre Alejandro Moral, ambaye amemaliza muhula wake wa pili. Siku za Mkutano Mkuu zitajumuisha vikao na mawasilisho ya marais wa mashirikisho ya watawa wa Kiagostinian na walei wa familia ya Agostinian, ambao hawana sauti hai katika uchaguzi.
Mnamo 2013, Misa iliongozwa na Papa Francisko
Miaka kumi na miwili iliyopita, alikuwa ni Hayati Papa Francisko ambaye alifungua Mkutano huo Mkuu, katika Basilika hiyo hiyo ya Kirumi, Mkutano Mkuu ambao ulihitimisha muhula wa miaka 12 ya Padre Robert Prevost ambaye, walifikiria kumwalika Bergoglio, Papa aliyeaga dunia hivi karibuni, "kuongoza, tarehe 28 Agosti, Misa ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu", kama alivyosimulia katika mahojiano ya mwisho kama Kardinali, yaliyotolewa kwa Vyombo vya Habari vya Vatican.
"Kwa mshangao mkubwa wa kila mtu," Papa Francisko alikubali na katika mahubiri yake alisisitiza kwamba "kutotulia kwa moyo ndiko kunaongoza kwa Mungu na upendo," akiongeza kwamba Mtakatifu Agostino anatualika kuweka uhai wa"kutotulia kwa kutafuta kiroho, kutotulia kwa kukutana na Mungu, kutokuwa na utulivu wa upendo." Papa wa Argentina alieleza kwamba "hazina ya Agostino ni mtazamo huu hasa: daima kwenda nje kwa Mungu, daima kwenda nje kuelekea kundi," na kuelezea Askofu wa Hippo kama "mtu aliyepasuka kati ya safari hizi mbili," "siku zote katika harakati," "siku zote bila utulivu! Na hii ndiyo amani ya kutotulia." Pia alihimiza "kuto 'binafsisha' upendo," na akamalizia kwa kueleza kwamba "kutotulia pia ni upendo, daima kutafuta, bila kuchoka, mema ya mwingine."