杏MAP导航

Tafuta

2025.06.19 Papa atemebelea Kituo cha kurusha matangazo cha Radio Vatican huko Santa Maria di Galeria. 2025.06.19 Papa atemebelea Kituo cha kurusha matangazo cha Radio Vatican huko Santa Maria di Galeria.  (@Vatican Media)

Papa:wasio na hatia wengi wanakufa,inahitajika kutafuta amani pamoja!

Mwishoni mwa ziara yake katika Kituo cha usambazaji wa matangazo cha Santa Maria di Galeria,katika mahojiano na Tg1 Rai Papa Leo XIV alibainisha umuhimu wa huduma ya Radio Vatican,hasa kwa maeneo magumu zaidi kufikiwa na alizungumzia mpango wa nishati ya jua uliopangwa kwa ajili ya Kituo hicho kwamba ni "fursa nzuri ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi."

Na Alessandro De Carolis – Vatican.

"Ningependa kupyaisha ombi hili la amani ili kujaribu kwa gharama yoyote ile kuepuka matumizi ya silaha kwa kutafuta mazungumzo kupitia vyombo vya kidiplomasia. Ulinganisho uliofanywa pamoja ili kutafuta suluhisho kwa mkasa huo wa watu wengi wasio na hatia ambao wanakufa." Nje ya kizingiti cha Kituo cha kurushia matangazo ya masafa mafupi katika eneo la  Santa Maria di Galeria, nje ya Roma, ambako alikuwa ametumia sehemu yake ya asubuhi Juni 19 kugundua vifaa vilivyoambatana na zaidi ya miaka 90 ya kazi ya Radio Vatican jana na leo, Baba Mtakatifu  Leo XIV alisimama kwa dakika chache kwenye kipaza sauti cha mwandishi wa Vatican wa Tg1,  Ignazio Ingrao, ili kuthibitisha upya maombi hayo ya amani katika ulimwengu unaozidi kuzidiwa na ghadhabu za hapa na pale.


Daima ni neno zuri kutoka Radio Vatican

Papa Leo XIV, pia alijikita  kuelezea juu ya historia na mustakabali unaongojea Kituo cha Usambazaji wa matangazo ya masafa mafupi kilichoanzishwa mnamo mwaka 1957 na Papa Pio XII na leo hii kinachokusudiwa kutoa jibu kwa hatari zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mipango ya kisasa. "Sikujua Kituo hiki, antena za Radio Vatican," alisema Papa Leo XIV ambaye, kama asubuhi ya  tarehe 19 Juni,  wakati wa ziara yake huko  Santa Maria di Galeria, alisisitiza jinsi ilivyofaa kwake, akiwa mmisionari barani Amerika ya Kusini. "Baada ya kukatiza matangazo ya masafa mafupi ya kituo cha Papa kwa kutumia radio ndogo, mara nyingi hata milimani ambako hakukuwa na uwezekano mwingine wowote.” Na kisha  alisema "vivyo hivyo katika Afrika, wakati wa ziara zake akiwa mkuu wa Shirika la Waagostiniani, akisafiri katika nchi mbalimbali."

Mfumo wa nishati ya jua ni mfano mzuri kwa Ulimwengu

Kituo cha Santa Maria di Galeria sasa kiko kwenye njia iliyofuatiliwa kwa muda uliopita na Hayati  Papa Francisko, ambaye mwaka mmoja tu uliopita alianzisha kwa barua ya motu proprio ya “Fratello Sole”, kwamba kiwe na mfumo wa nishati ya jua kwa ajili ya matumizi huru ya nishati ya jua kwa  Mji wa Vatican. Kwa upande wake  Papa Leo XIV, alisema kuwa “ni fursa nzuri na dhamira kwa upande wa Kanisa kutoa katika ulimwengu mfano ambao ni muhimu sana." Aidha alisisitiza kwamba: “Kila mtu anajua athari za mabadiliko ya tabianchi na lazima kweli tutunze ulimwengu wote, wa viumbe vyote kama Papa Francisko alivyofundisha kwa uwazi."

Papa Leo kwa TG1
20 Juni 2025, 09:09