Papa anatoa salamu za rambirambi kwa kijana wa Kimisri aliyefari safari kuja Roma
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumamosi tarehe 2 Agosti 2025 amehuzunisha na habari za kifo cha ghafla cha kijana mmoja wa miaka 18 aitwaye Pascale Rafic, kilichotokea akiwa safarini kuja Roma akitokea Misri ili kuweza kushiriki Jubilei ya vijana.
Papa Leo XIV aliwasiliana na Askofu Jean-Marie Chami, wa Jimbo la Tarso na msaidizi wa Kanisa la Upatriaki wa Antiokia ya Kigiriki-Melkiti kwa ajili ya Misri, Sudan na Sudan Kusini, kuelezea ukaribu wake wa kiroho na kwa familia ya kijana huyo ikiwa ni pamoja na jumuiya nzima.
Baba Mtakatifu Leo XIV vile vile katika siku ya Jumamosi, tarehe 2 Agosti, asubuhi, alikutana na kikundi cha wanahija, waliokuwa safarini na kijana huyo aliyefariki dunia. Mkutano huo uliashirika hisia kali na ulikuwa na fursa ya kusali kwa ajili ya Roho ya marehemu na kukabiliana kiroho kwa ajili ya kijana huyo ambapo bado wameshtushwa kwa uchungu na tukio hilo.
Kwa ushiriki uchungu huo, na wale wote ambao wamekumbwa na mkasa huo wa ajabu, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwakikishia sala zake na kuomba Bwana nguvu na faraja kwa ajili ya familia, marafiki na wote ambao wanaomboleza kwa kumpoteza kijana huyo.