Papa atuma rambi rambi huko Congo,DR:Damu ya mashahidi iwe mbegu ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 28 Julai 2025 alituma telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Petro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican kufuatia na shambulizi kwenye Parokia moja ya Mwenyeheri Anuarite katika kijiji cha Komanda katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (RD). Tukio lililotokea usiku wa kuamkia Dominika tarehe 27 Julai 2025 na kusababisha zaidi ya vifo arobaini. Katika Ujumbe huo ulielekezwa kwa Askofu Mkuu wa Lubumbashi, Fulgence Muteba Mugalu, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini DRC(CENCO) kwamba, “Baba Mtakatifu Leo XIV amepata taarifa la shambulizi hilo kwa masikitiko makubwa ya kina katika Mkoa wa Ituri ambayo yalisabisha vifo vya waamini” mikononi mwa magaidi wa ADF.
Papa anaungana na familia na jumuiya kuonesha ukaribu wake
Papa Leo XIV kwa njia hiyo anaungana na familia na jumuiya ya kikristo iliyoguswa huku akionesha ukaribu wake na kuwahakikishia maombi yake. “Janga hili linatusukuma kufanya kazi zaidi kwa ajili ya maendeleo fungamani ya binadamu ya watu katika kanda hiyo wanaoteseka.”
Baraka kwa wana na mabinti wa DRC
Baba Mtakatifu Leo XIV anamuomba Mungu ili damu ya mashahidi hawo iweze kuwa mbegu ya kupanda amani, maridhiano , udugu na upendo kwa watu wote wa Congo. Katika muktadha huo anatuma baraka yake ya kitume kwa Parokia ya Mwenyeheri Anuarite wa Komando, kwa namna ya pekee familia nyingi zilizoguswa na msiba huo kwa wana na binti wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC na Taifa zima.