"Amani iwe nanyi:kuelekea amani isiyo na silaha na kupokonywa silaha:”Ni mada ya Siku ya Amani Duniani 2026!
Vatican News
Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu imetoa taarifa juu ya Mada ya Iliyochaguliwa na Papa Leo XIV kwa ajili ya Siku ya Amani duniani, kwa Mwaka 2026 kwamba ni: “Amani iwe nanyi:kulekea amani isiyo na silaha na kupokonywa silaha,” ambayo inatoa mwaliki kwa ubinadamu wote kukataa mantiki ya vurugu na ya vita, ili kukumbatia amani ya dhati inayojikita msingi juu ya upendo na juu ya haki.
Lazima kupokonya kila aina ya silaha
Ni lazima kupokonywa silaha, yaani, sio msingi wa woga, vitisho, au silaha; na kupokonya silaha, kwa sababu ina uwezo wa kusuluhisha mizozo, kufungua mioyo, na kutoa uaminifu, huruma na matumaini. “Haitoshi kuomba amani; lazima imwilishwe katika mtindo wa maisha unaokataa aina zote za vurugu, ziwe za kuonekana au za kimuundo. Salamu ya Kristo Mfufuka: “mani iwe nanyi” (rej Yh 20,19) ndiyo mwaliko unaoelekezwa waamini wote na wasio waamini, wahusuka wa kisiasa au sera za kisiasa na raia, ili kujenga Ufalme wa Mungu na kujenga pamoja wakati mstakabali mwanadamu na amani.