Katekesi ya Papa Leo XIV:Ili kuwa mfuasi wa Yesu hakuna njia za mkato!
Na Angella Rwezaula â Vatican.
Baada ya kipindi cha mapumziko, Baba Mtakatifu Leo XIV amerudi kuendelea na katekesi yake ya kila Jumatano, tarehe 30 Julai 2025. Katika muktadha wa mzunguko wa Katekesi ya Jubilei 2025 kuhusu âYesu Kristo Tumaini letu.â Maisha ya Yesu. Misemo, mada ya tafakari ya siku ilikuwa ni kuhusu âKiziwi.â Kwa kuongozwa na Injili ya Marko, inabainisha kuwa âwakiwa wamejawa na mshangao, walisema: âAmefanya mambo yote vema: anawafanya viziwi wasikie na mabubu waseme!â (Mk 7,37).
Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kusema kuwa âkatika katekesi hii tunahitimisha mchakato wa maisha ya umma ya Yesu yaliyojikita kwa mikutano, misemo na uponyaji. Hata katika wakati huu ambao tunaishi unahitaji kuponeshwa. Dunia yetu inapitia hali ya vurugu na chuki ambayo inaaibisha hadhi ya binadamu. Tunaishi katika jamii ambayo imeugua kwa sababu ya uchu wa miunganisho mingi ya vyombo vya habari: Tumeunganishwa kuzidi kiasi, kwa bomu la picha ambazo wakati mwingine hata za uwongo au kupindishwa.
Papa alikazia kusema: "Tumezidiwa na jumbe nyingi sana ambazo zinaibua ndani mwetu dhoruba za hisia zinazopingana. Katika muktadha huo inawezekana kuzaliwa ndani mwetu shauku ya kuzima yote. Tunaweza kufikia hata kupendelea kutosikia chochote kile. Hata maneno yetu yako hatarini kutoeleweka, na tunaweza kushawishika kujifungia katika ukimya, kutowasiliana mahali ambapo hata kwa karibu, hatuwezi kusema tena mambo rahisi na ya kina. Katika muktadha huo, Baba Mtakatifu Leo alipenda kujikita katika andiko la Injili ya Marko ambalo anatuwakilisha mtu asiyezungumza na wala kusikia(Mk,731-37).â
Papa Leo alisema kuwa âsawa sawa na kile ambacho kinaweza kutukumba hata sisi leo hii, mtu huyo labda aliamua kutozungumza tena kwa sababu alihisi kutoeleweka, na kuzima kila sauti kwa sababu alikatishwa tamaa na kujeruhiwa kwa kile ambacho alisikiliza. Kwa hakika si yeye aliyekwenda kwa Yesu ili kuponeshwa, lakini alipelekwa na watu wengine. Inawezakana kufikiria kwamba wale waliompeleka kwa Mwalimu, ndiyo walikuwa wana wasiwasi wa kujibagua kwake.â
Jumuiya ya kikristo iliona katika watu hawa kuwa hata picha ya Kanisa, ambayo inasindikiza kila mtu kwa Yesu ili asikilize neno lake. Tukio linajikita katika eneo la kipagani na kwa hiyo tuko katika mahali ambapo sauti nyingine zinadaikufunika ile ya Mungu. Katika tabia ya Yesu, inawezekana mwanozni kuonesha ajabu, kwa sababu alimchukua mtu huyo na kumpeleka pembeni(Mk 7, 33). Utafikiri ni kuibua kujibagua kwake, lakini kwa kutazama vema inatusaidia kutambua kinachojificha nyuma ya ukimya wa kujifunga mtu huyo, kama vile alikuwa ametambua mahitaji yake ya kina na ukaribu.
Yesu anatoa kwanza kabisa ukaribu wa kimya, kwa njia ya ishara ambayo inazungumza katika mkutano wa kina: anagusa masikio, na ulimi wa mtu huyo (Mk 7,33). Yesu hatumii maneno mengi, anasema jambo moja ambalo limsaidie katika wakati huo: âFungukaâ (Mk 7, 34). Marko analeta neno la kiaramaiko "effata" yaani karibu kutaka kusikia âkwa uhaiâ ule mlio na pumzi. Neno hilo, rahisi na zuri lina mwaliko ambao Yesu anamwelekea mtu huyo ambaye alianza kusikiliza na kuzungumza.
Hapa ni kama Yesu anataka kumwambia: Mfungulie dunia hii ambayo inamwogopesha! Mfungulie katika mahusiano ambayo yalimkatisha tamaa! âFunguka katika maisha ambayo uliacha na kukabiliana! Kujifungia kiukweli kamwe siyo suluhisho.â Baada ya mkutano na Yesu, mtu yule hakurudi kuona tu, lakini kwa usahihi. Neno hilo lililowekwa na mwinjili utafikiri ni kutaka kutuonesha jambo la zaidi kuhusu sababu ya ukimya wake. Labda mtu huyo aliacha kuzungumza kwa sababu utafikiri alisema maneno kwa namna isiyo sahihi, labda hakujisikia kustahili.
Papa Leo XIV alikazia kusema kuwa: âSisi sote tunafanya uzoefu wa kueleweka vibaya, na kutokujisikia kueweleka. Sisi sote tunahitaji kuomba Bwana ili kuponya namna yetu ya kuwasiliana, siyo tu kwa ajili ya kuwa na ufanisi zaidi, lakini hata kujizuia kuwafanyia wengine vibaya kwa maneno yetu. Kurudi kuzungumza kwa usahihi ni mwanzo wa safari, na bado sehemu ya kufikia. Yesu kiukweli anakataza mtu huyo asisimulia kile ambacho kilimtokea(Mk 7,36). Ili kumjua Yesu kweli inahitaji kutimiza safari, hitaji la kukaa na Yeye na kupitia hata Mateso yake.
Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Fisichella alisema "Tutakapomwona amenyenyekezwa na kuteseka, tutakapofanya uzoefu wa nguvu inayookoa ya Msalaba wake, ndiyo basi tutaweza kusema ya kuwa tunatambua kweli. Ili kuwa mfuasi wa Yesu hakuna njia za mkato." Baba Mtakatifu Leo XIV alihitimisha akisema kuwa âtumuombe Bwana kujifunza kuwasiliana kwa namna ya karibu na busara. Tuwaombee wale wote ambao wamejeruhiwa na maneno ya wengine. Tuombee Kanisa ili lisikosekane kamwe kazi yake ya kupeleka watu kwa Yesu, ili waweze kusikiliza Neno lake, waweze kuponeshwa na kwa namna ya kuwa wabebaji wa tangazo lake la wokovu.