MAP

Amani  na iwe! Amani na iwe!  (@Vatican Media)

"Amani iwe nanyi:kuelekea amani isiyo na silaha na kupokonywa silaha:”Ni mada ya Siku ya Amani Duniani 2026!

Papa Leo XIV ametoa mada ya Siku ya Amani Duniani kwa 2026,kuwani: “Amani iwe nanyi:kuelekea amani ‘isiyo na silaha na kupokonywa silaha.”Kifungu kidogo cha Injili ya (Yohane 20,19,)kwa maneno ya Yesu mara tu alipowatokea wafuasi wake baada ya ufufuko.Kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Huduma Maendeleo Fungamani ya Binadamu imefafanua kuwa kuwa “Haitoshi kuomba amani bali imwilishwe katika mtindo wa maisha unaokataa vurugu zote!

Vatican News

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu imetoa taarifa juu ya Mada ya Iliyochaguliwa na  Papa Leo XIV kwa ajili ya Siku ya Amani duniani, kwa Mwaka 2026 kwamba ni: “Amani iwe nanyi:kulekea amani isiyo na silaha na kupokonywa silaha,” ambayo inatoa mwaliki kwa ubinadamu wote kukataa mantiki ya vurugu na ya vita, ili kukumbatia amani ya dhati inayojikita msingi juu ya upendo na juu ya haki.

Lazima kupokonya kila aina ya silaha

Ni lazima kupokonywa silaha, yaani, sio msingi wa woga, vitisho, au silaha; na kupokonya silaha, kwa sababu ina uwezo wa kusuluhisha mizozo, kufungua mioyo, na kutoa uaminifu, huruma na matumaini. “Haitoshi kuomba amani; lazima imwilishwe katika mtindo wa maisha unaokataa aina zote za vurugu, ziwe za kuonekana au za kimuundo. Salamu ya Kristo Mfufuka: “mani iwe nanyi” (rej Yh 20,19) ndiyo mwaliko unaoelekezwa waamini wote na wasio waamini, wahusuka wa kisiasa au sera za kisiasa na raia, ili kujenga Ufalme wa Mungu na kujenga pamoja wakati mstakabali mwanadamu na amani.

Mada ya Siku ya Amani 2026
26 Agosti 2025, 17:11