ĐÓMAPµĽş˝

Katekesi ya Papa Leo XIV:Bwana anawatafuta wanaosubiri ili kuwapatia maana maisha yao!

Ni mwenye shamba la mizabibu,ambaye anakwenda kutafuta wafanyakazi wake.Ni wazi kwamba anataka kuanzisha uhusiano wa kibinafsi nao.Ni mfano unaotoa tumaini,kwa sababu unatuambia kuwa bwana anatoka mara kadhaa kuwatafuta wanaosubiri ili kuwapatia maana ya maisha yao,maana Mungu anapenda maisha yetu.Vijana,tusingoje bali tuitikie kwa shauku Bwana anayetuita tufanye kazi katika shamba lake la mizabibu.Ni Katekesi ya Papa Leo XIV,Juni 4,2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV ameongoza Katekesi yake Jumatano tarehe 4 Juni 2025 katika Uwanja wa Mtakatifu petro mjini Vatican ambayo imedhuriwa na takribani ya waamini na mahujaji wa Jubileio wapatao 35,000 ambao wakati wa kuzungua akiwa juu Gari la JeeP nyeupe waamini waliomba baraka na wengine wakitoa zawadi. Na zaidi aliwabariki watoto wengi sana, na vile vile kuweka saini juu yam pira wa baseball lakini vile vile kufanya ishara ya kivaa vikofia alivyokuwa watu wameleta na baadaye kuwarudishia.  Baada ya kufika kwenye jukaa aliendeleza katekesi ya Jubilei ya 2025 Yesu Kristo Tumaini letu. Maisha ya Yesu: kifungu cha nane kinachohusu: “Wafanyakazi katika Shamba la  Bwana: “enendeni nanyi katika shamba.” Papa Leo kwa hiyo kwa kuongoza na somo kutoka Injili ya Matayo 20, 1-7 alisema Wapendwa kaka na dada, ningependa kusimama tena juu ya mfano wa Yesu. Katika muktadha huu ni historia ambayo inalisha tumaini letu.

Katekesi Papa 4 Juni 2025
Katekesi Papa 4 Juni 2025   (@Vatican Media)

Wakati mwingine, kiukweli, tunahisi kama hatuwezi kupata maana katika maisha yetu: tunajiona, hatufai, kama vile wafanyakazi wanaongoja sokoni, wakingojea mtu awapeleke kazini. Lakini wakati mwingine wakati unapita, maisha yanasonga na hatujisikii kutambuliwa au kuthaminiwa. Labda hatukufika kwa wakati, wengine walijitokeza mbele yetu, au wasiwasi umetuweka mahali pengine. Mfano wa uwanja  wa soko pia unafaa sana kwa nyakati zetu, kwa sababu soko ni mahali pa biashara, ambapo kwa bahati mbaya upendo na heshima pia hununuliwa na kuuzwa, kujaribu kupata kitu kutoka kwao. Na wakati hatujisikii kuthaminiwa, kutambuliwa, tunahatarisha hata kujiuza kwa mzabuni wa kwanza. Badala yake Bwana anatukumbusha kwamba maisha yetu yana thamani ya kitu fulani, na hamu yake ni kutusaidia kuigundua. Hata katika mfano tunaozungumzia leo hii, kuna wafanyakazi wanasubiri mtu wa kuwaajiri kwa siku hiyo.

Tuko katika sura ya 20 ya Injili ya Mathayo na hapa pia tunapata mhusika ambaye ana tabia isiyo ya kawaida, ambaye anashangaa na kuuliza maswali. Ni mwenye shamba la mizabibu, ambaye anakwenda kutafuta wafanyakazi wake. Ni wazi kwamba anataka kuanzisha uhusiano wa kibinafsi nao. Papa kama alivyosema kwamba huo ni mfano unaotoa tumaini, kwa sababu unatuambia kuwa bwana huyu anatoka mara kadhaa kwenda kuwatafuta wale wanaongoja ili kuwapatia maana maisha yao. Bwana anatoka mara moja alfajiri na kisha, kila saa tatu, anarudi kutafuta wafanyakazi wa kuwatuma kwenye shamba lake la mizabibu. Kufuatia mlolongo huu, baada ya kuondoka saa 9 alasiri, hakutakuwa na sababu ya kwenda nje tena, kwa sababu siku ya kazi iliisha saa sita. Huyu bwana asiyechoka, anayetaka kuyapa thamani maisha ya kila mmoja wetu kwa gharama yoyote, badala yake pia anatoka saa 11. Wafanyakazi waliobaki kwenye uwanja wa soko labda walikuwa wamepoteza matumaini kabisa. Siku hiyo ilikuwa bure.

Katekesi ya Papa 4 Juni 2025
Katekesi ya Papa 4 Juni 2025   (@Vatican Media)

Papa kuhusiana na hilo aliendelea kudadavua kuwa: “Na bado kuna mtu aliyewaamini. Je, kuna maana gani kuajiri wafanyakazi kwa saa ya mwisho ya siku ya kazi pekee? Inaleta maana gani kwenda kazini kwa saa moja tu? Na bado, hata wakati inaonekana kama tunaweza kufanya kidogo maishani, inafaa kila wakati. Daima kuna uwezekano wa kupata maana, kwa sababu Mungu anapenda maisha yetu. Na hapa uhalisi wa bwana huyu pia unaonekana mwishoni mwa siku, wakati wa kulipa. Pamoja na wafanyakazi wa kwanza, wale wanaokwenda kwenye shamba la mizabibu alfajiri, bwana huyo alikuwa amekubaliana nao dinari, ambayo ilikuwa gharama ya kawaida ya kazi ya siku moja. Kwa wengine anasema kwamba atawapa haki. Na ni hapa hasa ambapo mfano huo unarudi kututia changamoto: ni nini maana ya haki? Kwa mwenye shamba la mizabibu, yaani, kwa Mungu, ni sawa kwamba kila mtu awe na kile anachohitaji kuishi. Aliwaita wafanyakazi binafsi, anajua hadhi yao  na kulingana na hilo alitaka kuwalipa. Naye aliwapatia kila mtu dinari.

Historia inasema kwamba wafanyakazi wa saa ya kwanza walikata tamaa: hawakuwezi kuona uzuri wa ishara ya bwana, ambaye hakuwa na haki, lakini kwa ukarimu tu, hakuangalia  sifa tu, bali pia kwa mahitaji. Mungu alitaka kumpatia kila mtu Ufalme wake, yaani, uhai kamili, wa milele na wenye furaha. Na hivi ndivyo Yesu anafanya nasi: yeye hafanyi viwango, kwa wale wanaomfungulia mioyo yao yeye huwapa kila kitu mwenyewe. Kwa kuzingatia mfano huu, Mkristo wa leo  hii Papa Leo alisema anaweza kujaribiwa kufikiri: "Kwa nini kuanza kufanya kazi mara moja? Ikiwa malipo ni sawa, kwa nini kazi zaidi?" Kwa mashaka hayo, Mtakatifu Agostino alijibu hivi: “Mbona basi mnakawia kumfuata yeye awaitaye, na hali mmekwisha kuwa na hakika ya thawabu, lakini hamna hakika ya siku?”

Papa Leo katika Katekesi yake
Papa Leo katika Katekesi yake   (@Vatican Media)

Wito kwa vijana “Tusingoje,bali tuitikie Bwana kwa shauku

Papa Leo katika muktadha huo alipenda  kuwambia, hasa vijana, “tusingoje, bali tuitikie kwa shauku Bwana anayetuita tufanye kazi katika shamba lake la mizabibu. Usiivue, kunja mikono yako, kwa sababu Bwana ni mkarimu na hutakata tamaa! Kwa kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu, utapata jibu kwa swali hilo muhimu ambalo unabeba ndani yako: ni nini maana ya maisha yangu?” Kwa kuhitimisha Papa aliwashauri waamini kwamba, “tusikate tamaa! Hata katika nyakati za giza za maisha, wakati unapita bila kutupa majibu tunayotafuta, tumwombe Bwana atoke tena na atufikie pale tunapomngoja. Bwana ni mkarimu na atakuja mapema!”

Baada ya Katekesi salamu kwa kiingereza

Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya Katekesi yake,, Jumatano tarehe 4 Juni 2025 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alitoa salamu mbali mbali kwa lugha kadhaa. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu akizungumza kwa Lugha ya kiingereza alisema kuwa:  â€śKaka na dada zangu wapendwa: Katika katekesi yetu inayoendelea kuhusu mada ya Jubilei ya “Yesu Kristo Tumaini Letu”, leo tunatafakari mfano wa Yesu wa watenda kazi wa saa ya mwisho (Mt 20:1-16). Mwenye shamba ambaye aliwapatia ujira uleule hata wafanyakazi wa saa kumi na moja ni mfano wa Mungu Baba yetu, ambaye hutoka mara kwa mara kuwatafuta wale wanaomjia. Upendo wake na ukarimu wake huwapatia thawabu kwa wingi wale ambao, hata hivyo wamechelewa, huitikia mwaliko wake wa kushiriki katika ufalme wake wa uzima kamili na wa milele.”

Mungu hakati tamaa juu yetu; sikuzote yuko tayari kutukubali na kutoa maana na tumaini kwa maisha yetu, hata hivyo hali yetu inaweza kuonekana isiyo na tumaini na jinsi sifa zetu zinavyoonekana kuwa duni. Na sisi sote, na hasa vijana wetu, tuwe wakarimu na wenye shauku katika kuitikia wito wake wa kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu! Papa Leo XVI kwa njia huyo amepanua makaribisho ya joto kwa wale wanahija wanaozungumza kiingereza ambao wameshiriki Katekesi hiyo na hasa kutoka England, Scotland, Ireland, Finland, Kenya, India, Indonesia, Korea, Kusini, Ufilippo na Marekani. Papa alisema “tukiwa tunajiandaa kuadhimisha Siku Kuu ya Roho Mtakatifu, kuomba juu yao na familia zao kushukiwa na zawadi ya Roho Mtakatifu juu yao na Mungu awabariki. Kwa wanahija wanaozungumza Kireno kwa namna ya pekee waliotoka   Rio de Janeiro na São Paulo! Kwa moyo mnyenyekevu uliojaa upendo kwa wote, Papa alisema “Tujibu bila shaka mwaliko wa Kristo. Ninasema hayo hasa kwa vijana: “msiwe na woga wa kufanya kazi katika shamba la Bwana! Msisite kukutana na Yule tu ambaye anaweza kutoa maana ya maisha yetu. Ninawabariki.”

Umati ndani ya Katekesi
Umati ndani ya Katekesi   (@Vatican Media)

Kwa lugha ya kiitaliano

Aliwaelekea mahujaji wa lugha ya kiitaliano wa sehemu mbali mbali za majimbo.  Aliwaomba wasichoke kujikabidhi kwa Kiristo kwa kumtangaza kwa maisha yao katika familia na katika kila mazingira. Papa aliongeza “Hilo ndilo watu hata wa sasa wanasubiri kwa Kanisa. Na kwa waamini wengine kutoka Mtakatifu Severo, Canosa wa Puglia na Altamura, aliwatia moyo kutafakari kwa kina na zaidi katika maisha ya imani, ili kuwa wahusika wakuu wa ujasiri wa matendo ya uinjilishaji katika maeneno. Aliwakaribisha kwa upenda kikundi cha ANAS na shirika la wa Orsoline wa Mtakatifu Charles wa Milano akiwahakikisha sala zake ili Bwana awajaze kila mmoja zawadi zake. Kwa kuhitimisha, mawazo ya Papa Leo yaliwaendea vijana, wagonjwa na wenye ndoa wapya. Katika muktadha wa maandalizi ya Siku kuu ya Pentekoste inayoharibia aliwashauri kuwa wapole daima kwa matendo ya Roho Mtakatifu huku wakimuomba mwana na nguvu. Aliwabariki.

Katekesi ya Papa Leo XIV
04 Juni 2025, 15:30