Nia za Baba Mtakatifu kwa Mwezi Juni 2025:Na ili tukue katika huruma kwa Ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tunachapisha video ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa mara ya kwanza katika kiingereza kwa nia ya sala ya Baba Mtakatifu kwa ajili ya mwezi Juni 2025 iliyosambazwa tarehe 3 Juni 2025 kwa njia ya Mtandao wa Maombi Kimataifa ya Papa, kuhusu mada: “ili kukua katika huruma kwa ajili ya Ulimwengu: Tuombe ili kila mmoja apate faraja katika uhusiano kibinafsi na Yesu na kujifunza kutoka katika Moyo wake huruma kwa Ulimwengu. Katika mwezi ambao kwa kiutamaduni ni mwezi wa Ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Baba Mtakatifu Leo anawashauri waamini kwa hakika kujua kibinafsi Moyo wa Kristo kwa namna ya kuuneza kwa wote na kuwafariji hasa wale wanaoteseka katika Ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, ukosefu wa usawa na umaskini.
Sala Kamili ya Papa Leo XIV kwa nia za Juni 2025:
“Bwana, leo ninakuja kwenye moyo wako mwororo: kutoka kwako wew mwenye maneno yanayowasha moyo wangu, kutoka kwako unamimina huruma juu ya wadogo na maskini, juu ya wale wanaoteseka na juu ya taabu zote za ubinadamu. Ninatamani kukujua zadi, kukutafakari katika Injili, kukaa nawe na kujifunza kutoka kwako na kutoka katika upendo ambao uliacha uguswe na kila mtindo wa umaskini. Ulituonesha upendo wa Baba kwa kutupenda bila kipimo, kwa upendo wake, wa kimungu na kibinadamu. Utujalie sote watoto wako neema ya kukutana nawe. Ubadili, uunde na kubadili mipango yetu, ili tuweze kukutafuta wewe tu, kwa kila hali: katika sala, katika kazi, katika mikutano na katika maisha yetu ya kila siku. Kutoka katika mkutano huu, ututume katika utume: utume wa huruma kwa ulimwengu ambamo wewe ni chanzo ambacho kinabubujika kila faraja. Amen.”
Papa Leo XIV anatuhimiza upendo na huruma ya Yesu
Mjesuit Padre Cristóbal Fones, Mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Nia za Maombi ya Papa Ulimwenguni Pote, alitoa maoni yake juu ya maneno ya Papa Leo XIV, huku akisisitiza jinsi gani kupitia uhusiano wa kibinafsi na Yesu, moyo wa kila mtu unafanana zaidi na ule wa Kristo na mtu hujifunza huruma ya kweli kwa wengine. Padre Fones, alieleza kuwa "Yesu alionesha upendo usio na masharti kwa wote, hasa maskini, wagonjwa, na wale wanaoteseka. Papa anatuhimiza kuiga upendo huu wa huruma kwa kuwafikia wale walio katika magumu." Huruma inatafuta kupunguza mateso na kukuza hadhi ya binadamu." Kwa sababu hiyo, inatafsiriwa katika hatua madhubuti ambazo zinalenga kuondoa mizizi ya umaskini, ukosefu wa usawa, na kutengwa, kuchangia katika kujenga dunia yenye haki zaidi na inayounga mkono." Mjesuit pia alikazia jinsi ambavyo kazi ya Mtandao wa Nia ya Maombi ya Papa Duniani inavyoendana na Mwaka wa Jubilei ambamo pamoja na mambo mengine ni lazima kuombea nia ya Papa na kupata neema ya msamaha wa Jubilei.
Ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ilikuzwa katika karne ya 17 na ufunuo kwa Mtakatifu Margaret Maria Alacoque na tafsiri yake na Mjesuit Mtakatifu Claude de La Colombière. Papa Pio IX alitangaza sikukuu ya Moyo Mtakatifu kunako mwaka 1856 na baadaye, Papa Leo XIII, ambaye Baba Mtakatifu wa sasa alichukua jina lake, aliimarisha umuhimu wake kwa kuinua hadi 1889. Kisha aliandika Waraka wa Annum sacrum mwaka 1899 ambamo aliweka wakfu wanadamu wote kwa Moyo wa Yesu. Mapapa mbalimbali, kama vile Pio XI na Pio XII, wamejitolea nyaraka zao kwa ibada hii. Na hivyo karibuni zaidi mnamo 2024, Papa Francisko alichapisha Waraka wa Dilexit Nos,(,)ambamo alipendekeza Moyo wa Kristo kama jibu la kupinga utamaduni wa kutupa na kutojali.