ÐÓMAPµ¼º½

Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 23 Julai 2025 amemtumia salam za heri na pongezi nyingi Rais Sergio Mattarella wa Italia kwa kuadhimisha kumbukizi la miaka 84 Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 23 Julai 2025 amemtumia salam za heri na pongezi nyingi Rais Sergio Mattarella wa Italia kwa kuadhimisha kumbukizi la miaka 84   (ANSA)

Rais Sergio Mattarella Kumbukizi ya Miaka 84 ya Kuzaliwa

Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 23 Julai 2025 amemtumia salam za heri na pongezi nyingi Rais Sergio Mattarella wa Italia kwa kuadhimisha kumbukizi la miaka 84 tangu alipozaliwa tarehe 23 Julai 1941 huko Palermo, Italia. Huyu ni Rais wa kumi na mbili wa Italia. Ni kiongozi ambaye ameonesha uthabiti na umakini katika maamuzi yake kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao mapana ya watu wa Mungu nchini Italia. Heri na baraka tele katika maisha na utume wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 23 Julai 2025 amemtumia salam za heri na pongezi nyingi Rais Sergio Mattarella wa Italia kwa kuadhimisha kumbukizi la miaka 84 tangu alipozaliwa tarehe 23 Julai 1941 huko Palermo, Italia. Huyu ni Rais wa kumi na mbili wa Italia. Baba Mtakatifu Leo XIV anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpatia fursa Rais Sergio Mattarella kuwaongoza watu wa Mungu nchini Italia kwa awamu ya pili, kuanzia mwaka 2022 huduma ambayo anaendelea kuitekeleza kwa upendo na unyenyekevu mkuu, licha ya matatizo, changamoto na fursa mbalimbali zinazoendelea kujitokeza katika maisha na uongozi wake. Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kumhakikishia sala zake kwa kazi na huduma anayoitoa kwa watu wa Mungu nchini Italia bila ya kujibakiza kwa sadaka na majitoleo mapana kwa ajili ya ujenzi wa umoja na mshikamano wa Taifa la Italia.

Raais Mattarella akiingia mjini Vatican ili kukutana na Papa Leo XIV
Raais Mattarella akiingia mjini Vatican ili kukutana na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kuwashirikisha furaha hii, wale wote walio karibu na Rais Mattarella. Anamshukuru na kumpongeza kwa ajili ya kutafuta na kudumisha amani ulimwenguni. Anamweka chini ya ulinzi na maombezi ya Bikira Maria pamoja na watakatifu walinzi wa Italia. Rais Mattarella ni kiongozi ambaye ameonesha uthabiti na umakini katika maamuzi yake kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao mapana ya watu wa Mungu nchini Italia, mfano bora wa kuigwa. Baba Mtakatifu anaungana na watu wote wa Mungu kumtakia heri na fanaka Rais Sergio Mattarella wa Italia anapoadhimisha kumbukizi ya Siku yake ya Kuzaliwa. Mwishoni, mwa ujumbe wake, Baba Mtakatifu Leo XIV amempatia Rais Sergio Mattarella baraka zake za Kitume.

Rais Sergio Mattarella
24 Julai 2025, 15:16