ĐÓMAPµĽş˝

2025.06.17 Maaskofu wa CEI na Papa Leo XIV. 2025.06.17 Maaskofu wa CEI na Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV,Maaskofu CEI Italia:mpeleke Kristo katikati ya mishipa ya ubinadamu!

Papa Leo XIV alikutana kwa mara ya kwanza na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia(CEI),Juni 17 ambapo katika hotuba yake amewashauri umuhimu wa kichungajii kuhusu mada ya amani:siyo utopia wa kiroho”aidha waelimishe kutotumia nguvu na makaribisho,haki ya kibidamu mbele ya changamoto zinazoweza kuhatarisha hadhi ya binadamu kama vile AI,teknolojia ya kibayoteknolojia,mitandao ya kijamii.Kisha alihimiza ushirikiano na mamlaka za kiraia na kusonga mbele kwenye njia ya sinodi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumanne tarehe 17 Juni 2025 kwa mara ya kwanza amekutana na Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia (CEI) ambao ni zaidi ya miambili ambapo akianza hotuba yake alionesha furaha sana ya kukutana nao. “Katika Ukumbi huu, ambao ni kati ya Basilika na Uwanja, uliojawa hisia ambazo ziliambatana na matukio ya hivi karibuni. Kiukweli, Papa lazima alikuwa avuke ili kutazama kutokea dirisha la katikati. Mpendwa Papa Francisko naye alifanya hivyo kwa ajili ya ujumbe wake wa mwisho wa Pasaka 'Urbi et Orbi,' ambao ulikuwa wito wake wa mwisho, mkali wa amani kwa watu wote. Na mimi pia, jioni ya kuchaguliwa kwangu, nilitaka kurudia tangazo la Bwana Mfufuka: "Amani iwe nanyi!" (taz. Lk 24:36; Yoh 20:19)." Kwa kuendelea na hotuba hiyo Papa Leo XIV alishukuru kwa maombi yao na yale ya jumuiya zao kwamba: "Ninayahitaji sana! Ninamshukuru sana Kardinali Zuppi, pia kwa maneno aliyoniambia. Nawasalimu Makamu wa Rais watatu, Katibu Mkuu na kila mmoja wenu."

Maaskofu wa CEI
Maaskofu wa CEI   (@Vatican Media)

Historia ya Kanisa nchini Italia inaakisi uhusiano maalum unaowaunganisha na Papa na ambao - kulingana na Mkataba wa CEI - "unastahili kwa namna fulani ushirika wa Baraza  na Papa wa Kirumi" (Kifungu cha 4 § 2). Kufuatia mfano wa watangulizi wangu, mimi pia ninahisi umuhimu wa uhusiano huu wa "kawaida na maalum", kama Mtakatifu Paulo VI alivyofafanua alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa kwanza wa CEI (Hotuba, 23 Juni 1966). Katika kutekeleza huduma yake pamoja nao ndugu wapendwa, Papa Leo alitaka kupata msukumo kutoka katika kanuni za umoja, ambazo ziliendelezwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Hasa, katika hati ya Christus Dominus ambayo inasisitiza kwamba Bwana Yesu alifanya Mitume "kama Baraza imara au kundi, ambalo aliweka Petro, aliyechaguliwa kutoka kati yao, na kuwa kichwa" (n. 19). Ni kwa njia hiyo wanaitwa kuishi huduma yao: ushirikiano kati yao na ushirikiano na mrithi wa Petro.” Kanuni hii ya ushirika pia inaonekana katika ushirikiano mzuri na mamlaka ya kiraia. CEI kwa hakika ni mahali pa ulinganisho na mjumuiko wa mawazo ya Maaskofu juu ya masuala muhimu zaidi kwa manufaa ya wote. Inapobidi, inaongoza na kuratibu mahusiano ya Maaskofu binafsi na Mabaraza ya Maaskofu ya kikanda na mamlaka hizi katika ngazi mahalia..

Papa Benedikto wa kumi na sita, mwaka 2006, alilielezea Kanisa nchini Italia kama "ukweli wa kusisimua sana, [...] ambao unadumisha uwepo ulioenea kati ya watu wa umri na hali zote" na ambapo "tamaduni ya Kikristo mara nyingi bado ina mizizi na inaendelea kuzaa matunda" (Hotuba kwa Mkataba wa IV wa Kitaifa wa Kanisa, 19 Oktoba 2006). Hata hivyo, jumuiya ya Kikristo ya nchi hii kwa muda mrefu imelazimika kukabiliana na changamoto mpya, zinazohusishwa na usekula, hali fulani ya kutopendezwa na imani na mgogoro wa kupungua kwa idadi ya watu. Katika muktadha huo - Papa Francisko alibainisha kuwa  â€śtunaombwa tuwe wajasiri ili kuepuka kuzoea hali ambazo zimekita mizizi kiasi kwamba zinaonekana kuwa za kawaida au zisizoweza kushindwa. Unabii - alisema - hauhitaji mapumziko, lakini uchaguzi wa ujasiri, ambao ni sahihi kwa jumuiya ya kweli ya kikanisa: yanapelekea kujiruhusu "kusumbuliwa" na matukio na watu na kujitumbukiza katika hali za kibinadamu, zinazohuishwa na roho ya uponyaji ya Heri" (Hotuba katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 70 wa CEI, 22 Mei 2017).

Maaskofu wa Italia
Maaskofu wa Italia   (@Vatican Media)

Kwa nguvu ya dhamana ya upendeleo kati ya Papa na Maaskofu wa Italia, aidha Papa alipenda kuonesha wasiwasi fulani wa kichungaji ambao Bwana anaweka mbele ya njia yetu na ambao unahitaji tafakari, hatua thabiti na ushuhuda wa kiinjili. Kwanza kabisa, msukumo mpya unahitajika katika kutangaza na kusambaza imani. Ni suala la kumweka Yesu Kristo katikati na, katika njia iliyooneshwa na Evangelii gaudium, kuwasaidia watu kuishi uhusiano wa kibinafsi naye, kugundua furaha ya Injili. Katika wakati wa mgawanyiko mkubwa ni muhimu kurudi kwenye misingi ya imani yetu, kwa kerygma. Hii ndiyo dhamira kuu ya kwanza inayowapa motisha wengine wote: kumleta Kristo “katika mishipa” ya ubinadamu (rej. Katiba ya Kitume Humanae salutis, 3), kujipyaisha na kushiriki utume wa kitume: “Lile tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi pia” (1 Yh 1:3).

Na ni jambo la kupambanua njia za kupeleka Habari Njema kwa kila mtu, kwa matendo ya kichungaji yenye uwezo wa kuwazuia wale walio mbali zaidi na kwa zana zinazofaa kwa ajili ya kufanya upya katekesi na lugha za tangazo. Uhusiano na Kristo hutuita kukuza mtazamo wa kichungaji juu ya mada ya amani. Bwana, kiukweli, anatutuma katika ulimwengu kupeleka zawadi yake mwenyewe isemayo: "Amani iwe nanyi!", na kuwa mafundi wake katika maeneo ya maisha ya kila siku. Nafikiria parokia, vitongoji, maeneo ya ndani ya nchi, mijini na pembezoni. Pale ambapo mahusiano ya kibinadamu na kijamii yanakuwa magumu na migogoro inapotokea, labda kwa njia ya hila, Kanisa lenye uwezo wa upatanisho lazima lijidhihirishe. Mtume Paulo anatuhimiza hivi: “Ikiwezekana, kwa kadiri inavyowategemea ninyi, kaeni kwa amani na watu wote” ( Rm 12:18 ); ni mwaliko unaomkabidhi kila mtu sehemu madhubuti ya wajibu.

Maaskofu wa Italia
Maaskofu wa Italia   (@Vatican Media)

Ni matumaini, basi, kwamba kila Jimbo linaweza kukuza kozi za elimu katika kutokuwa na vurugu, mipango ya upatanisho katika migogoro ya ndani, kukaribisha mipango ambayo inabadilisha hofu ya mwingine kuwa fursa ya kukutana. Kila jumuiya inakuwa "nyumba ya amani", ambapo mtu hujifunza kupunguza uhasama kwa njia ya mazungumzo, ambapo haki inatendeka na msamaha unalindwa. Amani sio utopia wa kiroho: ni njia ya unyenyekevu, inayofanywa kwa ishara za kila siku, ambayo huingiliana na uvumilivu na ujasiri, kusikiliza na kutenda. Na ambayo leo, zaidi ya hapo awali, inahitaji uwepo wetu wa mtazamo na wa uzalishaji. Kisha kuna changamoto zinazotaka kuheshimiwa kwa utu wa binadamu. Akili Nunde, teknolojia ya kibayoteknolojia, uchumi wa data na mitandao ya kijamii zinabadilisha sana mtazamo wetu na uzoefu wetu wa maisha.

Katika hali hii, hadhi ya binadamu iko hatari ya kuwa bapa au kusahaulika, kubadilishwa na kazi, kimashinde. Lakini mtu sio mfumo wa mashine: yeye ni kiumbe, ana uhusiano, na fumbo. Kwa hiyo Papa Leo XIV alipenda kueleza matumaini: kwamba njia ya Makanisa nchini Italia ijumuishe, katika ulinganifu thabiti na ukuu wa Yesu, maono ya kianthropolojia kama nyenzo muhimu ya utambuzi wa kichungaji. Bila kutafakari kwa uchangamfu juu ya mwanadamu - katika umbile lake, katika mazingira magumu, katika kiu yake ya kutokuwa na kikomo na uwezo wa kuunganishwa - maadili yatapunguzwa kwa kanuni na hatari za imani kuwa tofauti. Papa Leo XIV alipendekeza hasa kukuza utamaduni wa mazungumzo. Inapendeza kwamba mambo yote ya kikanisa - parokia, vyama na harakati – viwe  nafasi za kusikiliza kati ya vizazi, kwa kulinganisha na ulimwengu tofauti, kwa utunzaji wa maneno na uhusiano. Kwa sababu ni pale tu ambapo kuna kusikiliza ndipo ushirika unaweza kuzaliwa, na ni pale tu ambapo kuna ushirika ukweli huweza kusadikika. Papa alihimiza kuendelea kwenye njia hiyo!

Maaskofu wa Italia
Maaskofu wa Italia   (@Vatican Media)

Utangazaji wa Injili, amani, utu wa binadamu, mazungumzo: hivi ndivyo viratibu ambavyo wanaweza kuwa Kanisa linalomwilisha Injili na ni ishara ya Ufalme wa Mungu. Kwa kumalizia, Papa alipendelea kuwapa ushuri kwa siku za usoni. Kwanza: kusonga mbele kwa umoja, hasa tukifikiria kuhusu Njia ya Sinodi. Bwana - anaandika Mtakatifu Augustino - "huweka mwili wake vizuri na kwa amani, hivyo huhutubia Kanisa kwa kinywa cha Mtume: Jicho haliwezi kuuambia mkono: Sina haja nawe; au vivyo hivyo kichwa kwa miguu: Sina haja na ninyi. Kama mwili wote ungekuwa macho, kusikia kungekuwa wapi? Kama mwili wote ungesikia, hisia ya kunusa ingekuwa wapi?" (Ufafanuzi wa Zaburi 130, 6). Kaeni na umoja na msijilinde kutokana na uchochezi wa Roho. Sinodi na iwe mawazo, moyoni, katika michakato ya kufanya maamuzi na katika njia za kutenda. Papa Leo XIV kwa kufafanua sehemu ya pili alieleza kuwa ni ile ya kutazama ya kesho kwa utulivu na wasiogope uchaguzi wa ujasiri! Hakuna anayeweza kukuzuia kuwa karibu na watu, kushiriki maisha, kutembea na wadogo, kuwatumikia maskini.

Hakuna anayeweza kukuzuia kutangaza Injili, na ni Injili ambayo tumetumwa kupeleka, kwa sababu hii ndiyo ambayo sisi sote, sisi wenyewe kwanza, tunahitaji kuishi vizuri na kuwa na furaha. Kuhakikisha kwamba waamini walei, wanaolishwa na Neno la Mungu na kujengwa katika mafundisho ya kijamii ya Kanisa, ni wahusika wakuu wa uinjilishaji mahali pa kazi, shuleni, hospitalini, katika mazingira ya kijamii na kitamaduni, katika uchumi, na katika siasa. Papa Leo XIV amewasihi kutembea pamoja, kwa furaha mioyoni mwao na wimbo kwenye midomo yao. Mungu ni mkuu kuliko hali yetu ya wastani: tujiruhusu kuvutiwa naye! Tutegemee majaliwa yake. Amewakabidhi wote kwa ulinzi wa Maria Mtakatifu zaidi: Mama Yetu wa Loreto, wa Pompeii na wa madhabahu mengi yasiyohesabika yaliyozunguka Italia. Anawasindikiza kwa sala na baraka zake.

Papa na maaskofu wa CEI

 

17 Juni 2025, 14:20