MAP

Daktari Carbone. Daktari Carbone.  (ANSA)

Papa Leo XIV amteua Dk.Carbone kuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Afya,Vatican!

Baba Mtakatifu amemteua Dk.Luigi Carbone kuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Afya na Usafi,Vatican.Hadi uteuzi huo alikuwa naibu mkurugenzi wa chombo hicho kinachotoa ulinzi wa usafi na afya ya umma katika eneo la mji wa Vatican na ataanza wadhifa huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2025.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jummne tarehe 2 Juni 2025 amemteua Dk. Luigi Carbone kuwa mkurugenzi wa Idara ya Afya na Usafi wa Mji wa Vatican, chombo chenye jukumu la kuhakikisha ulinzi wa usafi na afya ya umma mjini Vatican. Hadi uteuzi wake alikuwa ni naibu mkurugenzi wa idara hiyo hiyo, Dk. Carbone, ambaye alikuwa daktari wa rufaa wa Papa Francisko na kumfumsindikiza Papa wakati wa ugonjwa wake, atashika wadhifa huo  kuanzia tarehe 1 Agosti 2025. Anachukua nafasi ya Profesa Andrea Arcangeli, ambaye amekuwa mkurugenzi tangu tarehe 1 Agosti 2020 na ambaye anatimiza miaka 70 mwezi huu.

Profesa Arcangeli na Dk. Carbone kitaaluma wanatoka katika mazingira sawa ya hospitali ya Gemelli, ambako walikutana miaka 25 iliyopita. Katika mahojiano yaliyochapishwa kwenye tovuti ya Mji wa Vatican kwanza alisema aliitwa Vatican "katika hafla ya Jubilei Kuu kwa ajili ya usimamizi wa dharura za matibabu" na kwamba "katika muktadha huo, kikundi cha wafufuaji kiliundwa", baadaye kilichotakwa na mkurugenzi wa wakati huo Renato Buzzonetti, kulinda afya ya Yohane  Paul II. Mnamo tarehe 1  Aprili  2019 Arcangeli aliteuliwa kuwa naibu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi, wakati wa mwelekeo wa Profesa Alfredo Pontecorvi, mkurugenzi mnamo tarehe 1 Agosti 2020. Kati ya wakati muhimu sana anakumbuka 2020, katika kipindi cha janga la Uviko-19  wakati "dhamira ya kushangaza ilikuwa muhimu", na kisha "shirika la mfumo wa chanjo."

Profesa Arcangeli alifafanua kwamba "katika miaka ya hivi karibuni, shukrani kwa msaada wa ukarimu wa Mkuu wa Mji wa Vatican, vifaa vingi vya afya vimesasishwa, kwa mfano radiolojia na scanner zote za ultrasound zinazotolewa kwa usimamizi, zinazotumiwa katika (radiolojia,)picha ,  magonjwa ya moyo, magonjwa ya uzazi na angiolojia" na "huduma zingine, kama vile (physiotherapy),mazoezi ya viungo zimepanuliwa na "saikolojia mpya" imepanuliwa na "saikolojia ya Mwaka" imepanuliwa vifaa vimenunuliwa, hasa, magari ya wagonjwa mawili ya kizazi kipya."

Kwa upande wake, Dk. Carbone alibainisha kuwa “kutokana na miongozo ya hivi karibuni iliyotolewa na Vyombo vya Serikali, umuhimu unatolewa kwa usalama wa wafanyakazi” na kwamba Kurugenzi ya Afya na Usafi “inaundwa na wataalamu wengi ambao kila siku wanaitwa kutoa ujuzi wao katika nyanja mbalimbali”. "Kupokea uteuzi wa upapa ni, kwanza kabisa, heshima kubwa," anasema. "Mtu huona uzito wa kazi aliyokabidhiwa, inayohusishwa na nafasi ya umuhimu huo, pamoja na hisia ya kina ya shukrani kwa uaminifu ambao Baba Mtakatifu ametaka kutoa." "Kuitwa kutekeleza kazi hiyo nyeti moja kwa moja na Papa," anahitimisha, "kunahitaji umakini, heshima na uwajibikaji mkubwa unaostahili uaminifu uliowekwa ndani yako na Baba Mtakatifu."

02 Juni 2025, 19:46