Papa Leo XIV awatembelea Jumuiya ya Mtakatifu Agostino kwa siku ya kuzaliwa kwa Mkuu wa Shirika!
Vatican News
Baada ya Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Jubilei ya familia, watoto, babu, bibi na wazee, Baba Mtakatifu Leo XIV, Dominika tarehe 1 Juni 2025 aliwafikia jumuiya ya kitawa, kupitia njia ya Paolo VI; ambapo wanafunzi wa Shirika la Mtakatifu Agustino kutoka nchi mbalimbali duniani na baadhi ya walimu wa Taasisi ya Kipapa la Baba wa Kanisa wanaishi, kushiriki katika hafla iliyoandaliwa kuadhimisha miaka 70 ya kuzaliwa kwa Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino Padre Alejandro Moral.
Njia Sambamba
Urafiki wa muda mrefu unawafunga Papa na Padre Alejandro, mzaliwa wa La Vid, Hispania, tarehe 1 Juni 1955. Wawili hao walikutana miaka ya 1980 jijini Roma, katika Chuo cha Mtakatifu Monica, walipokuwa wakisoma Sheria kwa Provost, katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas wa Aquinas na Taasisi ya Maandiko Matakatifu ya Maadili katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoriana. Njia zao zilitengana mwaka 1985, pale ambapo Padre kijana Robert, aliyepewa daraja la Upadre mwaka 1982, alipotumwa kwenye utume wa Kiagostiniani, Chulucanas, huko Piura, Peru, wakati Padre Alejandro alipomaliza masomo yake akarejea Hispania. Watu hao wawili walikutana tena jiji Roma mwaka wa 2001, kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Waagostiniani.
Njia tofauti, dhamana iliyobaki
Alipochaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika, Padre Prevost alimchagua Moral kama makamu na akimthibitisha pia katika muhula wake wa pili. Kwa miaka 12 walifanya kazi bega kwa bega na urafiki wao ukukua na kuimarika. Uhusiano wa kidugu ambao unadumu hata wakati njia zao zimegawanyika tena. Mnamo mwaka wa 2013, mwishoni mwa muhula wa pili wa miaka sita kuwa Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino, Padre Prevost alirudi katika kanda yake ya kiagostino huko Chicago, wakati Padre Moral akateuliwa kuwa Mkuu wa 97 Shirika shirika hilo.
Na ikiwa mwaka mmoja baadaye Padre Robert Prevost aliteuliwa na Papa Francisko kuwa msimamizi wa kitume wa jimbo la Chiclayo, nchini Peru, na baadaye kuteuliwa kuwa Askofu na wakati huo upendo wa kiagostiniani ulibaki kwa Padre Alejandro, urafiki huo uliosifiwa sana na Baba wa Kanisa Agostino aliyependa maisha ya pamoja katika: “umoja wa akili na moyo” (Utawala)“kutafuta pamoja, kwa upatanisho kamili” na Mungu, ili yeyote aliyeipata ukweli kwanza aweze kuwaongoza wengine ....." ( Maandiko ya Mtakatifu Agostino Solil. 1, 12, 20-13, 22.)