Leo XIV anatembelea Kituo cha kurusha matangazo huko Santa Maria di Galeria
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vaticani, katika fursa ya kumbukizi ya kupewa daraja la ukuani miaka 43 iliyopita, imebanisha kuwa "Asubuhi ya leo Papa Leo XIV alitembelea Santa Maria di Galeria, katika eneo la nje ya mipaka ambako kuna Kituo cha Radio cha Mawimbi Mafupi cha Radio Vatican, cha Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Alikutana na wafanyikazi wa kituo hicho, ambaye alizungumza nao, alitembelea chumba cha kupitisha masafa kilichoundwa na mbunifu Pier Luigi Nervi na akaketi kwenye chumba cha kudhibiti kwa matangazo mafupi ya masafa. Papa alijifunza kuhusu utendakazi wa antena, usafirishaji na mfumo wa kidijitali wa kufufua maafa, na pamoja na wafanyakazi alisherehekea kumbukizi ya miaka 43 ya ukuhani, ambayo inaangukia leo, kwa kiburudisho kidogo."
Katika taarifa hiyo aidha inabainisha kwamba "Baba Mtakatifu Leo akizungumza nao - "amekazia jinsi ambavyo wakati wa kazi yake ya kimisionari huko Amerika ya Kusini na Afrika ilikuwa na thamani kubwa kuweza kupokea matangazo ya masafa mafupi ya Radio Vatican, ambayo yanafika sehemu ambazo watangazaji wachache wanafanikiwa kufika," na akasisitiza tena "thamani ya kimisionari ya mawasiliano." Hatimaye, katika kuwabariki wote waliohudhuria, aliwashukuru kwa kazi iliyofanyika kwa uaminifu na mwendelezo, hata katika siku ya kusherehekea siku kuu ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo."
Baba Mtakatifu kadhalika alipata fursa ya kuchunguza eneo la ziada ambalo hadhi yake ina makubaliano na Serikali ya Italia ya 1951, ambayo, kwa Barua ya motu proprio ya Fratello Sole, mpango unachunguzwa kwa ajili ya mfumo wa nishati ya Jua ambao utahakikisha sio tu usambazaji wa umeme wa kituo cha radio, lakini pia mafao kamili ya nishati ya mji wa Vatican.
Kituo cha Radio kilizinduliwa na Papa Pio XII mnamo 1957. Ziara ya mwisho ya Papa katika Kituo cha Radio na eneo la Santa Maria di Galeria lililoanza 1991, mwaka ambao Papa Paulo II alikwenda huko.